Hawa mawaziri ni wa serikali ipi?

baina

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
219
59
Kuna mambo yananitatiza kidogo, ni kwamba kuna mawaziri ambao wizara zao zimo ndani ya muungano kama ulinzi, mambo ya ndani, mambo ya nje n.k na kuna wizara ambazo mambo yake si ya ki muungano kama elimu, michezo n.k. kwakuwa zile wizara za muungano zinaitwa wizara katika serikali ya JMT.

Je hizi ambazo zinashughulikia masuala ya bara tu zenyewe zimo ndani ya serikali ipi? Hii ni kwa sababu kule Zenji kuna wizara ambazo zinahusika tu huko na si bara nazo ni wizara katika SMZ.

Na je baraza la mawaziri linaundwa na mawaziri wa serikali ngapi?

Katiba inasemaje kwenye hili?
 
Huo ndiyo mchanganyiko uliopo! yani kama simlitiniasi ekweshen vile lakini hata hiyo inajibu hii ya jmt na smz aaaaaaaagh! hakuna jibu hapo gundi ya mate!
 
Yani ni aibu watu kuikana asili yao! sijui wanaona aibu gani kusema miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika! shee!
 
unaweza (in red) kuwa unawakilisha Watanzania wengine zaidi ya milioni 40+ ambao kila ukiwauliza kitu hata yale mambo ya msingi kama hili tunadai hatujui.
Uliona hata JK hajui ni nani mmiliki wa DOWANS na si ajabu hata hili pia naye halijui.
Ndio maana tumeamua kutumia mabiliioni ya shillingi kusherehekea uhuru wa nchi tusiyoijua (tusiyotaka kuitaja!!!) ambayo inaonyesha kuwa tunaweza (Watanzania) kuwa miongoni mwa maajabu mapya ya dunia!
mhh mi apana jua.
ngoja wajuzi wakuje..
Yani ni aibu watu kuikana asili yao! sijui wanaona aibu gani kusema miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika! shee!
 
huu mchanganyo hata mimi siujui manake jiulize Shamsha Vuai ni mbunge wapi, mstaafu kupi na ni waziri huku kivipi?
 
Waasisi wetu waliamua hivyo na kuwaliuliza Watanganyika na Wazanzibari wakati huo, mnakubali muungano, Bunge likapitisha Baraza la mapinduzi likapitisha. Huo ndio muungano tulionao. Haujapata kutokea duniani na unaendelea kudumu kwa staili hiyo hiyo !!
 
Wanawakilisha serikali ya Tanganyika ambayo ipo lakini viongozi wetu hawataki
kuitambua ingawa wanaifanyia kazi kiujanjaujanja. Uhakika kwamba serikali ya
Tanganyika kuwepo unadhihirishwa na taaluma kadhaa wakiwemo madaktari
na wanasheria, kwani kuna Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na
Baraza la Madaktari wa Tanganyika (TMB)...
 
huu mchanganyo hata mimi siujui manake jiulize Shamsha Vuai ni mbunge wapi, mstaafu kupi na ni waziri huku kivipi?

Huyu ndio mshangao wangu mkuu...........ati alikataa kukaa nyumba(bara) isiyo na hadhi ya waziri kiongozi mstaafu(wa zanzibar) ilhali yeye ni waziri wa mambo ya ndani(muungano).........halafu ni mjumbe wa BLW Zanzibar na ni Mbunge wa kuteuliwa wa JMT............sasa sijui anahudhuriaje vikao vya mabunge mawili tafauti
 
Waasisi wetu waliamua hivyo na kuwaliuliza Watanganyika na Wazanzibari wakati huo, mnakubali muungano, Bunge likapitisha Baraza la mapinduzi likapitisha. Huo ndio muungano tulionao. Haujapata kutokea duniani na unaendelea kudumu kwa staili hiyo hiyo !!

Ukweli ni kwamba hakuna watu kutoka Zanzibar wala kutoka Tanganyika walioulizwa kama wanaukubali muungano. Muungano ulifanywa kwa siri kubwa sana na walioshuhudia walikuwa Mwalimu Nyerere, Sheikh Abeid Karume, Rashid Kawawa, Thabit Kombo na Oscar Kambona, wakati huo akiwa Waziri wa Mmabo ya Nje. Abdulrahman Babu alikuwa machachari sana (radical) akatumwa kupeleka ujumbe maalum China ili akiwa nje ya nchi majadiliano yafanyike na mikataba isainiwe. Muungano kausikia kwenye redio BBC na VOA alipowasili huko alikotumwa. Bado tu kuna wanaobisha tukisema kuna haja ya kuutazama upya muungano? Ni kweli haujapata kutokea duniani muungano kama huu. Kuna haja ya watanzania wote kuliulizia suala zima hili na lazima liwemo katika mjadala wa katiba mpya. Vinginevyo tutaendelea kujikanganya.
 
Clemence nafikiri bado huna uwezo wa kupambanua mambo, kwani mambo ya muungano yana wizara zake na kwahiyo hizo wizara ni za serikali ya JMT swali ni je hizi nyingine ambazo si za muungano maana yake ni za bara tu mawaziri wake ni wa serikali ipi?
 
Kwa mambo yalivyo kwa sasa, Serikali ya Muungano inashughulikia pia masuala yasiyo ya Muungano (yaani Tanganyika au Tanzania Bara), kwa kuwa hakuna serikali ya Tanganyika/ Tanzania Bara, mawaziri hawa ni wa Serikali ya Muungano wanaoshughulikia mambo yasiyo ya Muungano (Tanganyika au Tanzania Bara).
 
Back
Top Bottom