Haya ni machache kati ya mengi niliyoyasikia au kuyaona kutoka kwa maustaz, wachungaji na waganga wa kienyeji. Je, na wewe ushashuhudia lipi?

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu zangu katika nchi yetu kuna watu wamekuwa wakisabishiwa, au kusababisha wenyewe vifo vya ndugu zao bila wenyewe kujijua kutokana na imani zao, au mawazo yao. Hapo chini ni matukio mawili kati ya mengi ambayo nimeyashuhudia mimi mwenyewe.

1. Mnamo mwishoni mwa miaka ya 90, tulikuwa na jirani yetu ambae alianza kuugua ugonjwa ambao haikuwa rahisi mtu yeyote kuufahamu. Ugonjwa huu ulikuwa unamnyima mgonjwa hamu ya kula, kuoga, kukaa, kulalala nk. Mbaya zaidi hata kumpa mumewe haki ya ndoa ilikuwa ugomvi.

Kwa vile mgonjwa huyo alikuwa ametoka kufiwa na mtoto wake miezi kadhaa kabla ya ugonjwa, basi watu wengi haswa ndugu, jamaa na marafiki wakaunganisha ugonjwa huo na swala la kuondokewa na mwanae, hivyo wakajipa moyo kwamba mgonjwa wao akipatiwa watu au mtu wa kukaa nae karibu kwa lengo la kumliwaza, kumfariji na kumtoa katika mawazo ya kufiwa basi atakuja kuwa sawa kama zamani, hivyo wifi yake mmoja na mdogo wake wakachukua jukumu la kukaa nae. Ilikuwa ni familia inayojiweza maana mgonjwa alikuwa ni mwl mkuu katika shule fulani jijini Dar es Salaam, na mumewe alikuwa ni afisa wa jeshi mwenye nyota tatu, hivyo nyumba waliokuwa wanaishi ilikuwa kubwa na watoto wawili tu, mmoja alipofariki akabaki mmoja, hivyo swala la ndugu hao kubaki hapo halikuiathiri familia hiyo kiuchumi.

Bahati mbaya kila muda ulivyokwenda ndo hali ya mgonjwa ilivyozidi kuwa mbaya zaidi, ikabidi familia impeleke mgonjwa hospital ila Kwa vipimo vya wakati huo hawakuweza kuona tatizo linalomsumbua haraka. Ikashauriwa tu kwamba mgonjwa anatakiwa aendelee kuwa anapewa msaada wa kisaikolojia chini ya wanafamilia na ikiwezekane ajazwe imani kupitia dini yake ili aamini kwamba swala la kufiwa ni la kila mtu, Mungu anapoamua kuchukua kiumbe chake basi hamna haja ya kuendelea kusononeka sana kwani huenda leo amechukua mtoto mmoja, kesho akakupa wengine watatu nk.

Walivyoona hakuna kinachobadilika, ikabidi waende kutafuta maombi kwa mchungaji mmoja aliekuwa na jina kubwa miaka ya 90 (jina kapuni), mchungaji baada ya kuhadithiwa kilichomsibu mgonjwa, akawambia kwamba mgonjwa wao ametupiwa pepo mchafu (jini) na mwenzake ambae walikuwa wanafanya nae kazi ya ualimu shuleni. Na kwamba lengo la mwl huyo kumtupia mwenzake pepo, ni kutaka mgonjwa huyo afukuzwe kazini hapo ili yeye akaimu na hatimae kuchukua nafasi yake.

Familia hiyo nikimaanisha mgonjwa na mumewe walikuwa na nyumba tatu Dar es salaam. Nyumba moja ilikuwa mbezi beach, nyumba ya pili tabata makuburi na ya mwisho ambayo ndio walikuwa wanaishi ilikuwa Kagera "kimamba". Walifanyiwa maombi na mchungaji huyo Kwa muda mrefu bila mafanikio. Mara maji ya upako, mara usiku wa maombi na mazingaombo mengine kibao bila mafanikio yoyote, walishtuka wameuza nyumba zao mbili yani ile ya Mbezi Beach na Tabata.

Hela zote zikaishia katika mifuko ya mchungaji. Baadae ndo wakashtuka na kuamua kumpeleka katika hospital kubwa kwa ajili ya vipimo zaidi, baada ya kufanyiwa vipimo kwa kina ikagundulika kwamba ana tatizo katika mishipa ya fahamu. Inasemekana aliwahi kupata ajali udogoni akatibiwa akapona, ila baada ya kufiwa ile hali ilirudi tena ghafla hivyo ilitakiwa wamuwahishe hospital haraka kwa ajili ya vipimo vya kina na matibabu, so kwa bahati mbaya familia hawakulifikiria hilo, hali iliyopelekea kwenda kutapeliwa na mchungaji niliesema hapo juu.

Yule mama alipatiwa tiba japo hakupona kabisa kutokana na wahusika kuchelewa kumpeleka hospital kubwa kupata vipimo na tiba, lkn kwa kiasi kikubwa alikuwa na unafuu ukilinganisha na tiba alizopata maombini. Yule mama alifariki miaka ya baadae kidogo kwa sababu ya mshituko wa moyo.

2. Huyu ni msichana ambae mama yake alipanga kwetu. Huyu msichana alikuwa anafanya kazi saluni fulani ya kariakoo. Alianza kuumwa ghafla, ikabidi wakampeleka hospital akapatiwa dawa, ila bado hakuonesha dalili ya kupona. Huyu pia alikuwa amepoteza hamu ya kula, upungufu wa damu na nguvu mwilini, kutapika kila wakati. Nao walivyoona hali imezidi wakampeleka kwa sangoma, sangoma akachezesha tunguli na kuja na jibu kwamba binti karogwa na mwanamke fulani ambae alipata taarifa kuwa binti huyo anatembea na mumewe, kwahiyo ili kumkomoa akaamua kumtupia jini ili limnyonye damu na ikiwezekana limuue kabisa. Ndugu kusikia vile wakataka msaada zaidi kutoka kwa mganga ili binti yao apone. Wakamwambia mganga wapo tayari kumpa kiasi chochote cha pesa ili aokoe maisha ya mtoto, ndugu yao.

Mganga kusikia vile basi akaona hapa hapa, akawa anawapa miti, majani na kombe mbali mbali sijui ile miti eti ni ya kuchoma ndani kufukuza majini, majani wanaambiwa wachemshe na kumnywesha mgonjwa ili jini hilo likose sehemu ya kuishi katika mwili huo, kombe nalo aogee ili kusafisha mwili na kuondoa nuksi nk.

Wakalipishwa hela nyingi sana kwa ajili ya miti, majani na kombe bila mgonjwa wao kupata nafuu. Akatokea ndugu mmoja akashauri binti apelekwe kwa ustazi kupata dua.

Kweli bwana, familia hiyo hadi kwa ustaz fulani wa magomeni Mikumi. Ostaz nae alipopewa taarifa za mgonjwa akadai huenda binti alikumbana na kitu kibaya njiani, hivyo inabidi ifanyike dua ya maana kukikimbiza kitu hicho kilichomo katika mwili wa binti.

Mkono mtupu haulambwi, ustaz akaomba pesa ya vifaa kama udi, ubani nk ili afanye kisomo. Ndugu wakampa ustaz pesa, kweli ustaz alinunua vifaa ila alivyonunua havina uhalisia na pesa aliyopewa. Ustaz akapanga siku ya kisomo, ikapigwa dua pale, baada ya kumaliza ustaz akapewa na yeye chake cha kufutia jasho, mwisho wa siku hola mgonjwa hakupona.

Kuna sister wetu mmoja ni nesi, alipofika kutembea nyumbani akamkuta binti akiwa katika hali ile, kuuliza kilichomsibu binti huyo wakamwambia kwamba binti anasumbuliwa na jini. Ndo sister akashauri kwamba wampeleke hospital kwa ajili ya vipimo vingine, maana anaweza kuwa anasumbuliwa na tatizo la ini, figo nk. Mwanzo walipinga lkn mwisho wakakubali akapimwe.

Yule binti alivyopelekwa kupimwa akakutwa ana ukimwi, hivyo akapatiwa madawa ya kutumia. Leo hii yule binti karudi katika hali yake ya kawaida, hakuna cha jini wala pepo. Ukikutana nae kama hakukwambia kuwa anaumwa kamwe hauwezi kujua kama ana mwiba mwilini kwa jinsi alivyonenepa, kunawiri na kupendeza.

Ukweli ni kwamba watu wamepoteza wapendwa wao wengi tu kutokana na kuamini sana habari za uchawi, huku kiuhalisia ugonjwa wa mhusika hausiani na uchawi.
 
Kwenye Kutafta Tiba kuna kutapatapa kwingi ,Wakati mwingine watu huenda hosptali na maradhi yasionekani na wanaporudi upande wa pili napo ndo kunapatikana sababu ,ila huwenda mtu kweli ana maradhi ya hospitali ila yamechanganyika na kiswahili yakakosa kuonekana hosptali ,ila kama wangeenda hosptali tena kwa mara ya pili huwenda yangeonekana.
 
Kwenye Kutafta Tiba kuna kutapatapa kwingi ,Wakati mwingine watu huenda hosptali na maradhi yasionekani na wanaporudi upande wa pili napo ndo kunapatikana sababu ,ila huwenda mtu kweli ana maradhi ya hospitali ila yamechanganyika na kiswahili yakakosa kuonekana hosptali ,ila kama wangeenda hosptali tena kwa mara ya pili huwenda yangeonekana
Kweli kbs mkuu, kuna muda mtu anaweza kufanyiwa vipimo kiujanja ujanja ugonjwa wake usionekane. Ila atapoendelea kufanya vipimo zaidi mwisho wa siku maradhi yake huonekana na hatimae mgonjwa kupatiwa tiba ya kuendana na ugonjwa wake.

Kukimbilia kwa waganga wa kienyeji na sawa sawa na kwenda kuongeza matatizo zaidi ya ugonjwa na kutapeliwa juu.
 
Kuna wa2 mpk leo mtoto au ndg yao akiumwa maleria ya kichwa basi break yao ya kwanza ni kwenye maombi, duwa au mganga wa kienyeji kupiga ramli ya kumjua mlogaji.

Tz bado kuna safari ndefu ya kuwatenganisha wa2 na imani za kichawi.
 
Kuna wa2 mpk leo mtoto au ndg yao akiumwa maleria ya kichwa basi break yao ya kwanza ni kwenye maombi, duwa au mganga wa kienyeji kupiga ramli ya kumjua mlogaji.
Tz bado kuna safari ndefu ya kuwatenganisha wa2 na imani za kichawi.
Pamoja na vitabu vya dini kuwaonya watu kuhusu ushirikina, lkn bado watanzania wengi wamekuwa wagumu kuelewa.

So acha wapigwe hadi akili ziwakae sawa.
 
Na hivyo vitabu vya dini vinakiri kuwa uchawi upo na ukaeleza jinsi ya kujikinga nao kwasababu kuna namna ukijiweka uchawi haukupati
Kweli lkn hiyo ya kukimbilia kuhusisha ugonjwa wa mtu na uchawi, kabla ya kupata kwanza vipimo vya kina mahospitalini inapelekea watu wengi kulaghaiwa na hatimae kuliwa hela zao bila mgonjwa kupata nafuu au kupona kbs.
 
Kweli lkn hiyo ya kukimbilia kuhusisha ugonjwa wa mtu na uchawi, kabla ya kupata kwanza vipimo vya kina mahospitalini inapelekea watu wengi kulaghaiwa na hatimae kuliwa hela zao bila mgonjwa kupata nafuu au kupona kbs.
Hata huko hospital nako tunabet tu binafsi shangazi yangu aliwahi kupelekwa hospital ya kanisa inaitwa NAMBAYA wakampima hana ugonjwa wakampeleka hospital ya wilaya ya masasi (mkomaindo) kumpima hana homa yeyote ila mtu yupo hoi,pale tukaanza kugawanyika mwingine anadai twende kwa mganga kwasababu hospital hauonekani ugonjwa ila baada ya majadiliano ya muda mrefu tukaamua tumpeleke hospitalin ndanda ile tumemfikisha baada ya kupimwa kumbe ni kisukari tu
 
Back
Top Bottom