BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 422
- 1,049
Ndugu zangu katika pitapita zangu nimefanikiwa kufika mitaa ya Mbezi Luis karibu na ilipo Stendi ya Mabasi ya Magufuli, nadhani ile ni Kata ya Mbezi, kuna mambo kadhaa yanaendelea yanayohusu utapeli kama ilivyo kawaida kunapokuwa na purukushani za watu Jijini Dar.
Karibu na Daraja la kuelekea Stendi ya Magufuli, kuna wizi unaendelea lakini wahusika wanajificha kwa kivuli cha Bahati Nasibu.
Wanaoibiwa asilimia kubwa ni kina mama, hao wezi wameweka maspika makubwa na kuna makorokoro mengi, wanachofanya unachagua namba ili upate vitu, waliozunguka ni wengi na ukishiriki michezo hiyo wanakuibia.
Nashauri viongozi wa maeneo hayo waangalie, wasiruhusu wizi huu uendelee, wanaoteseka kwa asilimia kubwa ni Wanawake wanaotoka nje ya Mji, kwa kuwa matapeli waliopo hapo wanawatumia Wanawake wenzao kuigiza kama vile nao wanashiriki kume ni michezo ya tu.
Ndio maana wenyeji wengi hawashiriki michezo hiyo kwa kuwa wanajua kinachoendelea ni utapeli, wanaopigwa wengi wao ni Wageni.
Hata kama wanapewa vibali na Serikali za Mtaa au Wilaya hao watu waangaliwe matendo na mtukio yao, wasitumie kivuli cha bahati nasibu kuzingua.