Hawa funza wametoka wapi?

Radhia Sweety

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
4,434
1,765
Nilipata safari ya dharura nikiwa nimeacha nyama kwenye friji. Huku nyuma umeme ukaisha. Cha ajabu nimekuta nyama inatoa funza wakati friji ilikuwa imefungwa kabisa. Hawa wadudu wametokea wapi? Wamejiumba?
 
Nyama inapoandaliwa lazima inzi atue juu yake. Ukifika home huwa unaosha lakini si uchafu wote unatoka. Inzi anapotua tu, huanza kuzaa, mayai yake huwekwa mahali penye mficho wala sio juu hadharani, eg ndani ya utumbo au penye mkato ulioingia ndani bila kukatika kabisa.
Ulipoosha na kuweka kwenye freezer, wale mayai wakaanza kuishi, tena umeme ulipokatika, ikawa mazingira mazuri ya kuanza maisha. Asikudanganye mtu ati bacteria hugeuka funza. Hapo mkatalie. Funza ni stage flan ya inzi, baada ya yai
 
Labda wamejiingiza tu wakajikutiamo kwa nyama ndani ya friji
 
Nyama inapoandaliwa lazima inzi atue juu yake. Ukifika home huwa unaosha lakini si uchafu wote unatoka. Inzi anapotua tu, huanza kuzaa, mayai yake huwekwa mahali penye mficho wala sio juu hadharani, eg ndani ya utumbo au penye mkato ulioingia ndani bila kukatika kabisa.
Ulipoosha na kuweka kwenye freezer, wale mayai wakaanza kuishi, tena umeme ulipokatika, ikawa mazingira mazuri ya kuanza maisha. Asikudanganye mtu ati bacteria hugeuka funza. Hapo mkatalie. Funza ni stage flan ya inzi, baada ya yai

Na wale funza wa chooni ambao siku zote hubaki kuwa funza. Sipingi ulichokielezea hapo juu, maana nimeshawahi pata msaada polini, nikaona inzi wa kijani akitua kwenye mzigo anaacha funza na wanatembea kabisa, illa nataka elimu zaidi mkuu.
 
Mangatara emeeleza vizuri sana! Ila Savimbi Jr kachemka vibaya, eti bacteria anageuka kuwa funza? Tangu lini bacteria akaonekana kwa macho uchi?
 
Kwa hiyo roho imekuuma vibaya mno si ndio? Acha uchoyo wewe hiyo nyama ungegawa na fridge ungezima.
 
Mangatara emeeleza vizuri sana! Ila Savimbi Jr kachemka vibaya, eti bacteria anageuka kuwa funza? Tangu lini bacteria akaonekana kwa macho uchi?

Acha ubishi ndugu,Chukua chakula kichemshe weka na maji kichemke hadi kufikia nyuzi mia Kuua hayo mayai ya nzi Kisha kifunike kisiguswe tena na nzi halafu uje na jibu kitatoa funza au lah,tusibishane kishabiki fanyeni utafiti kwanza Kisha mrudi na majibu.
 
Hii mada tushaijadili kitambo humu na wala hatujafikia muafaka, uloandika hapa na mimi niliuliza.
 
Nilipata safari ya dharura nikiwa nimeacha nyama kwenye friji. Huku nyuma umeme ukaisha. Cha ajabu nimekuta nyama inatoa funza wakati friji ilikuwa imefungwa kabisa. Hawa wadudu wametokea wapi? Wamejiumba?

Innocent Chacha, hii mada imeshajadiliwa humu na mimi binafsi kwa kadri ya ufahamu wangu nikaitolea majibu jaribu kuitafuta soma kwa makini majibu yangu na ya wanajamii wengine usipoelewa amma ukiwa na maswali ya ziada rudi tena tufahamishane zaidi.
 
Hii mada tushaijadili kitambo humu na wala hatujafikia muafaka, uloandika hapa na mimi niliuliza.

Chakula cha aina yoyote kilichooza kama kitakingwa(protected)vizuri kutokana na inzi kamwe hakitozalisha funza(maggots) ambao ni hatua ya pili ya ukuaji wa inzi (larva stage),na jaribio la kuthibitisha hili alilifanya Italian biologist Francesco Redi mnamo mwaka 1668.
 
Mangatara emeeleza vizuri sana! Ila Savimbi Jr kachemka vibaya, eti bacteria anageuka kuwa funza? Tangu lini bacteria akaonekana kwa macho uchi?

Bacteria hawezi ku evolve kuwa funza funza ni funza na bacteria ni bacteria tu,funza(maggots) anaowazungumzia mtoa mada ni hatua ya pili kati ya zile nne wanazopitia inzi kabla ya kuwa kiumbe kamili ambazo ni, 1.Egg 2.larva(maggots)ambao ndio funza,3.pupa na 4.imago ambaye ni nzi kamili.Bacteria ni mojawapo tu ya factor nyingi zinazotakiwa ili chakula kiweze kuoza.
 
Na wale funza wa chooni ambao siku zote hubaki kuwa funza. Sipingi ulichokielezea hapo juu, maana nimeshawahi pata msaada polini, nikaona inzi wa kijani akitua kwenye mzigo anaacha funza na wanatembea kabisa, illa nataka elimu zaidi mkuu.

Jaim;
Unaposema funza maana yake ni larva stage ya mdudu flan. Hakuna funza wa kudumu kuwa funza. Hawapo na hawatakuwepo
 
Nilipata safari ya dharura nikiwa nimeacha nyama kwenye friji. Huku nyuma umeme ukaisha. Cha ajabu nimekuta nyama inatoa funza wakati friji ilikuwa imefungwa kabisa. Hawa wadudu wametokea wapi? Wamejiumba?

Innocent Chacha,bakteria ndio walioozesha chakula ntakuelezea kwanini; kwanza kabisa ili chakula kioze kinaitjaji bacteria kitaalamu wanaitwa(putreflying bacteria) watakaokuwa wanazalisha aina fulani za enzymes(vimeng'enya)ambavyo ndio hasa watameng'enya chakula na kukifanya kioze,na kitaalamu hawa enzymes wanafanya kazi at optimum tempereture ambayo ni 28-40 degree centigrade ndani ya freezer tempereture ni ndogo sana about 0 degree centgrade hivyo enzymes zinakuwa innactive na haziwezi kumen'genya chakula na kukiozesha,umeme ulipoisha ndani ya freezer tempereture ikapanda na kuwa optimum inayoruhusu enzymes za hao bacteria kuwa active na hivyo kuozesha chakula ulichoweka.
 
Mangatara emeeleza vizuri sana! Ila Savimbi Jr kachemka vibaya, eti bacteria anageuka kuwa funza? Tangu lini bacteria akaonekana kwa macho uchi?

Bacteria hawezi ku evolve kuwa funza funza ni funza na bacteria ni bacteria tu,funza(maggots) anaowazungumzia mtoa mada ni hatua ya pili kati ya zile nne wanazopitia inzi kabla ya kuwa kiumbe kamili ambazo ni, 1.Egg 2.larva(maggots)ambao ndio funza,3.pupa na 4.imago ambaye ni nzi kamili.Bacteria ni mojawapo tu ya factor nyingi zinazotakiwa ili chakula kiweze kuoza.
Mkuu hii sayansi naikumbuka kwa mbali.... labda tu kuwa pamoja... ina maana wale funza wa chooni kama vyoo vya shuleni baadae (saint Kanumba) wanageuka kuwa nzi wakifika stage ya 4?
 
Back
Top Bottom