Hatuwezi kuendelea kuilaumu Kenya na Mabeberu kwa matatizo binafsi ya Tanzania: 'We are paying the price of our own Wrongdoings!'

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,603
Wasalauumu wakuu!!

Uzi huu nilianza kuuandaa wakati Mama Samia anaenda Kenya, lakini sikuweza kuumaliza kwa wakati, nimeamua niuweke kwa sasa, japo muktadha wa sasa haupo kuijadili Kenya, ila itabidi niuweke kwasababu kuna mambo ambayo yapo relevant sana.

Imekuwa ni kawaida sana hapa jamvini kuona nyuzi ama comment za ‘wakuu’ kuishambulia sana nchi ya Kenya na wamekuwa wakitumia neno ‘Manyang’au’ kwa kunasabisha chuki zao dhidi ya Kenya ambazo pia zimekuwa zikichagizwa na hatua stahiki za viongozi wetu waandamizi dhidi ya Kenya. Mwelekeo wa maoni ya wadau na fikra za viongozi wengi wa ngazi za juu za Tanzania ni kwamba ‘Kenya imekuwa ikiihujumu Tanzania’ hivo ni jirani ambaye lazima atiliwe shaka.

Binafsi ntakuwa mmoja wa watu wachache wasiokuwa na ubaya wowote na Kenya, na ntakuwa wa mwisho duniani kuamini kwamba ni Kenya ndio imekuwa ikiihujumu Tanzania mpaka nchi yetu ipo hapa leo ilipo na Kenya ipo pale walipo. Nimefurahi pia sana kwa Mama Samia kuchukua hatua ya kuhuisha mahusiano yetu na Kenya. Kiongozi yeyote mwenye akili lazima angefanya kama Mama Samia. Ni kwasababu gani kwanza uwachukie Kenya?

Kama kichwa kinavosema, uzi huu ni mahsusi kuwapasha wale wote wenye mtizamo hasi juu ya Kenya. Na ujumbe ni kwamba ‘Kenya haiwezi kamwe kulaumiwa kwa matatizo yetu sisi watanzania, Tanzania inafaa kujilaumu yenyewe’

Ukifuatilia kwa makini, utofauti wa kiuchumi unaoonekana leo, kati ya nchi ya Tanzania na Kenya, umeanza kuonekana haswa miaka takribani 15 iliyopita – maana yake ni kwamba mwaka 2005 kurudi nyuma uchumi wa Kenya na Tanzania ulikuwa kwenye levels ambazo ni sawa kwa kuangalia urari wa pato la taifa kwa nchi hizi mbili.

gdp.JPG


gdp 1.JPG


So mpaka hapa, hoja ya msingi ni: Je? Wakenya wamefanya nini cha tofauti ambacho Watanzania hatukutilia maanani kuanzia mwaka 2005 mpaka sasa, kiasi cha uchumi wao kutuzidi kwa karibu USD 32 Billion (TZS 74 Trillioni) wakati mwaka 2005 tulikuwa nao sawa?

Kwa mtizamo wangu wa jicho la kiuchumi, niliweza kung’amua masuala yafuatayo. (Na tathmini yangu inaanzia mwaka 2005 kuja mbele) ambayo waKenya wameyafanya na ambayo waTanzania tuliyazembea.

1. Kuongozwa na viongozi wenye uelewa wa namna uchumi unavofanya kazi (Kuongozwa na vichwa wa kiuchumi)

‘Never underrate knowledge and what it can do to development’

Nimekuwa na mahaba makubwa na Marais wa Kenya kuanzia kwa Mwai Kibaki na hata kwa Uhuru Kenyatta, nakumbuka mwaka 2002 wakati Mwai Kibaki anamuangusha Daniel Arap Moi na chama chake cha KANU, nilikuwa darasa la sita kwa wakati huo, ila nakumbuka nilikuwa nikifuatilia utangazwaji wa matokeo ya urais kwenye redio na sikuweza kubanduka, nilimfurahia sana Mwai Kibaki bila sababu yoyote.

Ila ni wakati huu wa ukubwani, ndo nakuja kutambua haswa Mwai Kibaki alikuwa mtu wa namna gani, naweza sema ndo ambaye ameweka foundation yah ii rapid economic growth ya wakenya ndani ya hii miongo miwili. Na ndio umuhimu wa kuwa na viongozi wanaoelewa vema namna ya kukuza uchumi.

Mwai Kibaki -----> CV“ …. Kibaki instead attended Makerere University in Kampala, Uganda, where he studied Economics, History and Political Science, and graduated best in his class in 1955 with a First Class Honours Degree (BA) in Economics.[4] After his graduation, Kibaki took up an appointment as Assistant Sales Manager Shell Company of East Africa, Uganda Division. During the same year, he earned a scholarship entitling him to postgraduate studies in any British University. He consequently enrolled at the prestigious London School of Economics for a BSc in public finance, graduating with a distinction. He went back to Makerere in 1958 where he taught as an Assistant Lecturer in the economics department until 1961…..”

Baada ya Mwai Kibaki 2013, akamufuata Uhuru Kenyatta – exposed person, economist, bepari, mzalendo wa ukweli, opportunist. Huyu mwamba amefanya makubwa sana kwa Kenya.

Uhuru Kenyatta ---> CV “….After attending St. Mary's school, Uhuru went on to study economics, political science and government at Amherst College in the United States.[8][9][2] Upon his graduation, Uhuru returned to Kenya, and started a company Wilham Kenya Limited, through which he sourced and exported agricultural produce…..”

Kwa Tanzania, kutoka kwa Mkapa mpaka kwa Kikwete, tulikuwa at least heading in the right path, kwa sababu ni viongozi ambao walikuwa wanajua ni namna gani ya kukuza uchumi, na sera zao za uchumi wa soko ndio haswa zilisababisha booming ya private sector in Tanzania.

Laiti kama aliyempokea kijiti Kikwete angekuwa ni mtu dizaini ya Uhuru Kenyatta, Tanzania ingekuwa ya tofauti sana, hicho ndo nnachoamini. Ndo mana daima ntaamini kwamba, ujio wa Rais Magufuli ambaye hakuelewa vema the role of private sector to economic growth, itabaki kuwa janga la kihistoria kwa nchi ya Tanzania, as a result of Magufuli regime, kuna dynamics nyingi sana za kiuchumi zimebadilika ambazo zilisababisha huu uchumi uchechemee kwa at least 5 years, while in the same time, uchumi wa Kenya ulikuwa unapaa, chini ya MasterMind Uhuru Kenyatta.


2. Cost of doing business (mazingira ya ufanyaji wa biashara na uwekezaji)

Ni biashara na uwekezaji ndo unakuza uchumi wa taifa, nchi ya kenya imekuwa iki improve sana kwenye mazingira ya ufanyaji wa biashara na uwekezaji kwa miaka ya hivi karibuni kulinganisha na nchi ya Tanzania. Hii imepelekea mazingira rahisi ya kibiashara na uwekezaji kwa wakenya wenyewe na wawekezaji wa nje.

ease 1.JPG

ease 2.JPG


Ukiangalia hizi takwimu za ease of doing business kwa nchi ya Tanzania na Kenya, unaweza kuona kabisa kwamba kwa miaka mitano iliyopita, nchi ya Kenya imeweza ku improve in cost of doing business kwa points 15.21 wakati kwa Tanzania improvement ya mazingira ya kufanya biashara na uwekezaji yaliongezeka kwa points 4.77. (Ni kama kwenye era nzima ya Magufuli, ambayo unahesabu kuanzia mwaka 2017 kwa sababu hizi takwimu zinatolewa mwaka mmoja kabla, ni kwamba hakukuwa na improvement yoyote katika mazingira ya ufanyaji biashara na uwekezaji)

Kwenye hizi takwimu za mazingira ya ufanyaji biashara, huwa wanaangalia viashiria vifuatavyo

  • Paying Taxes – mazingira ya ulipaji kodi
  • Getting credits – kupata mikopo, riba za mikopo etc
  • Starting a business – leseni ya biashara, vibali etc
  • Construction permit – vibali vya ujenzi
  • Getting electricity
  • Registering properties
  • Protecting minority investors
  • Trading across borders
  • Enforcing contracts.
  • Resolving insolvency
Bila kuingia kwa ndani kabisa, kwenye hivo vigezo hapo juu, ila tuelewe tu kwamba Kenya walifanya improvements kubwa sana kwenye kuboresha mazingira kama ya upatikanaji wa mikopo (mfano bunge la Kenye lilileta sheria ya ku cap interest rate at 13% ambayo kwa kiasi fulani ilisaidia sana wakenya ku access mikopo) bila kusahau uraisi wa kufungua kampuni Kenya ambapo nadhani sheria yao, inaruhusu mtu kuanzisha kampuni bila kuwa na capital. Wameweza pia kuwa na uboreshaji mkubwa wa sheria za kodi.

Kwa Tanzania sote tunajua mambo yaliyotokea miaka ya hivi karibuni, na unaweza kuona ni namna gani mazingira yetu ya kufanya biashara yamakuwa ni mabovu mno na hii imekuwa na matokeo yake kwenye shuhuli za kiuchumi.


3. Elimu yenye tija kwa watu wake na lugha ya kiingereza.

Mfumo wa elimu wa Kenya umeimarika sana, sijui ni kwasababu ya mchango wa lugha ya ‘Kiingereza’ ila Wakenya wengi waliosoma tena shule na vyuo vyao vya ndani, wamekuwa ni watu wakujiamini sana, hii imepelekea miaka ya hivi karibuni wakenya wengi waende kufanya kazi nje ya nchi yao, as a result wengi wamepata exposure kulinganisha na watanzania ambao wengi ni waoga kutoka nje ya nchi yao kwa sababu ya kutokujiamini partly inawezekana ni kwasababu wengi wa watanzania Kiingereza imekuwa ni tatizo, kwahiyo wanaogopa kuvuka boda.

Mwisho wa siku impact inaonekana kwenye uchumi, ukiangalia kwenye takwimu za remittances flow, utakubaliana na huu ukweli ambao mimi nauhusianisha na ‘elimu na lugha ya kiingereza’ – whether ukubali au ukatae, ndo ukweli huo.

rem 1.JPG


So basically, Tanzania is paying the heavy price kwa vitu ambavyo tunakuwa tunavipuuzia na ambavyo wakenya wanavipa kipaumbele. Tumekuwa nyuma sana Tanzania na wanasiasa wetu bado hawajatambua namna ya kubadilisha.


4. Katiba, sheria, na miongozo

Kipindi cha Mwai Kibaki, Kenya walibahatika kupata katiba bora sana ambayo imeweza kutoa mazingira bora ya kufanya shughuli za kiuchumi kwa wakenya. Imefanya wakenya ku embrace ubepari ambao ndo mfumo unaofanya kazi katika kukuza uchumi, while Tanzania bado tunagandana na ujamaa usiofanya kazi.

As a result, katiba ya wakenya ambayo ime grant freedom of thinking imekuwa chachu ya kufungua akili za wakenya, no matter hata ukiona trend ya remittances flow, inakuambia kitu fulani.

Huku kwingine Tanzania, na vyombo vya kutuga sheria wamekuwa wapo busy kuzidi kukandamiza watanzania kwa kutunga sheria ambazo zinaminya uhuru wa fikra ambayo ni chachu ya kukuza uchumi na kufanya innovation.

Ni kama vile wanasiasa na watunga sheria wa Tanzania wamekuwa wapo busy kuonesha wao ni miamba na miungu watu, utaangalia type ya viongozi kama Magufuli, Ole Sabaya, Paul Makonda, Job Ndugai and the likes.. yaani ni kama walikuwa na uadui na watanzania wakati wangetakiwa kuwa busy kufikiri ni namna gani wataboresha mazingira wao walikuwa busy kuwakomesha watu – Take it or leave.. ndo ukweli ambao wengi tunaochambua haya mambo tutabaki kuushika.


Hitimisho
So all in all, sioni ni kwanini tuwe tunaendelea kulaumu Wakenya au Mabeberu kwa matatizo ambayo watanzania wenyewe tunayalea na tumeyatengeneza wenyewe.
  • Wakenya au mabeberu hawakutuambia tuwe na mazingira magumu ya kufanya biashara na kuwekeza – tulichagua wenyewe kuwa sheria kandamizi za uwekezaji.
  • Sio wakenya au mabeberu waliotuambia tuendelee kuwa na elimu ambayo haiwapi watu kujiamini kuvuka border na ku explore the world – tulichagua wenyewe
  • Sio wakenya au mabeberu walituambia tuendelee kuwa na mfumo wa kijamaa usiofanya kazi – tulichagua wenyewe
  • Sio wakenya au mabeberu walituambia tuwe na viongozi wanaokanyaga sheria – tulichagua wenyewe
  • Sio wakenya au mabeberu walituambia tununue ndege cash wakati kuna vipaumbele vingine ambavyo tungeweza kuwekeza na kutoa return nzuri kwa jamii – ni sisi wenyewe tulilipa pesa cash hawakutushika mkono
  • Sio wakenya au mabeberu walituambia tununue ndege halafu tuandike ‘Hapa kazi tu’ badala ya kuandika ‘Karibu Tanzania nchi ya Mlima Kilimanjaro’ – ni sisi wenyewe
So, watanzania wenzangu, tuache hii tabia ya kupenda kuwatwisha mizigo Kenya na nchi nyingine hata Mabeberu, kwa matatizo ambayo ni sisi wenyewe tunayasababisha, tunayakumbatia, na tulichagua kuwa nayo.

Maisha yamenifundisha kwamba, ‘you will always pay the price of your mistakes’ iwe kwenye mahusiano, iwe kwenye kitu chochote, utalipia makosa yako. So watanzania wenzangu wenye akili, adui wentu hawezi kuwa Kenya, adui wetu hawezi kuwa Mabeberu, adui wetu ni hawa ambao mpaka sasa hatuna katiba ya kueleweka, demokrasia ya kueleweka, sheria kandamizi, na wapo wanadunda kila siku tunawaona. Ni hawa hawa ndio wanakesha wakituaminisha kwamba Wakenya ni wabaya, mabeberu ni wabaya, wakati wao ndo wabaya.

Wako katiba ujenzi wa Taifa
N.Mushi
 
Duh! Mimi Mkenya, inanibidi nisome kwa kurudia rudia hili bango limesheheni madini balaa..... sijawahi kukutana na upembuzi wa kihivi...muhimu sana great thinkers humu wakasoma na kujadili kwa kutumia weledi na akili.
 
Ongezea na hili :

Hadi Magufuli anaingia, balance of trade ilikuwa inaelekea kuwa chanya. Kikwete aliacha imports za 14.6 tr (na zilikuwa na trend ya kupungua from 18.5 tr mwaka 2013) na exports za 12.4 tr (na zilikuwa zikiongezeka kutoka 8.9 tr mwaka 2013). Kwa hiyo balance ilitoka -9.6 tr mwaka 2013 hadi -2.2 tr mwaka 2015

Ila tukajiharibia wenyewe mazingira ya biashara na kufukuza wawekezaji wa kigeni na wengine wazawa. Wakaondoka na mitaji yao na ujuzi wao wakapeleka kwingine ikiwemo Kenya. Matokeo yake import hazikubadilika sana, zilishuka kidogo kuja kuwa 12.6 tr kutoka 14.6 tr alizoziacha kikwete na uuzaji wa bidhaa nje ulipungua sana kutoka 12.4 tr alizoacha hadi kufika 6.2 tr mwaka 2020 !!!! Balance ya biashara ilitoka -2.2 tr mwaka 2015 kuja -6.4 tr !!!

Kwa maana nyingine ni kuwa sera ya viwanda ilikuwa ni maneno matupu huku kiongozi wa juu hajui hata namna ya kuhuisha viwanda. Hivi tunawezaje kusema uchumi wetu ulikuwa ukikua wakati viashiria vyote vilikuwa vikionesha kwamba tunarudi nyuma??

Source: TheChanzo
Uagizaji na uuzaji bidhaa kutoka nje

 
Naona Mzee Mkapa ndiye alifanya vyema zaidi kama sikosei. Hongera kwa kuweka vielelezo na kuvitumia kwenye kujenga hoja yako.

Umeanzia 2005 kama ulivyosema, ambapo ndipo Wakenya walipoanza kutuacha mbali. Nimezitizama hizo “graphs”, na kuona kwamba tulikuwa sambamba kuanzia 1999-2005. Kuna la kujifunza kutoka kwenye miaka hiyo?
Ni kweli hatuna dira ya Taifa, na ndiyo maana akiingia rais wa tofauti, hakuna muendelezo bali vurugu mechi tu.
 
Mkuu uzi ni mzur na nakupongeza kwa hilo
Mimi naomba kuongezea kuhusu woga wa watanzania kwenye kufanya biashara na kenya
Watanzania ni waoga sana wa biashara nadhani ujamaa umetuathiri sanaaaa na ndo moja ya chanzo cha haya yote
 
Naona Mzee Mkapa ndiye alifanya vyema zaidi kama sikosei. Hongera kwa kuweka vielelezo na kuvitumia kwenye kujenga hoja yako.

Umeanzia 2005 kama ulivyosema, ambapo ndipo Wakenya walipoanza kutuacha mbali. Nimezitizama hizo “graphs”, na kuona kwamba tulikuwa sambamba kuanzia 1999-2005. Kuna la kujifunza kutoka kwenye miaka hiyo?
Ni kweli hatuna dira ya Taifa, na ndiyo maana akiingia rais wa tofauti, hakuna muendelezo bali vurugu mechi tu.
Nadhani miaka ya 1999 mpaka 2005 ambayo ni kipindi cha Mkapa, ni kipindi ambacho Mkapa ali introduce taasisi za kuregulate uchumi huku akiendelea kufungulia na kulea sekta binafsi. Hiyo ndiyo ilikuwa key kwa upande wangu.

Point ya kuwa na dira ya taifa pia naikubali, na utaona tangu kipindi cha mkapa, JK, na Magufuli nchi haijaweza kusimama na sera moja ambayo ilitakiwa ili kufanya mapinduzi ya kiuchumi, ni kama vile uchumi wetu umekuwa kama kuku aliyekatwa kichwa.. no direction
 
..well done.

..Tz tuna ardhi nzuri kuliko majirani wetu wengi.

..If we want to be competitive in the region, then ni lazima tuboreshe kilimo, ufugaji, na uvuvi.

..mapinduzi ya viwanda Tz yaanze na mapinduzi ya kilimo.
Yap

Na mimi huwa nafikiri kama wewe, Tanzania ni resource rich, ikiwa tutaweza kutumia tu hizi rasilimali, uchumi lazima utoke kwenye hizi levels.

Changamoto ndo kama hizo sasa kwamba... ease of doing business in Tanzania bado ipo weak, so mwisho wa siku inaua motive ya investment kwenye natural resources, mwisho was siku unajikuta tuna resources lakini nchi bado ni masikini.. ni vitu kama hivo yani
 
Mkuu uzi ni mzur na nakupongeza kwa hilo
Mimi naomba kuongezea kuhusu woga wa watanzania kwenye kufanya biashara na kenya
Watanzania ni waoga sana wa biashara nadhani ujamaa umetuathiri sanaaaa na ndo moja ya chanzo cha haya yote
Ni kama vile mfumo wa kijamaa ume corrupt akili za watanzania. Na hilo ndo tatizo maana mpaka leo hata katiba yetu bado inasema hii ni nchi ya Kijamaa. Ndo maana unakuwa na Rais haoni umuhimu wa private sekta,,, na hiyo inaenda mpaka kwenye mawazo na mtizamo wa wananchi.
 
Back
Top Bottom