Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kuzikwa tarehe 2 badala ya siku ya kesho ndani ya masaa 24 ni kukiuka mazishi ya kiislam. Napendekeza ratiba ibadilishwe

Uncle bright

JF-Expert Member
Feb 9, 2023
1,040
4,080
Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kafariki saa 11 na nusu jioni ya leo tarehe 29/2/2024 hivyo kwa taratibu za kiislam inabidi azikwe kesho 01/03/2024 kabla ya saa 11 na nusu jioni, ikipendeza zaidi ilibidi iwe kesho asubuhi au mchana


Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayra رضى الله عنه akisema: Amesema Mtume ﷺ : “Harakisheni mazishi! Kwani kama maiti ni mja mwema basi haifai kumchelewesha, na kama ni mja muovu basi ni shari na balaa mnaweka mabegani mwenu.
Muttafaq Alayhi.

951. Imepokewa kutoka kwa Huswayn bin Wahwah akisema: “Aliumwa Twalha bin al-Baraa’ bin ‘Azib akatembelewa na Mtume nyumbani kwake. Baada ya kumuona, alisema: “Naona mwisho wa maisha ya Abu Twalha unakaribia, hivyo akifariki nijulisheni, na harakisheni kumtayarisha kumzika; kwani haifai kuachwa mzoga wa mwili wa Mwislamu kusalia nyumbani na familia yake” Ameipokea Abu Daud.
 
Unaweza kuweka angalau aya au kifungu cha sheria hiyo ya kiislam kuipa nguvu hoja yako. Mambo ya imani yanataka vyanzo sio utamaduni.

Kwa ufahamu wangu huo ni utamaduni wa watu wa mashariki ya kati, waarabu na wayahudi. Ndio maana Yesu, Anania na Safira, watu wa mashariki ya kati walizikwa ndani ya 24hrs. Ni utaratibu ninaoupenda maana unasaidia kumpunguzia aliye hai machungu.
Mwanadamu ni mavumbi arudishwe mavumbini alikotoka kwa wepesi.
 
Back
Top Bottom