Haujakaa Uswazi!!!

* Kama hujawahi kumuona Albino (Zeruzeru) ukajitemea mate mwilini ! (eti usipofanya hivyo nawe utakua kama yeye!)
* Kama hujawahi ng'oa jino ukamtupia Kunguru ukisema "Kunguru chukua jino lako bovu unipe zima"
* Kama hujaogopa kutembelea karibu ya nyumba zilizokua zimejengwa mbali ya zingine (nyumba iliyojitenga na imezungukwa aidha na miti au vinginevyo iliitwa ya mumiani , mnyonya damu)
* Kama hukucheza kachiri saga!
* Kama hukua captain wa timu ya mtaani, wenzio wakachanga pesa mnunue gozi (mpira) na wewe ndiyo muhazini ukala pesa ya timu! Na ulaji wenyewe wa pesa sanasana hua ni mishkaki, ice cream, maembe, maandazi, kashata n.k.
 
Hiyo ya arnold ya jini terminator imenibidi ni cheke kwanza.Massawe bill blanks ndo umenikumbusha huko
 
Kama haujawahi kucheza kombolela
Kama haukuangalia "The Hard Way" , mniga aliliwa na mamba
Kama hauwezi kuimba "**** kina kaaloki.....Na Jimmy, acha acha hilo gitaa..ahaaahaaa aya madiscoooo dansa
Kama haujacheza kombolela usiku
Kama ya Arnold ya jini (terminator)haujaiona kwenye kibanda cha sinema
Kama haujawahi kudandia gari halafu likaongeza kasi ukashindwa kuruka halafu unashushwa 5Km away
Kama haujawahi kukimbia na kumtosa mshikaji baada ya kudondoka juu ya mti na kuumia
Kama haujapiga chabo
Kama haujagombea ndege zinazopita angani
Kama haukupigwa kwa kuwatia vidole watoto wenzako na kuchungulia wamevaa chupi ya rangi gani
Kama haujawahi kuchonganisha majogoo hadi yakapigana
Kama siku ya kuogesha mbwa haujasababisha wakadandiana
Kama haujawahi kucheza mchezo wa kujipikilisha na baba na mama
Kama haujachungulia dirisha la jirani kuangalia video
Kama haujawahi kwenda shule na fagio la chelewa na kidumu cha maji
Kama haujawahi kugombania kusukuma baisikeli za viwete ili uingie uwanjani bure

Endeleza na wewe......

Wikiendi Njema
Kama ujawai kuwa na njiwa chokichoki na sonara
Kama ujawai paisha kishada
Kama ujawai cheza kula mbakishie baba
Kama ujaangua maembe
Kama ujanywa togwa,kula visheti na ubuyo shuleni
Kama ujawai kula aiskrim kijiti chelewa
Kama ujatengeneza magari kwa madebe na matairi ya ndalankuwinda ndege na manati
 
kama hujawah kuchezesha joyce wowowo na kupata cent
kama hujawah kucheza ki-bruslee huu haa
kama hujawah chezesha sinema 6a mabuksi nyuma kibatari,
kama hujawah kucheza nilonge, nisilonge,
kama hujawah kuiba kopo la kujitawazia ukatengenezea magari, dah longi sana
 
aisee The Finest,
Hiyo ya Mniga kuliwa na mamba the Hard way nimeipenda. Umenikumbusha mbali kweli yani.
 
Kufuga samaki wa urembo!!!gapi,teksido!red!zebra!tambara!gold!mkasi!black more n.k!!!!njiwa kama sanaa,fungo,choki,kombokombo,kwankwaruu,kwankwaruu kisoda,choki matepe!!!!!!.......
 
....ni noumer....
..kama hujawahi goma kwenda church kwa kutonunuliwa nguo za skukuu....
...kama hujajifunza vuta sigara kwa kusokota karatasi....

kaka unalijua gosho!??basi ile mtoto anaweza akafa akijaribu iga dingi yake anapiga marlboro!!piga sana yale ma-kitu aisee!
 
da kwa ujumla mwanzisha thread katukumbusha mbaliii....enzi za trela loketo, bongo man, madilu system, yondo sister..kama hujaenda kutembea sikukuu na kikundi cha watoto wenzio halafu wewe ndo kiongozi wao...mnanunua miguu ya kuku,
 
Back
Top Bottom