kapotolo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2010
- 3,727
- 2,214
Waziri wa fedha Mustapha Mkulo amesema hali ngumu ya uchumi na ukali wa maisha unaowakabili watanzania serikali haitaweza kuvitatua na amewataka watanzania wasitegemee serikali itaondoa matatizo yaliyopo na kwamba kila Mtanzania ale kwa jasho lake.
Amesema hakuna wa kulaumiwa kutokana na hali ngumu ya maisha na kushuka kwa uchumi.
Pia kamwe kodi ya mafuta haitapunguzwa na hivyo tusitegemee bei ya mafuta kushuka kwenye hii serikali iliyoko madarakani.
Gazeti la Nipashe.
Nilivyomwelewa Mkullo.
Kula kwa Jasho Sawa hakuna mtu anaetegemea kulishwa na serikali lakini serikali ina wajibu wa kuandaa mazingira ili kila mtu aweze kujipatia mlo kwa jasho lake, kama mazingira ni haya ya sasa, umeme tabu, tiba hovyo, elimu duni, miundombinu kichekesho, shillingi inaporomoka kila kukicha......hawa watanzania labda watoke damu ndio watakula kwani kwa mazingira yaliyopo jasho pekee halitoshi. Kwa kauli ya mkulo watanzania 'mtajiju', mwenye uwezo ale, asiye na uwezo alale njaa.
Lakini kama wamekubali kushindwa si watoke basi.