hawa ndo wasanii wa bongo,aibu tupu..

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Q-Chief, TID wakamatana uchawi

Amani
pix.gif
Ishu nzima ilitokea hivi juzi kati jijini Dar es Salaam, baada ya Mtangazaji wa Kipindi cha Bongo Beats kinachovunja mawinguni kupitia Kituo cha Runinga cha Star TV, Sauda Mwilima kuomba kupiga stori na Q-Chief.

Wakiwa kwenye mahojiano ya laivu, Q-Chilah alisikika akisema kuwa tangu ameacha kufanya kazi na TID mambo yake yamekuwa hayaendi vizuri na kwamba tatizo hilo limekuwa ni la kudumu kwa upande wake.

Q-Chief aliendelea kusema siku moja akiwa katika mishemishe zake alikutana na mama mmoja (hakumtaja jina) aliyemwambia kuwa amelogwa na wasanii wenzake wawili akiwemo TID.

Akiongea na Amani kwa njia ya simu, Q-Chief aliendelea kupigia msumari kuwa, ni kweli amelogwa na wasanii hao na hakuna ubishi.

Kwa upande wa TID aliliambia Amani kuwa, kauli ya Chilah imemdhalilisha sana hivyo ameamua kwenda kuripoti polisi na kwamba atahakikisha anamshughulikia kadiri ya uwezo wake.
 
Bifu la TID, Q-Chief latinga polisi

risasi jumamosi
pix.gif
Taarifa zilizotufikia zimedai kuwa, bifu la wawili hao limefika polisi baada ya juzi kati Q-Chiller kuanza kumsaka mwenzake huku akiwa na silaha.

Akiongea na Risasi hivi karibuni, Meneja wa TID Khamisi Dakota alisema kuwa, Desemba 8 mwaka huu, akiwa maeneo ya Magomeni, Q- Chief alimvamia akiwa na wenzake wanne na kuanza ‘kumjazia inzi' huku akimuuliza aliko TID.

Hata hivyo, kutokana na mazingira ya kutokuelewana kati ya wawili hao, inadaiwa Q-Chiller alianza kumsemea mbovu Dakota na mwishowe kuchomoa kisu na kutaka kumchoma.

Kufuatia hali hiyo, Dakota alikwenda moja kwa moja kuonana na TID ambapo walishauriana kulifikisha suala hilo polisi ambapo walikwenda kituo cha Magomeni na kufungua jalada la kesi lenye namba Mag/RB/22117/09 kutishia kuua kwa kisu.
 
Usupastaa wa Bongo ni kazi saaana!
Hivi bi Bange nini zinawasumbua?
Ukosefu wa elimu?...mtu unaanza kumtuhumu mwenzio tu kuwa amekuroga, kumbe mwenyewe unaejiroga kwa kujiona wewe ndo wewe, na ushamaliza kila kitu chini ya jua!
Je mahakama itapataje evidence ya suala kama hili la uchawi?
Hapo obviously kesi itakuwa ni ya kutishia raia kwa silaha, na si ugagura!
 
Huku ni kujitia ujuaji usio kuwa na maana, huyu Q- chillar alishashindwa muziki muda mrefu tu mara utasikia anaimba taarabu mara anaimba mchiriku! sasa atasemaje amelogwa?
 
Huku ni kujitia ujuaji usio kuwa na maana, huyu Q- chillar alishashindwa muziki muda mrefu tu mara utasikia anaimba taarabu mara anaimba mchiriku! sasa atasemaje amelogwa?

mhhh.
 
Msiwaze sana wakubwa, mlishawahi kujiuliza kwamba hata huyo meneja wa msanii ana upeo gani? Na anajua kwamba kum expose vibaya mteja wake ni hatari kwa kampuni (kama wanayo).

Wewe meneja wa kampuni nawe unakubaliana kwamba unaamini uchawi, angekuwa meneja makini asingeruhusu hizi habari ziendelee kwenye vyombo vya habari kwani ni hatari kwa mwenendo mzima wa kampuni. Kwa kuwa inafahamika kwamba sio siri kwamba miongoni mwa wateja wenu hawaamini huu upuuzi.

Shame to maneger also!
 
wanatuaibisha na kutudhalilisha,ingekuwa nchi za wenzetu wangegoma kwenda kwenye miziki yao na kununua cd zao but sisi ni bendera ufuata upepo always
 
Q-Chief, TID wakamatana uchawi

Amani
pix.gif
Ishu nzima ilitokea hivi juzi kati jijini Dar es Salaam, baada ya Mtangazaji wa Kipindi cha Bongo Beats kinachovunja mawinguni kupitia Kituo cha Runinga cha Star TV, Sauda Mwilima kuomba kupiga stori na Q-Chief.

Wakiwa kwenye mahojiano ya laivu, Q-Chilah alisikika akisema kuwa tangu ameacha kufanya kazi na TID mambo yake yamekuwa hayaendi vizuri na kwamba tatizo hilo limekuwa ni la kudumu kwa upande wake.

Q-Chief aliendelea kusema siku moja akiwa katika mishemishe zake alikutana na mama mmoja (hakumtaja jina) aliyemwambia kuwa amelogwa na wasanii wenzake wawili akiwemo TID.

Akiongea na Amani kwa njia ya simu, Q-Chief aliendelea kupigia msumari kuwa, ni kweli amelogwa na wasanii hao na hakuna ubishi.

Kwa upande wa TID aliliambia Amani kuwa, kauli ya Chilah imemdhalilisha sana hivyo ameamua kwenda kuripoti polisi na kwamba atahakikisha anamshughulikia kadiri ya uwezo wake.

wanashindwa kuhoji thamani ya album inayotungwa kwa wiki moja,WANAHALALISHA ALBAMU HIZO HIZO ZIVUME MIAKA MIA MOJA!

WAMESAHAU:kwamba wapenzi wa muziki wa kizazi kipya ni wale wale,wanachokifanya ni kuangalia nani anaweza kwa kipindi hicho,WANASINGIZIA UCHAWI!
FOOLS!:mad:
 
Hivi mtu ukilogwa ile transmission ya uchawi inapita kwa electromagnetic waves au inakuwa particles?

Au ina some sort of wave particle duality?

Maanake kama kweli haya mambo yapo mtu anaweza kuchukua Nobel ya Physics au Chemistry hivi hivi watu wakashangaa.

Mimi siamini uchawi, na kama kuna mchawi anasoma au mtu anayesoma anamjua, naomba aniloge tuone.
 
Mimi siamini uchawi, na kama kuna mchawi anasoma au mtu anayesoma anamjua, naomba aniloge tuone.

Yep...mimi nimeshawa dare waniloge lakini wapi. Halafu mimi hapa natumia jina langu la kweli na wakitaka jina la mwisho nitawapa hapa. Nyinyi wachawi kama mpo hapa nawaombeni mniloge.
 
Hivi mtu ukilogwa ile transmission ya uchawi inapita kwa electromagnetic waves au inakuwa particles?

Au ina some sort of wave particle duality?

Maanake kama kweli haya mambo yapo mtu anaweza kuchukua Nobel ya Physics au Chemistry hivi hivi watu wakashangaa.

Mimi siamini uchawi, na kama kuna mchawi anasoma au mtu anayesoma anamjua, naomba aniloge tuone.

Bluray uchawi upo wachawi wapo..ni mambo ya kishirikina...hazielezewi kwa physics wala hesabu!
ila imani yako naipenda kama huamini hawawezi kukuloga hawana huo uwezo, ila uombe sana imani isiterereke!!!
 
shule ndo tatizo kuu la wasanii wa bongo...

kwani unafikiri ni shule kwa wanamuziki, wanamuziki wengi duniani ni wachache sana walioenda shule, tatizo la Tanzania sekta ya sanaa imekuwa kama ni kitu cha kujitolea tu na wala sio ajira wala biashara, we unakuta mtu kama Dakota, Fella ndio wawe mameneja wa wanamuziki mtu hana hata taaluma moja ya mambo ya management, wala marketingna kwa sababu ya ubovu huo unakuta hata quality ya muziki, movies, maigizo, soka, riadha, ngumi nk zote ziko poor tu, haya ya uchawi hajaanza leo sijuhi kama mnakumbuka hizi1) Mabesi na Matumla2) Charles Libondo na Anton Ndaki (ndaki alifia ulingoni)3) Tindwa5) nicco zengekala5) Dede na wenzie7)Yanga kuruka ukuta taifa, mambo ya njiwa
 
Mimi ni msanii kama jina langu lilivyo.
Wanabodi fahamuni kwamba wengi muwaitao wasanii wa bongo si wasanii ni bosheni na chariot chassers tu.
Wengi hawataki shule (mfano Mr. Blue) na sana sana wanaiga hawana creative link ktk vichwa vyao.
Msihuzunike ni kuwahurumia na KUWAPUUZA
 
hivi mtu ukilogwa ile transmission ya uchawi inapita kwa electromagnetic waves au inakuwa particles?

Au ina some sort of wave particle duality?

Maanake kama kweli haya mambo yapo mtu anaweza kuchukua nobel ya physics au chemistry hivi hivi watu wakashangaa.

Mimi siamini uchawi, na kama kuna mchawi anasoma au mtu anayesoma anamjua, naomba aniloge tuone.

be carefull on what you wish for.......
 
Usupastaa wa Bongo ni kazi saaana!
Hivi bi Bange nini zinawasumbua?
Ukosefu wa elimu?...mtu unaanza kumtuhumu mwenzio tu kuwa amekuroga, kumbe mwenyewe unaejiroga kwa kujiona wewe ndo wewe, na ushamaliza kila kitu chini ya jua!
Je mahakama itapataje evidence ya suala kama hili la uchawi?
Hapo obviously kesi itakuwa ni ya kutishia raia kwa silaha, na si ugagura!
ni kweli ndumu si nzuri
 
huyu Q-Chies sifjui Q Chillah, (kutojua jina gani analolitumia sasa ni weak point kwake!) alikuaga mwanamziki mzuri sana mwanzoni...sasa mara akaanza kubadilisha jina...mara anaimba kiingereza kibovu...2 by 2 makes four, jamani mi nilifeli hesabu, ila sio kihivyo...sasa mtu kama mimi siwezi kusikiliza upupu, basi akawa anapoteza shabiki mmojammoja, mimi nikiwa mmoja wapo, sasa hapo anamlaumu TID kwa kosa gani? au TID alimloga awe anaandika mashairi aysiyokua na miguu wala mikono na broken english zake?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom