Hatuna deni na Magufuli, kama hakukuachia maarifa basi alikuachia ujasiri

Wengi amewaacha yatima na wengine vilema vya maisha, wengine kuwafiisi, huku wengine akiwapa ubilionea kama akina Sabaya na Makonda n.k
 
Hatuna deni na huyu MwambašŸ™šŸ¼ Kama hakukuachia maarifa basi alikuachia ujasiri,Gone too soon Mwamba.
Huyu Mwamba huyu alikuwa ni kiumbe wa ajabu sana kuwahi kutokea barani Afrika.

1. Ninapoyatazama masoko nchi nzima huwezi amini kama tupo Afrika
2. Fly overs mpaka unaogopa
3. Madaraja hususani Tanzanite na Daraja la busisi, Wallah Mungu ampe pumziko la milele
4. Barabara tena mfano mmoja tu wa barabara ambayo imeishia pale Kimara..... Roho zinatuuma sana Watanzania.
5. SGR na miundombinu yake zikiwemo Tunnels pale Kilosa, aah JPM pumzika Mzee.
6. Madege na viwanja vya ndege... Kha
7. Funga kazi ni ule mradi wa kuzalisha Umeme (JNHP); pamoja na wahuni kuuhujumu lakini ule mradi unatusha.

Maswali ya kujiuliza ni kwamba huyu mwamba alitoa wapi mapesa yote haya? Jibu ni kwamba Tanzania Ina pesa ila hupigwa tu.

Swali jingine, kwa Sasa tunakwama wapi?

JPM Legacy yako haihujumki milele

R.I.P Mwamba
 
Watu wametumia billion kuhonga watoto wao wawe viongozi,
 

Attachments

  • IMG-20231223-WA0243.jpg
    IMG-20231223-WA0243.jpg
    23.2 KB · Views: 2
Wengi amewaacha yatima na wengine vilema vya maisha, wengine kuwafiisi, huku wengine akiwapa ubilionea kama akina Sabaya na Makonda n.k
Ndioo,wengi wameachwa yatima,hasa wale wapolaji,panya Road na wale waliohusika na kibiti.

Na wale wafugaji na wachimba madini,ni kweli ametuachia utajiri mkubwa,hatukusumbuliwa na hawa wanaoitwa leo ni wawekezaji kumbe ni matapeli tu.
 
Back
Top Bottom