Haya ndio mambo yanayombeba na kumpatia ushindi Rais Samia uchaguzi ujao

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,340
9,767
Ndugu zangu watanzania,

Naomba niende moja kwa moja kueleza kwa kina Mambo yatakayombeba na kumpa ushindi wa kishindo Rais Samia Uchaguzi Ujao.

Moja, Rais Samia anakubalika na watanzania wa Rika zote,Dini zote,makabila yote,Kanda zote Na jinsia zote, miaka michache iliyopita CCM na wagombea wake walikuwa wanapewa Taabu na shida Sana na baadhi ya makundi katika kupata uungwaji mkono,mfano kundi la vijana likiongozwa na wale wa vyuo vikuu waliokuwa wanapeleka ushawishi wao mpaka mitaani walikuwa Ni ngome ya kutumainiwa na vyama vya upinzani hasa CHADEMA kwa Bara na CUF kwa Zanzibar,CCM na wagombea wake walipata Taabu Sana katika kuwashawishi vijana kuwaunga mkono,hata vijana wenyewe walijiona aibu kuvaa sare za CCM mitaani na kutambulikana Kama Ni Wana CCM,walijiona fahari kuwa upinzani na kujiita makamanda,hii yote ilitokana na skendo za Rushwa na ufisadi kwa baadhi ya viongozi ndani ya CCM na serikalini zilizokuwa zinatawala na kugonga vichwa vya habari,Hali hii iliwapa hasira Sana vijana kuona Taifa lao likitafunwa na wachache huku wao wakihangaika mitaani bila mitaji Wala ajira na kuambiwa tu wajiajiri pasipo kusaidiwa hata namna ya kupewa mikopo,waliona ni Kama Wana baguliwa na kutopewa kipaombele na serikali ya CCM na viongozi, ndio maana wakaamua kuiadhibu CCM katika majimbo mengi Sana kwa kuchagua upinzani hasa katika majiji makubwa na miji mbalimbali.

Lakini Tangia Rais Samia aingie madarakani Hali imebadilika ghafla,kwa Sasa vijana kuanzia wale wa vyuo vikuu mpaka wa mitaani wanatafuta kadi za CCM na kumuunga mkono Rais Samia kwa Kiwango Cha juu Sana,wanavaa sare za CCM na kutamba nazo mitaani bila hofu Wala wasiwasi kutokana na kuguswa na uchapa kazi wa mh Rais wetu mama Samia pamoja na serikali yake ya CCM,kwa kuwa amewawezesha Sana vijana kimaisha kwa kuwapatia ajira za moja kwa moja serikalini Kama alivyotoa ajira zaidi ya elfu 42,lakini pia kuwawezesha mitaji kupitia mikopo ya halmashauri,kwa Sasa vijana wanasema wanakwenda na mama na mama Samia ndio chaguo lao uchaguzi ujao.

Lakini pia Rais Samia anakubalika Sana na watu wa Dini zote na jinsia zote ,kwa kuwa ameonyesha kushirikiana na watu wa Dini zote pasipo ubaguzi,anahudhuria shughuli na kufanya mazungumzo na viongozi wa Dini zote, hatabkatika jinsia Rais Samia anakubalika na jinsia zote ambapo wote wanaridhishwa na uchapa kazi wake na kumuona Kama kiongozi wa mfano na kuigwa.

Pili,Rais Samia anakubalika na watu wa vyama vyote,kwa Mara ya kwanza katika historia ya mfumo wa vyama vingi Tumeona viongozi wa upinzani wakipanda majukwaani na kumsifu na kumpongeza Rais Samia kwa uchapa kazi wake ,umadhubuti, ushupavu, uzalendo na ujasiri wake katika kuliongoza Taifa letu na kuwatumikia watanzania,Hii yote Ni kutokana na kuguswa na utendaji kazi wa Rais Samia na serikali yake ya CCM,Hali hii inampa nafasi Rais Samia kupita bila kupingwa uchaguzi ujao.

Tatu ,Rais Samia Amekidhi matarajio ya watanzania, Matarajio waliyokuwa nayo watanzania kwa Rais Samia ameyakidhi na kupitiliza , watanzania walihitaji Rais Samia awaongoze na kuwatumikia Kama Mtumishi wao,awasikilize wanataka Nini,Atatue kero na changamoto zao,atoe majibu na suluhisho kwa wakati juu ya kero mbalimbali,aimarishe demokrasia na umoja wa kitaifa n.k,mambo hayo yote na mengine mengi Rais Samia ameyatimiza na kuyatekeleza kwa Kiwango Cha juu Sana na kumpa nafasi ya kushinda kwa kishindo uchaguzi ujao.

Nne,Ujenzi wa uchumi jumuishi, Rais Samia Amefanikiwa Kujenga uchumi Unaogusa maisha ya watu,uchumi unaoonekana na kukua katika maisha na mifuko ya Watanzania,Rais Samia Amejenga miradi ya kimkakati inayotoa ajira kwa vijana wengi,Amejenga na kusogeza hudumu za kijamii karibu ya mwananchi ,ameweka Sera nzuri za kiuchumi zinazochochea na kuupa Afya mzunguko wa fedha hapa nchini.

Tano Ni Umri, Katika suala hili kwa hakika linabeba na kumpa fursa kubwa Sana Rais Samia ya kutuongoza watanzania muhula wanpili,kwa kuwa ndio umri ambapo kiongozi amekomaa kibusara,kihekima,kiutu,kimaamuzi,kimsimamo na pia amekomaa kiuongozi na kiuzoefu katika masuala ya kiutendaji, jiulize Rais wa marekani ana miaka mingapi na alikuwa na miaka mingapi anapochaguliwa? Jiulize hata hapa Tanzania vijana wangapi walipopewa madaraka wakabadilika na kuwa Kama walevi kwa kuanza kutukana watu,kutesa watu,kudharau Hadi wazee,kuvunja Sheria bila hofu Wala uoga, watanzania kwa Sasa wanamhitaji Sana Rais Samia ili aendelee kupitiliza Taifa letu na kuwalea vijana kuja kulitumikia Taifa letu siku za usoni, Rais Samia Anayo nafasi kwa kuwa umri wake unahitajika Sana hasa katika kufanya maamuzi kwa busara na hekima kwa maslahi ya Taifa letu.

Sita Ni uzoefu wa kiuongozi,hapa itoshe kusema kuwa hakuna wa kumfikia ,Rais Samia anao uzoefu mkubwa Sana wa kiuongozi ndani ya serikali na hata katika secta binafsi,tunahitaji kiongozi Aina ya Rais Samia ili ajuwe pia umuhimu wa secta binafsi katika uchumi wetu Kama Taifa,ndio maana kwa uzoefu wake tunaona kwa Sasa ambavyo uchumi wetu unakuwa kwa Kasi kutokana na kwamba anafahamu ni Nini afanye ili kukuza uchumi au vipi ashirikiane na secta binafsi au kuvutia wawekezaji au watalii au hatua za kisheria na kisera katika kuvutia fursa za kiuchumi na kibiashara nchini.

Saba ni uwezo wake kiuongozi,Rais Samia ameonyesha uwezo mkubwa Sana kiuongozi katika kuliongoza Taifa letu,ameonyesha umadhubuti na ushupavu katika kuchukua hatua mbalimbali katika maeneo mbalimbali,ndio sababu ya kuona Taifa letu likiendelea kutamalaki kwa amani na utulivu.

Nane ni utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM,Rais Samia ametekeleza vizuri Sana ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo ilisheheni mambo mengi mazuri yanayogusa maisha ya watanzania wanyonge,mfano uboreshaji wa secta ya Elimu,Afya , usambazaji wa huduma za maji Safi na salama,ujenzi na ukamilishaji wa miradi ya kimkakati,mfano katika Elimu kwa Sasa Elimu ni bure Mpaka kidato Cha sita japo awali ilikuwa Hadi kidato Cha nne,ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20 na hivyo kufanya wanafunzi wote kuripoti shuleni kwa wakati mmoja bila mwanafunzi kukaa nyumbani kwa kukosa madarasa kama ilivyokuwa awali, kuwapa mikopo wanafunzi wote wenye sifa wa Elimu ya juu.

Kujenga umoja wa kitaifa,Rais Samia kwa Sasa anapongezwa kila Kona na kupewa nafasi ya kupita bila kupingwa kutokana na kuliweka Taifa pamoja,kuwafanya watanzania kuzungumza lugha moja,kusalimiana na kushirikiana katika shughuli za kijamii,kutobaguana kwa misingi ya Dini au kabila au Kanda au vyama,amefanya haya kwa maneno na matendo ya kiungwana ,amefanya haya kwa ulimi wake. Hali hii imewagusa Sana watanzania na kuwa na kiu ya kutaka utumishi wake kwa muhula wa pili.

Kuleta maendeleo katika kila secta,Rais Samia ameleta mapinduzi katika kila secta utakayokwenda na kutazama lazima utaona mikono yake, juhudi zake,hatua zake , uwekezaji wake,mipango Yake mizuri ,sauto yake, Hakuna ambako Rais Samia haijafika au kugusa au kutazama kwa jicho la kiuongozi.

Kujenga matumaini katika maisha ya watanzania, Rais Samia Amefanikiwa Kujenga matumaini katika mioyo ya watanzania juu ya kesho yao iliyo Bora, kwa Sasa kila mtanzania anaona Anayo nafasi ya kufanikiwa na kutimiza Ndoto zake chini ya uongozi wa Rais Samia ,hakuna aliekata Tamaa ya kimaisha,kila mtu anaona Giza lililo mbele yake litapita tu na ni la muda tu,kila mtanzania anaona ana uwezo wa kuwa Tajiri na kuondokana na Hali ya umaskini wa kipato.

Usikivu wake kwa watanzania,Rais Samia Ni msikivu Sana na mnyenyekevu Sana kwa watanzania,amejiweka katika nafasi ya kuwa Kama Mtumishi wa watu ,muajiriwa wa watanzania na anayetakiwa kufanya na kuamua kulingana na mahitaji ya watanzania,Hali hiyo imewavutia Sana watanzania na kuwagusa mioyo Yao,maana wanamuona Rais Samia Kama Mtumishi wao muungwana na mwaminifu Sana katika kuwatumikia na kuwaongoza.maana siku zote watanzania hawapendi mtu au kiongozi anayewapuuza au kuwadharau au kujiona Mungu mtu au kuwadhalilisha bila sababu au kushindwa kuwasaidia wanapohitaji msaada wa serikali au kuwasikiliza wanataka Nini na kwa wakati gani,katika hili Rais Samia Amefanikiwa kuziteka nyoyo za watanzania kwa usikivu wake.

Kuwa karibu na wananchi, Rais Samia wakati wote wa uongozi wake amekuwa karibu Sana kiuongozi na watanzania,amefanya mengi kwa kuwasikiliza wanataka Nini na wanaomba Nini na kwa wakati gani,amewatembelea katika maeneo yao na kuzungumza nao hatua mbalimbali na mipango ya serikali yao pamoja na kuwasikiliza kero zao, ametatua kero kwa wakati na kutoa majibu kwa wakati,kwa hakika imekuwa Ni serikali ya watu Inayowatumikia watu na kuwasaidia watu badala ya kuwaumiza au kuwatesa au kuwadidimiza kiuchumi,Rais Samia amekuwa mfariji wa Taifa na mwenye kuwapa watu matumaini wakati wote kikauli na kivitendo.

Rais Samia anakubalika Sana na wanaccm na CCM yote kwa ujumla wake,Wana CCM wanampenda na kumkubali Sana Rais Samia ,Ndio Maana wakati wote wamekuwa wakimuunga mkono katika utekelezaji wake wa ilani ya CCM katika kuwahudumia watanzania,wanaccm wanasubiri muda ufike tu ili wampatie baraka zao za kupeperusha bendera na kumfanya mgombea pekee baada ya upinzani kuwa umekata pumzi na kupoteza muelekeo na Dira,Wana CCM wameridhishwa na uchapakazi na utendaji kazi wa Rais Samia na serikali yake ulioiletea heshima CCM mbele ya watanzania ambao Sasa wanaiamini na kuiunga mkono serikali Yake.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu

0742-676627
 
Basi hapo umeweka namba ya cm ili wakutafute wakutumie pesa ya bando la internet 😂😅 vijana wa mnapenda mteremko shauri yenu mtaendelea kufirimbwa
 
Huyu kaandika mambo yatakayompa ushindi Samia, kuna mwingine kaandika mambo yatakomfanya ashindwe kuongoza nchi 2025

😂😂

Yani ni mvurugano
 
Rais Samia Ndio chaguo la watanzania uchaguzi ujao,wanachosubiri kwa Sasa Ni muda ufike ili wakampigie kura za Ndio kwa kishindo
Jf sijawahi kuona mpumbavu kama wewe. Sisi tupo kwenye ripoti ya CAG mpumbavu wewe upo kwenye uchaguzi ambao hata wewe huna uhakika nao
 
Acha uongo.

SABABU KUBWA ni kuwalambisha asali wapinzani wake na kuwafanya mazuzu. Basiii.

Nchi inachangamoto sana hii kwa sasa kuliko wakati wowote.
 
Kwani andiko langu Ni wapi limekuzuia kuwa kwa CAG,pia lazima ufahamu ya kuwa ripoti ya CAG imetoka Kama ilivyo kutokana na uongozi wa Rais Samia kuzingatia suala Zima la utawala Bora na uwazi katika kuendesha serikali yake
 
Acha uongo.

SABABU KUBWA ni kuwalambisha asali wapinzani wake na kuwafanya mazuzu. Basiii.

Nchi inachangamoto sana hii kwa sasa kuliko wakati wowote.
Basi na wewe anzisha chama chako ili tukusikie hoja zako Kama unaona wapinzani wameshindwa kufanya vile unavyotaka wewe,pia lazima ufahamu ya kuwa uchapa kazi uliotukuka wa Rais Samia Ndio umepelekea kuungwa mkono na hata upinzani
 
Ndugu zangu watanzania,

Naomba niende moja kwa moja kueleza kwa kina Mambo yatakayombeba na kumpa ushindi wa kishindo Rais Samia Uchaguzi Ujao.

Moja, Rais Samia anakubalika na watanzania wa Rika zote,Dini zote,makabila yote,Kanda zote Na jinsia zote, miaka michache iliyopita CCM na wagombea wake walikuwa wanapewa Taabu na shida Sana na baadhi ya makundi katika kupata uungwaji mkono,mfano kundi la vijana likiongozwa na wale wa vyuo vikuu waliokuwa wanapeleka ushawishi wao mpaka mitaani walikuwa Ni ngome ya kutumainiwa na vyama vya upinzani hasa CHADEMA kwa Bara na CUF kwa Zanzibar,CCM na wagombea wake walipata Taabu Sana katika kuwashawishi vijana kuwaunga mkono,hata vijana wenyewe walijiona aibu kuvaa sare za CCM mitaani na kutambulikana Kama Ni Wana CCM,walijiona fahari kuwa upinzani na kujiita makamanda,hii yote ilitokana na skendo za Rushwa na ufisadi kwa baadhi ya viongozi ndani ya CCM na serikalini zilizokuwa zinatawala na kugonga vichwa vya habari,Hali hii iliwapa hasira Sana vijana kuona Taifa lao likitafunwa na wachache huku wao wakihangaika mitaani bila mitaji Wala ajira na kuambiwa tu wajiajiri pasipo kusaidiwa hata namna ya kupewa mikopo,waliona ni Kama Wana baguliwa na kutopewa kipaombele na serikali ya CCM na viongozi, ndio maana wakaamua kuiadhibu CCM katika majimbo mengi Sana kwa kuchagua upinzani hasa katika majiji makubwa na miji mbalimbali.

Lakini Tangia Rais Samia aingie madarakani Hali imebadilika ghafla,kwa Sasa vijana kuanzia wale wa vyuo vikuu mpaka wa mitaani wanatafuta kadi za CCM na kumuunga mkono Rais Samia kwa Kiwango Cha juu Sana,wanavaa sare za CCM na kutamba nazo mitaani bila hofu Wala wasiwasi kutokana na kuguswa na uchapa kazi wa mh Rais wetu mama Samia pamoja na serikali yake ya CCM,kwa kuwa amewawezesha Sana vijana kimaisha kwa kuwapatia ajira za moja kwa moja serikalini Kama alivyotoa ajira zaidi ya elfu 42,lakini pia kuwawezesha mitaji kupitia mikopo ya halmashauri,kwa Sasa vijana wanasema wanakwenda na mama na mama Samia ndio chaguo lao uchaguzi ujao.

Lakini pia Rais Samia anakubalika Sana na watu wa Dini zote na jinsia zote ,kwa kuwa ameonyesha kushirikiana na watu wa Dini zote pasipo ubaguzi,anahudhuria shughuli na kufanya mazungumzo na viongozi wa Dini zote, hatabkatika jinsia Rais Samia anakubalika na jinsia zote ambapo wote wanaridhishwa na uchapa kazi wake na kumuona Kama kiongozi wa mfano na kuigwa.

Pili,Rais Samia anakubalika na watu wa vyama vyote,kwa Mara ya kwanza katika historia ya mfumo wa vyama vingi Tumeona viongozi wa upinzani wakipanda majukwaani na kumsifu na kumpongeza Rais Samia kwa uchapa kazi wake ,umadhubuti, ushupavu, uzalendo na ujasiri wake katika kuliongoza Taifa letu na kuwatumikia watanzania,Hii yote Ni kutokana na kuguswa na utendaji kazi wa Rais Samia na serikali yake ya CCM,Hali hii inampa nafasi Rais Samia kupita bila kupingwa uchaguzi ujao.

Tatu ,Rais Samia Amekidhi matarajio ya watanzania, Matarajio waliyokuwa nayo watanzania kwa Rais Samia ameyakidhi na kupitiliza , watanzania walihitaji Rais Samia awaongoze na kuwatumikia Kama Mtumishi wao,awasikilize wanataka Nini,Atatue kero na changamoto zao,atoe majibu na suluhisho kwa wakati juu ya kero mbalimbali,aimarishe demokrasia na umoja wa kitaifa n.k,mambo hayo yote na mengine mengi Rais Samia ameyatimiza na kuyatekeleza kwa Kiwango Cha juu Sana na kumpa nafasi ya kushinda kwa kishindo uchaguzi ujao.

Nne,Ujenzi wa uchumi jumuishi, Rais Samia Amefanikiwa Kujenga uchumi Unaogusa maisha ya watu,uchumi unaoonekana na kukua katika maisha na mifuko ya Watanzania,Rais Samia Amejenga miradi ya kimkakati inayotoa ajira kwa vijana wengi,Amejenga na kusogeza hudumu za kijamii karibu ya mwananchi ,ameweka Sera nzuri za kiuchumi zinazochochea na kuupa Afya mzunguko wa fedha hapa nchini.

Tano Ni Umri, Katika suala hili kwa hakika linabeba na kumpa fursa kubwa Sana Rais Samia ya kutuongoza watanzania muhula wanpili,kwa kuwa ndio umri ambapo kiongozi amekomaa kibusara,kihekima,kiutu,kimaamuzi,kimsimamo na pia amekomaa kiuongozi na kiuzoefu katika masuala ya kiutendaji, jiulize Rais wa marekani ana miaka mingapi na alikuwa na miaka mingapi anapochaguliwa? Jiulize hata hapa Tanzania vijana wangapi walipopewa madaraka wakabadilika na kuwa Kama walevi kwa kuanza kutukana watu,kutesa watu,kudharau Hadi wazee,kuvunja Sheria bila hofu Wala uoga, watanzania kwa Sasa wanamhitaji Sana Rais Samia ili aendelee kupitiliza Taifa letu na kuwalea vijana kuja kulitumikia Taifa letu siku za usoni, Rais Samia Anayo nafasi kwa kuwa umri wake unahitajika Sana hasa katika kufanya maamuzi kwa busara na hekima kwa maslahi ya Taifa letu.

Sita Ni uzoefu wa kiuongozi,hapa itoshe kusema kuwa hakuna wa kumfikia ,Rais Samia anao uzoefu mkubwa Sana wa kiuongozi ndani ya serikali na hata katika secta binafsi,tunahitaji kiongozi Aina ya Rais Samia ili ajuwe pia umuhimu wa secta binafsi katika uchumi wetu Kama Taifa,ndio maana kwa uzoefu wake tunaona kwa Sasa ambavyo uchumi wetu unakuwa kwa Kasi kutokana na kwamba anafahamu ni Nini afanye ili kukuza uchumi au vipi ashirikiane na secta binafsi au kuvutia wawekezaji au watalii au hatua za kisheria na kisera katika kuvutia fursa za kiuchumi na kibiashara nchini.

Saba ni uwezo wake kiuongozi,Rais Samia ameonyesha uwezo mkubwa Sana kiuongozi katika kuliongoza Taifa letu,ameonyesha umadhubuti na ushupavu katika kuchukua hatua mbalimbali katika maeneo mbalimbali,ndio sababu ya kuona Taifa letu likiendelea kutamalaki kwa amani na utulivu.

Nane ni utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM,Rais Samia ametekeleza vizuri Sana ilani ya uchaguzi ya CCM ambayo ilisheheni mambo mengi mazuri yanayogusa maisha ya watanzania wanyonge,mfano uboreshaji wa secta ya Elimu,Afya , usambazaji wa huduma za maji Safi na salama,ujenzi na ukamilishaji wa miradi ya kimkakati,mfano katika Elimu kwa Sasa Elimu ni bure Mpaka kidato Cha sita japo awali ilikuwa Hadi kidato Cha nne,ujenzi wa vyumba vya madarasa zaidi ya elfu 20 na hivyo kufanya wanafunzi wote kuripoti shuleni kwa wakati mmoja bila mwanafunzi kukaa nyumbani kwa kukosa madarasa kama ilivyokuwa awali, kuwapa mikopo wanafunzi wote wenye sifa wa Elimu ya juu.

Kujenga umoja wa kitaifa,Rais Samia kwa Sasa anapongezwa kila Kona na kupewa nafasi ya kupita bila kupingwa kutokana na kuliweka Taifa pamoja,kuwafanya watanzania kuzungumza lugha moja,kusalimiana na kushirikiana katika shughuli za kijamii,kutobaguana kwa misingi ya Dini au kabila au Kanda au vyama,amefanya haya kwa maneno na matendo ya kiungwana ,amefanya haya kwa ulimi wake. Hali hii imewagusa Sana watanzania na kuwa na kiu ya kutaka utumishi wake kwa muhula wa pili.

Kuleta maendeleo katika kila secta,Rais Samia ameleta mapinduzi katika kila secta utakayokwenda na kutazama lazima utaona mikono yake, juhudi zake,hatua zake , uwekezaji wake,mipango Yake mizuri ,sauto yake, Hakuna ambako Rais Samia haijafika au kugusa au kutazama kwa jicho la kiuongozi.

Kujenga matumaini katika maisha ya watanzania, Rais Samia Amefanikiwa Kujenga matumaini katika mioyo ya watanzania juu ya kesho yao iliyo Bora, kwa Sasa kila mtanzania anaona Anayo nafasi ya kufanikiwa na kutimiza Ndoto zake chini ya uongozi wa Rais Samia ,hakuna aliekata Tamaa ya kimaisha,kila mtu anaona Giza lililo mbele yake litapita tu na ni la muda tu,kila mtanzania anaona ana uwezo wa kuwa Tajiri na kuondokana na Hali ya umaskini wa kipato.

Usikivu wake kwa watanzania,Rais Samia Ni msikivu Sana na mnyenyekevu Sana kwa watanzania,amejiweka katika nafasi ya kuwa Kama Mtumishi wa watu ,muajiriwa wa watanzania na anayetakiwa kufanya na kuamua kulingana na mahitaji ya watanzania,Hali hiyo imewavutia Sana watanzania na kuwagusa mioyo Yao,maana wanamuona Rais Samia Kama Mtumishi wao muungwana na mwaminifu Sana katika kuwatumikia na kuwaongoza.maana siku zote watanzania hawapendi mtu au kiongozi anayewapuuza au kuwadharau au kujiona Mungu mtu au kuwadhalilisha bila sababu au kushindwa kuwasaidia wanapohitaji msaada wa serikali au kuwasikiliza wanataka Nini na kwa wakati gani,katika hili Rais Samia Amefanikiwa kuziteka nyoyo za watanzania kwa usikivu wake.

Kuwa karibu na wananchi, Rais Samia wakati wote wa uongozi wake amekuwa karibu Sana kiuongozi na watanzania,amefanya mengi kwa kuwasikiliza wanataka Nini na wanaomba Nini na kwa wakati gani,amewatembelea katika maeneo yao na kuzungumza nao hatua mbalimbali na mipango ya serikali yao pamoja na kuwasikiliza kero zao, ametatua kero kwa wakati na kutoa majibu kwa wakati,kwa hakika imekuwa Ni serikali ya watu Inayowatumikia watu na kuwasaidia watu badala ya kuwaumiza au kuwatesa au kuwadidimiza kiuchumi,Rais Samia amekuwa mfariji wa Taifa na mwenye kuwapa watu matumaini wakati wote kikauli na kivitendo.

Rais Samia anakubalika Sana na wanaccm na CCM yote kwa ujumla wake,Wana CCM wanampenda na kumkubali Sana Rais Samia ,Ndio Maana wakati wote wamekuwa wakimuunga mkono katika utekelezaji wake wa ilani ya CCM katika kuwahudumia watanzania,wanaccm wanasubiri muda ufike tu ili wampatie baraka zao za kupeperusha bendera na kumfanya mgombea pekee baada ya upinzani kuwa umekata pumzi na kupoteza muelekeo na Dira,Wana CCM wameridhishwa na uchapakazi na utendaji kazi wa Rais Samia na serikali yake ulioiletea heshima CCM mbele ya watanzania ambao Sasa wanaiamini na kuiunga mkono serikali Yake.

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu

0742-676627
Chawa big
 
Hivi wewe maisha yako ni mazuri sana si ndio?
 
Kwani Hali yangu ya maisha inabadilisha Nini juu ya ukweli wa kukubalika na kupendwa kwa Rais Samia na watanzania, hata nikiwa na maisha ya chini lakini ukweli Ni kuwa Rais Samia Ndio chaguo la watanzania ,kwa kuwa wameona juhudi za mh Rais katika kugusa maisha Yao na kuleta matumaini katika mioyo Yao
 
Kumbe umeamua kuishi maisha ya chini na kuwa Chawa? Unakela ila hujui tu. Na sijui kama unajua maisha yako yanavyotakiwa kuwa.
 
Mimi nimekuiliza maisha yangu yawe mazuri au ya chini yanabasilisha vipi ukweli na uhalisia wa namna Rais Samia anavyopendwa na kukubalika na watanzania
 
SIJASOMA UJINGA HUO.

KIJANA BADALA AWAZE KAZI ANATAKA MTEREMKO WA TEUZI

TUSHAKUBALINA KUACHA NAMBA COMRADE KWAAJILI YA TEUZI UMEFANYA VZURI
 
kofia ya Askari haiuziki bro. Ni kama unalazimisha mk...u utafune Muwa.... jamaa utaumia vibaya
 
Back
Top Bottom