Hawa ndiyo makocha wa kumrithi Jose Mourinho pale Old Trafford

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,447
WATU bana! Jose Mourinho ameshaonekana kuwa mzigo tu huko Manchester United kutokana na kujaa vizingizio tu kila timu yake inapofanya ovyo kwenye Ligi Kuu England.
Kikosi hicho cha Old Trafford kimekuwa kikicheza kwa sare tu baada ya usiku wa juzi Jumamosi kutoka sare ya tatu mfululizo kilipomenyana na Southampton.

Jambo hilo limeifanya timu hiyo kushushwa kutoka kwenye nafasi ya pili hadi ya tatu huku wakiwa wameachwa kwa pointi 14 dhidi ya vinara Manchester City kabla ya mechi yao ya jana Jumapili ugenini kwa Crystal Palace.

Mashabiki wa Manchester United wanaonekana kumchoka Mourinho kutokana na staili yake ya kupaki basi huku akiwataka wachezaji kama Paul Pogba na Henrikh Mkhitaryan kukaba, wakati mastaa hao ubora wao upo kwenye kushambulia tu.

Jamie Carragher hivi karibuni alisema Man United hii ya sasa, kwa wachezaji hawa hawa waliopo, kikosi hicho akipewa Pep Guardiola kinachochukua ubingwa.
Stori kwa sasa zimeanza kupigwa juu ya Mourinho kufunguliwa lango la kutokea huko Old Trafford na kuna makocha kadhaa wameshawekwa kwenye orodha ya wanaofaa kuja kuchukua mikoba ya Mreno huyo pale Man United.

5. LEONARDO JARDIM(AS MONACO)
Pengine si kocha maarufu sana na anayeandikwa kila siku kwenye vyombo vya habari kama ilivyo kwa Jose Mourinho na Pep Guardiola, lakini Jardim ni kocha anayejielewa na kazi yake si ya kitoto huko AS Monaco. Jardim ameiongoza Monaco kubeba taji lao la kwanza la Ligue 1 baada ya kusubiri kwa miaka 17 na alifanya hivyo mbele ya timu yenye pesa nyingi kama PSG. Jordim amewafanya mastaa kibao kwenye kikosi cha Monaco kuonekana kuwa matata kabisa na kufanya timu vigogo kuvamia kwenye timu hiyo kusajili wachezaji kadhaa. Hakika, huyu Leonardo Jardim ndiye kocha hasa ambaye Man United inahitaji kuwa naye. Monaco anafundisha soka la kuvutia sana na timu yake inapocheza ina mvuto, hivyo litakuwa jambo kubwa na la msingi sana kama atatua Old Trafford kuchukua mikoba ya Mourinho.

4. MAURICIO POCHETTINO (Tottenham)
Mauricio Pochettino ni kocha mwenye kipaji kikubwa sana huko Ulaya kwa sasa. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana ni kwamba Pochettino yupo kwenye rada za timu ya PSG.
Pochettino amekuwa akihusishwa na Manchester United tangu Louis van Gaal alipokuwa kwenye kikosi hicho cha Old Trafford. Mashabiki wa Man United ni kitu ambacho watakiunga mkono kwa nguvu zote kama Pochettino atakubali kuja kuchukua mikoba ya kuinoa timu yao.
Staili ya Muargentina huyo ni kutoa nafasi kwa wachezaji makinda, pia ni mfuasi wa soka la kushambulia, hivyo mashabiki wa Man United watakuwa kwenye furaha kubwa kama atatua kwenye timu yao kubadili mfumo na staili ya uchezaji hii ya sasa ambapo timu imewekeza zaidi kwenye kujilinda kuliko kusaka nafasi za kufunga mabao ya ushindi.

3. DIEGO SIMEONE (Atletico Madrid)
Mmoja wa makocha wanaoweza kulinda ubora wao huko Ulaya kwa sasa. Simeone aliongoza Atletico Madrid kutoka kusikojulikana na kubeba ubingwa wa La Liga mbele ya vigogo Real Madrid na Barcelona msimu wa 2013/14. Tangu wakati huo hadi sasa ameifikisha fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya timu hiyo mara mbili tofauti.
Shida inayomkwamisha asifanye vizuri zaidi huko Atletico ni kukosekana kwa pesa, hivyo kama atatua Man United mahali ambako pesa zinatoka tu, basi anaweza kufanya mambo makubwa yenye maajabu kwenye Ligi Kuu England.
Simeone ni kocha hatari kwa kutengeneza timu yenye ukuta mzuri na ujio wake wa huko Old Trafford kama utatokea basi ni jambo litakalokuwa na maana kubwa kwa timu hiyo.

2. MASSIMILIANO ALLEGRI (Juventus)
Mataji matatu ya Serie A na fainali mbili za Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka mitatu ya karibuni, Allegri ni mmoja wa makocha mahiri kabisa Ulaya kwa sasa na fundi kweli kweli wa kimbinu kwenye mechi

Allegri utaalamu wake ni kuweza kupata huduma bora kabisa kutoka kwa wachezaji wake
Kiungo Andrea Pirlo aliwahi kusema kuwa chini ya Allegri anakufanya mchezaji uanze kutumia sehemu ya kipaji chako ambayo hukuwa ukifahamu namna ya kuitumia. Hatarajiwi kuondoka Juventus siku za karibuni, lakini kama kutawekwa mezani ofa ya maana kutoka Man United, basi kocha huyo anaweza kukubali na kwenda kuchukua mikoba ya Jose Mourinho huko Old Trafford.

1. CARLO ANCELLOTI (hana kazi)
Mtaliano huyo ameshinda mataji kila mahali alipokwenda. Kocha huyo ana taji moja la Serie A, moja la Ligi Kuu England, moja la Bundesliga, moja la Ligue 1 na matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Lakini kwa sasa hana kazi. Ni kocha anayependelea staili ya soka la kushambulia, huku akiwa na mbinu matata kabisa.

Wakati Jose Mourinho, Juande Ramos, Manuel Pellegrini na Fabio Capello waliposhindwa kufanya kweli kwenye misimu yao ya kwanza Bernabeu, Ancelotti mwenzao alitamba mwanzo tu huko Real Madrid. Rekodi za kocha huyo amezinoa timu za maana duniani kuanzia Juventus, AC Milan, Chelsea, Paris Saint-Germain, Real Madrid na Bayern Munich. Hivyo ni kocha anayeweza kuleta mabadiliko Old Trafford.
 
story za mwanaspot bana hapo hamna hata kocha mmoja mwenye cv ya kuifundisha manchester united ZAIDI YA MOURINHO mwenyewe ni bora apewe giggs tu kabeba mataj yote ngazi ya club na anaujua utamaduni wa manchester united.
 
Moyes alipopewa alikuwa na cv ipi
 
mbona morinho hana shida jaman......shida ni mpira mbovu tu uwanjan..
..

wakina martial na lingard et siku hz ndo tegemez kikosini...looooollll
 
Simeone na Mourihno ni sawa tu. Kujihami kwingi. Falsafa ya Man U ni attack to defend. Mourihno ilikuwa suala la muda achemshe. Aende kwa Waarabu kule Paris
 
Man united ni ya pili mpaka sasa, sioni sababu ya mou kuondoka!! Kama unapenda pass nenda kashabikie aseno.
 
Mourinho till now his the best coach in the world__so for that mantic he will continued to be a Manchester united manager!!.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom