Hatimaye Serikali yakiri Kushindwa, Kila Mtanzania atakula kwa Jasho lake.

kapotolo

JF-Expert Member
Sep 19, 2010
3,727
2,213
Waziri wa fedha Mustapha Mkulo amesema hali ngumu ya uchumi na ukali wa maisha unaowakabili watanzania serikali haitaweza kuvitatua na amewataka watanzania wasitegemee serikali itaondoa matatizo yaliyopo na kwamba kila Mtanzania ale kwa jasho lake.

Amesema hakuna wa kulaumiwa kutokana na hali ngumu ya maisha na kushuka kwa uchumi.

Pia kamwe kodi ya mafuta haitapunguzwa na hivyo tusitegemee bei ya mafuta kushuka kwenye hii serikali iliyoko madarakani.

Gazeti la Nipashe.

Nilivyomwelewa Mkullo.
Kula kwa Jasho Sawa hakuna mtu anaetegemea kulishwa na serikali lakini serikali ina wajibu wa kuandaa mazingira ili kila mtu aweze kujipatia mlo kwa jasho lake, kama mazingira ni haya ya sasa, umeme tabu, tiba hovyo, elimu duni, miundombinu kichekesho, shillingi inaporomoka kila kukicha......hawa watanzania labda watoke damu ndio watakula kwani kwa mazingira yaliyopo jasho pekee halitoshi. Kwa kauli ya mkulo watanzania 'mtajiju', mwenye uwezo ale, asiye na uwezo alale njaa.

Lakini kama wamekubali kushindwa si watoke basi.
 
  • Thanks
Reactions: ral

tutakula Ekarist Takatifu madhabahuni. Wala asitutishe.

Kwanza Mkulo siyo Mtanzania. That's y hana uchungu na mateso yetu.
 
yale yale ya Cleopa David Msuya .... kila mtu atabeba msalaba wake
 
kila mtu ale Jasho lake, kodi zoote zifutwe, kila mtanzania ajipane kwa pesa yake, kwanza kodi inafanya kazi gani zaidi ya kupeleka wake za viongozi dubai na kupeleka watoto wa viongozi samaki samaki
 
Pamoja na hayo. Kikwete lazima atekeleze ahadi zote alizoahidi wakati wa uchaguzi ama sivyo aachie madaraka kwa vile anakaa magogoni kwa sababu huyo: at least kulingana na taratibu za uchaguzi ambao anatuaminisha kuwa alishindwa kihalali kwa sababu ya ahadi hizo.
 
Sasa kama mafuta hayatashuka bei katika serikali hii kwa hiyo suluhisho ni kuiondoa serikali iliyo madarakani kwa njia yeyote ile iwe kwa nguvu ya umma au kwa kura(tunisia au misri).
Maana inaonekana wamedhamiria hta bei ya mafuta ikishuka kwenye soko la dunia serikali yao haiwezi shusha bei hiyo
 
Bei ya mafuta huwa inashuka kwenye soko la dunia, sijawahi kuona kama bongo huwa inashuka kwa kiwango kile kile.
 
Mkullo hana hata akili hata za kuazima kauli gani ya kuwaambia wananchi kuwa serikali hali yake ni mbaya wakati juzi juzi tu benno ndulu alisema hali si mbaya hazina ina maana hapo tumuamini nani? Mkullo au ndulu?
 
Waziri wa fedha Mustapha Mkulo amesema hali ngumu ya uchumi na ukali wa maisha unaowakabili watanzania serikali haitaweza kuvitatua na amewataka watanzania wasitegemee serikali itaondoa matatizo yaliyopo na kwamba kila Mtanzania ale kwa jasho lake.

Amesema hakuna wa kulaumiwa kutokana na hali ngumu ya maisha na kushuka kwa uchumi.

Pia kamwe kodi ya mafuta haitapunguzwa na hivyo tusitegemee bei ya mafuta kushuka kwenye hii serikali iliyoko madarakani.

Gazeti la Nipashe.

Nilivyomwelewa Mkullo.
Kula kwa Jasho Sawa hakuna mtu anaetegemea kulishwa na serikali lakini serikali ina wajibu wa kuandaa mazingira ili kila mtu aweze kujipatia mlo kwa jasho lake, kama mazingira ni haya ya sasa, umeme tabu, tiba hovyo, elimu duni, miundombinu kichekesho, shillingi inaporomoka kila kukicha......hawa watanzania labda watoke damu ndio watakula kwani kwa mazingira yaliyopo jasho pekee halitoshi. Kwa kauli ya mkulo watanzania 'mtajiju', mwenye uwezo ale, asiye na uwezo alale njaa.

Lakini kama wamekubali kushindwa si watoke basi.

Ndugu zangu wana JF,

Hii si kauli ya kuiwekea mzaa.kwa kiongozi yeyote mwenye maono hawezi kutamka hivyo.Ni juzi tu nilimsikia Kikwete akizungumza suala la kupunguza kodi ili kuwapa wananchi unafuu wa maisha,leo waziri anatamka maneno ya kejeli na dharau kubwa kwa watanzania ambao wamemuweka hapo alipo na anaishi kwa kodi zao hii ni halali?
Ni lazima ufahamu wetu ufunguke,Ni mpaka lini tutaendekeza kauli hizi kutoka kwa viongozi wasio na mawasiliano?

Juzi ni Mkulo huyoyo aliyesema watajikita katika makusanyo ya kodi,atakusanya kodi ya nani ukiacha ya wafanyakazi wanaokatwa moja kwa moja toka katika mishahara yao? Hii inamaana wafanyakazi watakuwa katika hali mbaya sana.Hakuna mfanya biashara atakae endekeza hali kama hii ni kiwwa na maana wengi watakwepa kulipa kodi ama makusanyo yatapungua.

Accountability is the core element of democratic politics and good governance.when Human rights are denied from voice based approach that leads to something else.But this shows the representative of self interest,in this case the ability to demand change will be stimulated.
 
Tatizo la nchi kuongozwa na vilaza! wanajua hata sisi wote ni vilaza! Mungu ibariki TZ! hatuna serikali ila tuna wasanii.
 
Inakuwaje hakuna wa kulaumiwa? Nani anayetunga sera za maendeleo kama si serikali?

Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
 
hii ndo serikali tuliyoishagua hakuna wa kulaumu ila2015 jamani tusifanye makosa kama haya
 
Bu shit mkulo na mahayawani wote walioshindwa kuongoza nchi yetu

Baba! tunasukumwa kwa sana kuelekea njia ya tunisia,Misri, Libya.
Mkulo hakika anatuwezesha kuelekea huko tushukuru kwa hilo.
 
Amesema hakuna wa kulaumiwa kutokana na hali ngumu ya maisha na kushuka kwa uchumi.

Amesahau ni juzi tu walikuwa wana ahidi watu kwamba wataleta maisha bora kwa kila mtanzania? But that is a good statement. It shows the true colour of what ccm and its governnent is. Mlioichagua sasa "akili kumkichwa!"
 
Back
Top Bottom