Saikosisi
JF-Expert Member
- May 4, 2007
- 528
- 31
Mambo ya kusikitisha yanayotokea BongoTZ, je tutaendelea kweli?
1. Mafisadi wanajitahidi kutuwekea mabomba ya maji ingawa ni kwa spidi ndogo lakini wauza maji (ya mkokoteni) wanakata mabomba hayo ili kuwe na uhaba wa maji wao wauze yao kwa bei ya juu!
2. Tanesco nao wametuletea umeme hadi huku mabondeni, vibaka wanakata na kuiba nyaya (sijui wanaenda kuzifanyia nini!). Tena hao vibaka nao wanakaa maeneo haya haya!
3. Hayo hayo ya umeme wengine wanaiba mafuta ya transforma kwenda kukaangia chips!
4. Madereva wa magari makubwa wanasababisha ajali kwa makusudi (kuzifanyizia gari ndogo ama mabasi ya abiria) eti watu wakifa ni kafara mambo yao yatakuwa mazuri! Sawa na wale wanaoua albino au kuchuna watu ngozi ama kuchukua viungo vingine!
5. Ukisahau simu kwenye taxi (tena mnafahamiana na taxi driver) hauipati tena, au hata hotelini ambapo umefikia kwa siku 2, 3 ukiacha simu mezani unakuta imetembea!
Je, tutaendelea kweli na attitude zetu hizi?
Suluhisho ni nini kwa mambo haya?
Masuala ya uaminifu yawe yanafundishwa mashuleni kuanzia msingi na kuendelea au?
Au wananchi wenye hasira kali waongeze kasi?