Kinachozungumzwa hapa ni jinsi ya kujipanga kuenea kwa vuguvugu la mageuzi nchi nzima na si swal la bora mwakilishi. Kuna sehemu ambazo chama hakijaijeng saaana lakini mgombea wake labda amepata kura nying za kumfanya awe wa pili, basi jimbo au mkoa huo watafute mwanachama wa huko anyeweza kukijenga chama. Wa huko sina maana ya kabila bali ukazi.Mi nafikiri la muhimu kwanza ni kumpata mwenye moyo wa kukijenga chama kutegemea na uwezo wake wa kujenga hoja na kutoa muda wake kukisaidia chama. Huu ni wakati wa mapambano. Hata Jeshini huwezi kumweka kamanda legelege kwa sababu ati anatoka mkoa fulani. Ujasiri, umakini, na moyo wa kukitumikia chama wakati wa shida na wakkati wa raha ni muhimu zaidi.
Kama wapo wanaotoka mikoa ambayo haikupata wabunge ambao ni majasiri na wanajua kujenga hoja ni vizuri zaidi wakachukuliwa hao. Kama hawapo si vizuri ukamuokota mtu ukamwambia nenda bungeni wakati haoni kuna tatizo.
Bahati mbaya CHADEMA hawakusikilizwa walipopinga utaratibu wa kupeleka majina tume hata kabla ya uchaguzi. hili ndilo linalotakiwa libadilishwe ili vyama viweze kuweka mikakati ya uchaguzi ujao. Ni wazo zuri ila lisitazamwe kama kwamba utaratibu huu utumike irresponsibly na wala wale ambko CHADEMA ndio stronghold wasijisikie kunyang'anywa mkate. Tuweke ujenzi wa chama nchi nzima mbele.