Hatua za kupata mkopo kwa kutumia nyumba

chifu77

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
902
595
Heshima kwenu waungwana wa JF.

Naomba kufahamishwa hatua za kufuata ili kupata mkopo benki kwa kutumia nyumba kama dhamana. Kwa sasa sina hata hati ya nyumba yenyewe. Nyumba iko katika jiji mojawapo zilizoko hapa nchini kwetu. Wataalamu na wasio wataalamu ila wenye uzoefu na maswala haya msaada wenu ni wa muhimu.

Wenu katika ujenzi wa Taifa.
 
Hata uwe na nyumba 100 kama huna biashara huwezi kupata mkopo bank
Naungana na Kanga moja hapo juu kwamba hata uwe na nyumba lukuki bila biashara huwezi kupata mkopo.
Na sio Biashara tu,nikwamba biashara yenye tija na angalau uwe umeifanya si chini ya miezi sita kwa mafanikio.
 
Sasa mkuu tuseme una hako kabiashara watakayo. Enhee... hatua za kufuata ni zipi sasa.

Ukishakuwa na biashara yenye muda usiopungua miezi sita uwe na leseni ya biashara pamoja na TIN.
Cash flow ya biashara yako hapo lazima uwe na bank statement kuonyesha mapato unayoingiza, Then ndio iinakuja dhamana ya mkopo hiyo nyumba yako itathaminishwa na mkopo utakaochukua usizidi 80% ya thamani ya dhamana yako. Na kiwango cha mkopo kitatolewa kulingana na income unayoingiza kutoka kwenye biashara yako.
 
Kwa kuongeza tu, pia ni lazima uwe na mchanganuo wa biashara kuonyesha hizo fedha utazifanyia nini na hela zitarudije. Lazima afisa mikopo ashawishike kuwa mchanganuo wako unaweza kulipa ndo aruhusu uchukue mkopo.
 
Hapo kwenye hiyo pointi yako nasikia ndo mahali hao maafisa mikopo huwa wanajipigia vijisenti na wao!! Ukitaka kula inabidi na wewe ukubali kuliwa!!
 
Ama kweli.... mimi mwenyewe nahitaji mkopo ili nijikwamue halafu naanza kuliwa na bwana mkopo hata kabla ya kupata pesa yenyewe.
 
Ukishakuwa na biashara yenye muda usiopungua miezi sita uwe na leseni ya biashara pamoja na TIN.
Cash flow ya biashara yako hapo lazima uwe na bank statement kuonyesha mapato unayoingiza, Then ndio iinakuja dhamana ya mkopo hiyo nyumba yako itathaminishwa na mkopo utakaochukua usizidi 80% ya thamani ya dhamana yako. Na kiwango cha mkopo kitatolewa kulingana na income unayoingiza kutoka kwenye biashara yako.

Nashukuru sana mkuu, sasa naanza kupata mawili matatu yatakayo nisaidia katika mchakato mzima. Mkuu laki si pesa... je hiyo nyumba inahitajika kuwa na nyaraka zipi.
 
Back
Top Bottom