Haya maonyesho/sherehe zamiaka hamsini mnazi mmoja zinanikera sana

mikonomiwili

JF-Expert Member
Jan 11, 2011
273
50
Nianze kwa kutoa salamu kwa wana Jamii wote

nimekaa nikawaza sana kuhusu hayamaonyeshao yakila wizara hivi yanatusaidia nini ? na je inawaongezea nini wananchi wakati huu wakusherekea miaka hamsini ?

Mimi nilitegemea huumwaka wa kusherekea Tunge fanya kitu chamaana ambacho hata wajukuu wetu wangekuja kuona kua kulikua na sherehe za miaka hamsini.kama vile sisi tunavyo ona kua kipindi kile cha uhuru watuwalijenga minara na kulikua na mwenge na vitu vingi ambavyo hata sasa ukiviona unajuakweli wale wazee walisherekea na walifurahia . lakini chaajabu leo tunakua na moonyesho ya wizara yanafanyika mkoani Dar es salamu pale mnazimmoja ,Hiyo hela inayo tumika kukaa mnazimmoja tungechanganya nazakuchanga kama tunavyo fanya kwenye kampeni tungejenga hosipitali mpya kila wilaya ama shule ama tungenunua ndegekubwa ama treni yakwenda kasi ama barabara moja ya juu ama chochote kingine ilimradi tu baada yamiaka kathaa tukikiona tuseme ulemwaka tulisherekea miakahamsini na tukawa na hiki,
Lakini mpaka sasa sijui kama kunakitu kimefanyika kushuudia kua kweli Tanzania imefikisha miaka hamsini .

Mfano mdogo tu ni kwenye familia zetu huaga tukiwa na birthday tuna toa zawadi ambako inakua na kumbukumbu kwayule mwenye birthday ,hata baada ya miaka miwili atakumbuka.sasa kwa hii miaka hamsini ya uhuru serikali imetuongoza tufanye nini ili kiwe kama kumbukumbu hata baada ya miaka hamsini mingine ?

badala yake wameweka maonyesho Mnazimmoja Dar es salamu je yule mwananch wa kule Masasi aatafikaje mnazimmoja kwaajili ya kujionea hayomaonyesho ya wizara ?so serikali inamwongozaje kwenye kusherekea hiimiaka hamsini ?

Lingine ni hili la slogani ya hii miaka hamsini ya uhuru naisikia watu wanaiongeatu lakini sijawahi kusikia mtu anaitolea ufafanuzi kua ina maana gani ''Tumethubutu tumeweza na tunazidi kusongambele'' huaga nashindwa kuelewa Tumethubutu nini ? yaani ni sawa na nyumba ni yako halafu unamwa nunua godoro kisha uwaambie majirani eti nimethubutu kununua godoro wakati nyumba niyako na kitanada nichako. Ama hii tumethubutu nikua tumethubutu kuibafetha za uma ,Mwenye maana halisi ya hili neno tumethubutu anifafanulie .

Ukija kwenye hii ya tumeweza nayo pia inanichanganya nikipi amabacho tulikua tunashindwa kabla ya uhuru sasa tumeweza ,kabla ya uhuru kulikua hakuna shule zakutosha na kulikua hakuna madawati yakutosha na mpaka sasa havitoshi je tumeweza nini ,ama nihili lakuweza ku iba na kuweka watu wanao chukua rasilimalizetu na hakuna anehoji? umeme ule ule wa uhuru ndo tunao mapakaleo na ile reli alio jenge mkoloni ndo tunayo mpaka leo tumeweza nini ?

ok Tunasongambele hukombele ni wapi , shilingi sasa inazidi kuporomoka kila kukicha ndombele huko? Vifo vya mama wajawazito vinaongezeka ,mashirika viwanda tulivyo kua navyo vime kufa , swali ni kipi tunachosonganancho mbele ?

Mimi sioni faida ya hayo moonyesho pale mmnazimmoja zoidi naona niupotevu wahela za walipa kodi huku wakiwa wanafaidi wachache
 
halafu ukienda wizarani kupata huduma unaambiwa watendaji wapo mnazimmoja.na siku ukiwakuta wanakuambia umeme hakuna.kama umetoka mkoani ndo utasota hitelini hadi uhamie jwa ndugu ambai nao watakuchoka shida yako haiishi
nji hii ya wagagagigikoko!!
 
Sio bure Mzee wa Upako alisema juu ya maonyesho,(MTU MZIMA KUVAA NEPI NA KUTEMBEA NAY BARABARANI) juu ya mafanikio ya miaka 50 ya uhuru. Eti wamethubutu, wameweza na wanasonga mbele. Kwa uhalisi wa mambo tukliangalia kero mbalimbali za wananchi, maji, afya, barabara, elimu wameshindwa na wamerudisha maendeleo nyuma. Ni bora wakubali kushindwa na kusahihishwa na wajipange upya. Pesa zinazotumika kusherehekea mafanikio hewa zingeelekezwa kwa kero hizo.
 
Wakimaliza kila wizara ieleze umma wa watanzania kuwa wametumia kiasi gani kama utasikia dowans nyingine.Haya maonyesho ya Mnazi mmoja ni matunda ya semina elekezi Dodoma.Mkulo shillingi inakwenda chini kwenye maonyesho ya wizara yake kaalika makirikiri na Ngwasuma.Hivi haya matumizi ni ya muhimu kweli?Hizi wizara zote zilishiriki saba saba,nane nane na wiki ya mashirika ya Umma sasa kulikuwa na umuhimu gani wa kufanya haya maonyesho?Hivi yale haliyosema PM kuwa watadhibiti matumizi yasiyo ya muhimu hanatekeleza kwa vitendo?
 
Subiri ifike Jan 2012 ujaribu kufanya utafiti ujue kufanikisha sherehe za miaka hamsini ya Uhuru wa Tanganyika ni fedha kiasi gani imetumiwa utashangaa, na hapo ndio utajua viongozi wako wanaubunifu na umahiri uliotukuka wa kutafuna kodi zenu.
 
Back
Top Bottom