Hayati Magufuli alikuwa Nabii katika angle zifuatazo

Salaam, Shalom!!

Tunapoelekea katika kumbukumbu ya kukumbuka miaka 3 ya Mzalendo Magufuli,

Tujikumbushe misimamo yake iliyolivusha Taifa huku akiwaacha mbali viongozi wa Dini na Viongozi wa Vyama vya siasa na Dunia Kwa ujumla.

Sisi tusiokuwa na vyama tulikaa katikati na kupima upi Hasa ulikuwa ushauri wenye maslah ya Wananchi.

Viongozi wa Dini walikuwa tayari KUFUNGA nyumba za Ibada kuogopa corona, Magu akasema HAPANA msifunge, twendeni tukamwombe Mungu atatusaidia, na Kweli tukavuka salama.

Wanasiasa wa Upinzani walishauri tupigwe LOCKDOWN, Magu akagoma, akatoa HOJA kuwa wananchi wengi ni deiwaka, wasipotoka, familia haijala, na huo ndio ulikuwa UKWELI, maana Nchi zingine, watu walivunja Sheria ya lockdown Ili wakatafute chakula wakidai ni Afadhali kufa Kwa korona Ukiwa umeshiba, kuliko kufa Ukifa njaa umefungiwa.

Mwanasiasa mmoja, Mwenyekiti wa chama Cha upinzani akatoa wazo na kutaka wanaokaidi Chanjo, wakamatwe, wapingwe pingu na kuchanjwa Kwa lazima.

Wazo la kuhamisha IKULU Toka Dar Magogoni kwenda Dodoma, yalikuwa ni maono makubwa.

Kuanza mradi wa JNHP pia yalikuwa ni maono mema Kwa Taifa.

Kwa uchache, Itoshe kusema, Kwa Muda Mchache Mungu aliompa Magu kuwa Rais, Kweli alifanya KAZI iliyotukuka, mapungufu yake kama mwanadamu tuhakikishe hatuyafuati.

Ahsante Mungu Kwa zawadi ya Nabii Magufuli.

Amen
Halafu anakuja mpuuzi/mpumbavu mmoja anamsema vibaya Hayati kwa ujira wa buku 7 au tamaa ya cheo!
 
Huwa unafanya makosa sana kumpa mtu kichwa chako akuwazie badala yako. Hao hao unaowaamini ndio hao hao waliowatangezieni kuwa malaika wenu yuko fiti na anachapa kazi kumbe Bwana ashatwaa siku mingi sana. Tumia kichwa chako vizuri na sio ukigeuze kama kifaa cha kubebea meno!
Hivi ndugu yangu kwa akili ya kawaida kiongozi wa nchi afe hivi unadhani wanatangaza tu kienyeji kama anavyofariki bibi yako? Tumia akili kuwaza
 
Rabbon hafungwi na pingu za uchama linapokuja suala lenye maslah mapana ya Taifa.

Kwa Kweli mlipuko wa corona uliikuta Tanzania ikiwa strong chini ya Magufuli.

Mtu yule aliipenda nchi yake.

Katika hili la Corona nitasimama na UKWELI.

Mungu alimsaidia atuvushe.
Baadhi ya mambo machache sana niliyoona dhalimu magu alifanya sawa, ni kutotuweka lockdown. Na angetuweka lockdown, chuki yangu kwake ingezidi kuwa kubwa.
 
Hivi ndugu yangu kwa akili ya kawaida kiongozi wa nchi afe hivi unadhani wanatangaza tu kienyeji kama anavyofariki bibi yako? Tumia akili kuwaza
Mbona Sokoine alivyofariki walitangaza siku hiyo hiyo? Ni kweli hizo ni protocol, lakini hazina maana sana.
 
Salaam, Shalom!!

Tunapoelekea katika kumbukumbu ya kukumbuka miaka 3 ya Mzalendo Magufuli,

Tujikumbushe misimamo yake iliyolivusha Taifa huku akiwaacha mbali viongozi wa Dini na Viongozi wa Vyama vya siasa na Dunia Kwa ujumla.

Sisi tusiokuwa na vyama tulikaa katikati na kupima upi Hasa ulikuwa ushauri wenye maslah ya Wananchi.

Viongozi wa Dini walikuwa tayari KUFUNGA nyumba za Ibada kuogopa corona, Magu akasema HAPANA msifunge, twendeni tukamwombe Mungu atatusaidia, na Kweli tukavuka salama.

Wanasiasa wa Upinzani walishauri tupigwe LOCKDOWN, Magu akagoma, akatoa HOJA kuwa wananchi wengi ni deiwaka, wasipotoka, familia haijala, na huo ndio ulikuwa UKWELI, maana Nchi zingine, watu walivunja Sheria ya lockdown Ili wakatafute chakula wakidai ni Afadhali kufa Kwa korona Ukiwa umeshiba, kuliko kufa Ukifa njaa umefungiwa.

Mwanasiasa mmoja, Mwenyekiti wa chama Cha upinzani akatoa wazo na kutaka wanaokaidi Chanjo, wakamatwe, wapingwe pingu na kuchanjwa Kwa lazima.

Wazo la kuhamisha IKULU Toka Dar Magogoni kwenda Dodoma, yalikuwa ni maono makubwa.

Kuanza mradi wa JNHP pia yalikuwa ni maono mema Kwa Taifa.

Kwa uchache, Itoshe kusema, Kwa Muda Mchache Mungu aliompa Magu kuwa Rais, Kweli alifanya KAZI iliyotukuka, mapungufu yake kama mwanadamu tuhakikishe hatuyafuati.

Ahsante Mungu Kwa zawadi ya Nabii Magufuli.

Amen
Huwa nawaza sana hivi ile CORONA ingetukuta chini ya utawala wa Mama Kizimkazi,ingekuaje!!
 
Back
Top Bottom