Haya ndiyo maandamano yanayoruhusiwaTanzania tu!

Straight corner

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
385
132
Wana JF nimejaribu Kufikiria ni maandamano ya aina gani yaliyowahi kupewa baraka na serikali yetu kwa miaka ya hivi karibuni nimekosa jibu, pengine tukumbushane tu!

Naona sasa maandamano yanayoruhusiwa na serikali ya Tz ni ya viongozi wakubwa tena wengine mafisadi wanapokuwa wanarejea vijijini kwao, wanapotua airport wakitokea nchi za nje kuuza ka-inchi ketu.
Jamani mbona hata Mchungaji mmoja waumini wake waliwahi kuandamana kumpokea kutokea airport hadi kanisani kwake bila shida wala sababu zozote za kiintelijenjia kujitokeza?
Nafikiri ile ibara inayoruhusu maandamano ya amani ifutwe kwa sababu imetawaliwa sana na habari za kiintelijensia
hapa nchini.
 
Maandamano ya kupinga malaria haikubaliki, miaka 50 ya uhuru, mashujaa wa uhuru na yanayofanana na hayo! Maandamano yoyote ya kupinga uamuzi wa serikali hayakubaliki na serikali kwa sababu za kiintelejensia au kiusalama kwani ni ngumu kuthibitisha.
 
Maandamano ya kumpokea JK kuwa mwenyekiti wa Africa.

Maandamano ya kumpokea JK akitokea Ulaya kubadilisha damu.

Maandamano ya kumpokea JK akitokea Chalinze kutoa Kafara.

Hayo yote ruksa!
 
Back
Top Bottom