Magaidi wa RENAMO hawawezi kuyumbisha maendeleo ya Tanzania kwa hiyo wana Mtwara wamekanusha vikali wanasiasa uchwara ambao hawana kazi ya kufanya bali kuchonganisha wananchi ilimradi wapate mtaji wa kisiasa. Kifo hakiepukiki kwa vyama TATA
Simwamini Pinda.....
Rejea sakata la madaktari na la Jairo!!!!!!
Huyu jamaa ni dhaifu zaidi kuliko JK
Kama wana Mtwara wamekubali kupeleka gas Dar basi wameingizwa King............. nasubiri kamatakamata siku chache zijazo!!
Anyway, Mpaka sasa sioni justification ya kutokuzalisha umeme mtwara na kuunganisha kwenye grid. Hivi hivyo viwanda ambavyo vinahitaji gas Dar kwa kiasi cha serikali kujenga bomba kwa gharama kubwa hivyo ni vipi?? Kama ni gas ya kupikia tu majumbani hivi kweli kuna haja ya kutumia gharama zote hizo kuipeleka Dar?? Pinda kapiga blah blah wananchi wanashangilia lakini ukiangalia kwa undani hakuna alichozungumza cha maana. Kama bomba ni kwa ajili ya umeme tu basi nafikiri ni vema kama Mtwara angeendelea kulikataa hilo bomba.
Kufuatia mgogoro uliodumu kwa muda sasa na kusababisha maafa makubwa huko Mtwara juu ya suala la gesi, Serikali hatimaye imeamua kunyoosha mikono kuhusu uamuzi wake wa kutaka kuipeleka gesi hiyo toka Mtwara kwenda jijini Dar es salaam.
Serikali kupitia Waziri Mkuu pamoja na Mawaziri wengine kwa upande Mmoja na Wawakilishi wa wananchi wa Mtwara imeamua kukubaliana na wananchi hao wa Mtwara walioonesha kuwa ngangali juu ya kutohamishwa gesi hiyo kwenda DSM, hivyo Gesi hiyo sasa itabaki Mtwara.
Taarifa pia inasema kutajengwa mtambo mkubwa wa uzalishaji umeme huko huko Mtwara.
My Take:
Endapo Watanzania tungekuwa na msimamo ktk mambo mengi yahusuyo Taifa kama walivyofanya wananchi wa Mtwara leo hii kusingelikuwa na Mafisadi na tungekuwa mbali sn kimaendeleo. Tunawaomba watu wa Mtwara sasa ni wakati wa kuunga nguvu kutetea twiga wetu wanaosafirishwa nje, mabilioni ya uswiss, nk. Kwa pamoja Kuifikia Tanzania tunayoitaka Inawezekana. Nazidi kuwapongeza sana wananchi wa Mtwara.
Source: Hotmix Eatv
Mhh...Mbona kuna taarifa tofauti kutoka Mtwara kwenyewe ? Angalia habari hii kutoka MTWARA KUMEKUCHA blog
MTWARA KUMEKUCHA
DONDOO MUHIMU KATIKA MAJUMUISHO
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Mstaafu Simbakalia kawaomba radhi wananchi wa Mtwara.
Waziri Nchimbi kutumia lugha kibabe na vitisho dhidi ya raia pamoja na taarifa isiyokuwa na tathmini halisi na yenye uwiano pale alipotolea mfano askari aliyevamiwa dukani/baa yake na kuibiwa pesa kiasi cha sh. 1,895,oo/= na Kupoteza mali ya sh 200,000,00/= (milioni mia mbili) na kusababisha watu wagune.
Kawambwa kawahimiza wazazi kuwaruhusu watoto kwenda shule kupata elimu sanjari na chuo cha VETA kutoa masomo ya mitaala ya gesi sanjari na uchomeleaji baharini.
Tibaijuka amezungumzia kuhusu upanuzi wa mji wa Mtwara na kuleata kauli mbiu ya "Amani na maendeleo" kutoka kwao Kagera.
Mwakyembe amezungumzia upanuzi wa bandari kavu na ujenzi wa reli Mtwara, Liganga, Mchuchuma hadi Mbamba bay na kuahidi kuja Mtwara kila baada ya miezi 3 na kujadili na kutathmini changamoto.
Waziri Mkuu ametoa udhuru wa waziri wa ujenzi Dr Magufuli ambaye alitakiwa kuwepo lakini hataweza kuhudhuria.
Bi Mapunjo kaahidi mipango mikubwa ya ujenzi wa viwanda mkoani Mtwara.
Mbilinyi kaainisha idadi ya makampuni yaliyoonyesha nia ya kuja kuwekeza Mtwara (Sina hakika sana kama ni Mtwara).
Waziri Mkuu katoa majumuisho ya ziara yake ambayo hayana tofauti na haya yaliyojadiliwa.
Kwa ufupi ni sarakasi, sanaa, ngonjera, kwaya na maigizo hakuna jipya.
Khaa!! wewe vipi?? wameshakubaliana kuwa gesi itasafishiwa Mtwra itasafirishwa hadi Dar kwa ajili kuwasha majenereta kisha umeme utarudishwa mtwara. hivyo pipeline lazima ijengwe. JIULIZE KWANZA kabla hujakurupukaWajenge viwanda na sio pipeline Wana mtwara Mimi nimeshtukia hiyo ni kupoozwa kazi iendelee naibu waziri kasema Wana mtwara hamjasoma kwa iyo fursa yenu ni kuuza chapati na mandazi kwa wachina Leo pinda anawaadaa na mambo mengi siku zote walikuwa wapi? Au baada ya kuonekana gas? Msikubali
Hakukuwa na njia nyingine zaidi ya serikali kunyoosha mikono kwa kuzingatia yaliyokuwa yanaendelea. Approach nyingine ingemwaga damu nyingi za wananchi, polisi, na viongozi pia na hakuna serikali iko tayari kwa hilo kama inataka kudumu madarakani. Hili lina negative na positive impacts kwenye Taifa hili. Lakini angalau limetuachia somo la kushirikisha wananchi katika miradi ya maendeleo, zama za ubabe na ulevi wa viongozi zimefika mwisho, kuigeuza Dar ni kila kitu ni kosa na walioamua kujiajiri kwenye ufisadi.
Siyo kuwapiga changa la macho bana, kuwapa ukweli waliokuwa wamepotoshwa!! wao blue waliambiwa ni whiteHapo kwenye RED: Jamani serkali haijasalimu amri!!! Kilichofanyika ni kuwapiga changa la macho watu wa Ntwara, basi!!!
kesho na sisi tunalianzisha huku nyamongo!!watu wa Mtwara wametutoa tongotongo!
Kama ni kweli, japokuwa simuamini Pinda basi Serkali ya kikwete itegemee migogoro mingi toka maeneo mengine! Walitakiwa kusimamia kauli sio kufuata upepo! "Dhaifu"