Mlenge
R I P
- Oct 31, 2006
- 2,125
- 2,291
Wandugu,
Leo (Juni 30 2010) ndio mwisho wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama tunavyoifahamu, kwani kuanzia kesho (Julai mosi 2010) Tanzania itakuwa chini ya "Soko la Pamoja" la EAC. EAC ndiyo itakayokuwa imeshika hatamu za uongozi kwa vile maamuzi yake yatakuwa ya mwisho. Kwa Kiswahili kingine, huo ndio mwisho wa kuwapo kwa Tanzania kama dola na jamhuri ya muungano.
Iwapo kufuta Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni jambo zuri au baya imefikia kuwa suala la mjadala, pengine watawala wetu waliofikia maamuzi haya wako sahihi, maana miaka ya zamani, na katika nchi nyingine, kufuta 'dola' ilikuwa ni suala wanaloliita 'uhaini', na dola zilizofutika yalikuwa ni matokeo ya kushindwa vita vya moto.
La kutia mashaka, ni pale ambapo hata watawala na 'wasomi' wetu hawaelekei kuelewa nini hasa maana ya EAC. Baadhi ya wachache wanapoeleweshwa maana halisi ya EAC huja juu kwa maneno "haiwezekani! hiyo itakuwa hatari! hatutakubali! maneno unayosema ni makali sana! watawala wetu hawawezi kusaini mikataba ya namna hiyo!" n.k. n. k. n.k.
Pasipotokea serikali ya Tanzania kuzinduka kungali na mapema na kujitoa EAC na soko lao la pamoja kabla ya Julai mosi (kesho), hatari yake si kidogo.