Hatimaye Mahakama Kuu yaamuru DOWANS walipwe

Tulisema sana humu, kesi hii TANESCO haishindi hata iende mahakama ya mbinguni. Dowans walitimiza masharti yote waliokubalina na TANESCO, walileta mitambo, inafanya kazi. Halafu uje useme sikulipi ondoa mitambo yako? huo tulisema ni upunguani wa hali ya juu.

Sasa wajiandae kulipa hizo na gharama za kesi na malimbikizo ya riba toka walipokaidi amri ya ICC. Itabidi walipe mara mbili ya hizo kwa ujinga tu wakutaka kudhulumu.

Zitto na Rashid Idriss na wengine tulioona mbali kuhusu hili sakata, tulisema, tukubali tu kuinunuwa hiyo mitambo iwe yetu na hili sakata liishe kwani kupinga ni kujitafutia matatizo, na kweli, Dowansa wakashitaki Kimataifa wakashinda, tukasema tena walipwe tu, watu wakajifanya wajanaja eti wakaenda kushtaki Uingereza, huko nako wakapigwa chini.

wewe sasa unamlaumu nani hapa? Na wanaofanya haya madudu yote si ni serikali yako ya ccm ambayo unajitahidigi kuitetea kuwa ipo kwa maslai ya wananchi? Wewe ukiitwa pungu one je utamlaumu mtu?au utamlaumu maana wewe ni pungu one
 
wewe sasa unamlaumu nani hapa? Na wanaofanya haya madudu yote si ni serikali yako ya ccm ambayo unajitahidigi kuitetea kuwa ipo kwa maslai ya wananchi? Wewe ukiitwa pungu one je utamlaumu mtu?au utamlaumu maana wewe ni pungu one

Teh teh teh! Mkuu unaogopa ban!
 
Ile ya mahanga na lema?


Mahakama haifanyi kazi kwa kumridhisha mtu, kuna Mbunge mmoja(Sebastian Mkiza Kinyondo-kama siijakosea) amewahi kuvuliwa ubunge akiwa Waziri. Waulize hata wanasheria nguli watakwambia ukweli, ile kesi tusingeza kushinda kupitia sheria labda kama tukiamua kutumia mabavu.
 
Wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine kuiingiza Tanesco katika mkataba tata na richmond na baadae dowans inabidi mali zao zikamatwe na kupigwa bei ili lipatikane fungu la kuwalipa dowans.
Watanzania ni lazima tukatae huu wizi wa mchana tunaotaka kufanyiwa hapa.

Na Sitta je aliyefunga mjadala bungeni kabla hajutaifisha mitambo ya Dowans? naye ana kesi ya kujibu hapa tusingefika huku kama tungeitaifisha mapema mitambo ya matapeli hawa
 
wakilipwa nasubiri kuona MWAKYEMBE na SITTA wakijuzulu la sivyo nitaamini wamwhongwa vyeo ili wawasaliti watz

namsubiri SITTA kwa hamu. mzee wakuropoka achukue maamuzi magumu kama kweli ni mzalendo kama anavyodai na kujisifu na kukandia wenzake

Amini nakwambia, kabla ya Jumapili, waziri Sitta atakuwa ameshajibu hoja yako hii

 
...Kikwete na mafisadi wenzie ndani ya magamba wameshakaa mkao wa kula wakisubiri mgao wao.
 
Kutopatikana kwa majibu sahihi ya maswali haya kunaniuma sana. Nakumbuka JK anawambia wanaccm wenzake kuwa naye hajui..wakambigia makofi mkutanoni Kimwaga. Baadae kidogo nikasikia sijui mmiliki ni mwaarabu fulani... Kichefuchefu...

wakati mitambo ikiwa ya mwarabu ukaiona ukaiona kichefuchefu...huyo mwarabu nakumbuka hadi alitoa offer waongee ,awauzie mitambo na ikibidi asamehe deni watu wakawekamo siasa.
Leo hii mitambo kanunua mzungu na anaendelea kuwakamua mabilioni kwa siku na hausikii kichefuchefu.
Mtawakumbuka kina zito waliosema tuinunue mitambo.
 
wakati mitambo ikiwa ya mwarabu ukaiona ukaiona kichefuchefu...huyo mwarabu nakumbuka hadi alitoa offer waongee ,awauzie mitambo na ikibidi asamehe deni watu wakawekamo siasa.
Leo hii mitambo kanunua mzungu na anaendelea kuwakamua mabilioni kwa siku na hausikii kichefuchefu.
Mtawakumbuka kina zito waliosema tuinunue mitambo.

Ni kweli kabisa, wanajifanya wamesahau. Zitto alisema jamani tuinunuwe, ni faida kwetu, watu wakamtukana sana humu JF na wakamponda sana na wengine tuliotetea hiyo mitambo ilnunuliwe tukaitwa kila jina, upinzani humu ukiongozwana Mzee Mwanakijiji.

Ndio maana huwa namuuliza, vipi? mbona ya Symbion husemi? anakaa kimya kwa kuona haya.
 
Last edited by a moderator:
Serikali itupunguzie hii mizigo ya kisaikolojia, iwalipe DOWANs (whoever they are) pesa yao yote mara moja waanze kuifaidi kama walivyopangilia toka mwanzo. Tumetoka kufadhaika na mateso ya Ulimboka, mauaji ya kishenzi ya Mwangosi halafu tuzidi kuendelea kuugua na DOWANs? Mpaka tumeanza kusahau kama siye ni taifa au mkusanyiko wa watu wa ajabu (aliens). Give us a break please!
 
Ni kweli kabisa, wanajifanya wamesahau. Zitto alisema jamani tuinunuwe, ni faida kwetu, watu wakamtukana sana humu JF na wakamponda sana na wengine tuliotetea hiyo mitambo ilnunuliwe tukaitwa kila jina, upinzani humu ukiongozwana Mzee Mwanakijiji.

Ndio maana huwa namuuliza, vipi? mbona ya Symbion husemi? anakaa kimya kwa kuona haya.

Labda hujui msimamo wangu toka awali ni nini? jaribu kusearch hapa na utajua position yangu. Utanunua vipi mtambo ambao umeuziwa kwa hila? inaonekana hulijui vizuri sakata la Dowans...
 
Kwani kuna mtu aliyekuwa anafikiri tofauti na matokeo haya?

Yani msimlipe Al Adawi? Si atakuja kuchukua twiga na simba wote mbaki na nyumbu tu.
msoga town, mkulima wa mananasi.
 
Last edited by a moderator:
NAPENDA KULIARIFU BUNGAE LAKO TUKUFU SERIKALI IMEPATA USHAURI WA KUVUNJA MKATABA HUU TOKA KWA KAMPUNI YA KISHERIA ILIYOBOBEA KWENYE MIKATABA YA KIMATAIFA. Hiyo ni kauli nzito toka mh waziri mkuu akilihakikishia bunge na taifa kwa ujumla. REX ndo iliishauri serikali kuvunja mkataba wakalipwa mapesa kwa kazi nzuri ya kuishauri vema serikali. REX wameenda mahakani kutetea walichoshauri na kuiaminisha serikali WAMEBWAGWA. JE REX BADO WANAFABNYA KAZI YA USHAURI NDANI YA MIPAKA YA NCHII?? KAMA NDIO KWA NINI NA NANI YUPO NYUMA YAO. wakuu sitaraji kampuni kama hiyo kuendelea kufanya kazi za kisheria maana imedhihiri kuwa si wabobezi wa sheria si tu za kimataifa bali pia hata za tanzania. vinginevyo nambieni NANI YUPO NYUMA YA HAWA R E X ????????????SHIIIIIIIIIT
 
Labda hujui msimamo wangu toka awali ni nini? jaribu kusearch hapa na utajua position yangu. Utanunua vipi mtambo ambao umeuziwa kwa hila? inaonekana hulijui vizuri sakata la Dowans...

Hakuna hila wala ila. Wewe simply hujui biashara ni nini. Mbona mitambo hiyohiyo imenunuliwa na Symbion na ukakaa kimya? Leo mbio mbio umekuja na kusema nini? Hivi majaji wote wa ICC, wa Uingereza, wa Tanzania hawajui kama kuna hila au la, unaejuwa ni wewe? ambae hujafanya biashara yoyote ya maana duniani zaidi ya kuandika vingi usivyovielewa na kufata emotions zako zaidi ya kuufata ukweli ulivyo.
 
Hii ni furaha kwa kikwete, lowasa na rostam kwani diri lao sasa limkamilika pamoja na kuwazuia kujichotea 152,000,000 kila siku kipindi kile.......
Kweli ta kichwa cha mwenda wazimu
 

Mafisadi wailipe Dowans - Mnyika

na Mwandishi wetu
Tanzania Daima


SIKU moja baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kulitupilia mbali ombi la Shirika la Ugavi wa Umme nchini (TANESCO) la kutaka izuie utekelezwaji wa ulipwaji wa fidia ya Kampuni ya Dowans Tanzania Ltd, Waziri Kivuli wa Nishati na Madini, John Mnyika, amesema mafisadi waliohusika ndio wabebeshwe hasara hiyo badala ya wananchi.

Juzi, mahakama hiyo, ilitupa ombi la TANESCO lililokuwa likiomba itoe amri ya kuzuia utekelezwaji wa ukazaji wa hukumu ya mahakama hiyo iliyoruhusu tuzo ya dola 65,812,630.03 za Marekani iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Kibiashara (ICC) mwaka 2010 kwa Kampuni ya Dowans Hodlings SA (Costa Rica), sasa Dowans Tanzania Ltd isajiliwe hapa nchini.

Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Ubungo (CHADEMA), alitoa kauli hiyo jana kupitia taarifa yake aliyoisambaza kwenye vyombo vya habari akisema kuwa serikali isitumie kizingizio cha uamuzi wa mahakama kuharakisha mpango wa kulipa Dowans kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania.

Vile vile, Mnyika alisema kuwa ikiwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete imezidiwa na Dowans kwa sababu ya kujiingiza katika mikataba mibovu, inapaswa kuwabebesha deni hilo wazembe, mafisadi na waliokuwa wakihujumiana na kusababisha hasara hiyo.

"Serikali kupitia Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, anapaswa kueleza ni hatua gani ilichukua kutoka TANESCO ilipowasilisha Mahakama ya Rufani taarifa ya kusudio la kupinga hukumu iliyotolewa na Jaji Emilian Mushi, Septemba 28 mwaka jana ikiruhusu tuzo hiyo isajiliwe," alisema.

Aliongeza kuwa, Mwanasheria Mkuu wa Serikali naye anapswa kueleza ni kiasi gani cha fedha kilichotumika kwenye kuendesha kesi za Dowans na IPTL mpaka sasa na hatua zilizochukuliwa dhidi ya mawakili wa TANESCO na makampuni binafsi yanayotuhumiwa kusababisha mzigo mkubwa wa gharama za kesi ambazo serikali inashindwa.

"Ni muhimu umma ukafahamu kuwa kwa mwaka wa fedha 2011/2012 pekee, jumla ya sh bilioni 10 zimetumika kwa ajili ya gharama za kuendesha kesi hizo kwa kuilipa Kampuni ya Rex Attorneys na makampuni mengine ambayo kwa nyakati mbalimbali yamekuwa yakiiwakilisha serikali na TANESCO," alisema Mnyika.

Alishauri kuwa hukumu ya juzi inapaswa kuibua tena mjadala uliodumu kwa miaka minne, kuanzia mwaka 2008 tangu yalipopitishwa maazimio 23 ya Bunge juu ya mkataba baina ya TANESCO na Kampuni ya Richmond Development Company LLC ikiwamo kuhusu mkataba na Dowans.

Alisema katika mazingira hayo, Waziri Muhongo anapaswa kueleza kwa umma ni mabilioni mangapi yamelipwa na TANESCO mpaka hivi sasa kwa kampuni hiyo na nyingine.

"Kama hoja binafsi niliyoiwasilisha ofisi ya Bunge mwaka jana kutaka utekelezaji wa maazimio yote yaliyobaki kuhusu mkataba kati ya TANESCO na Richmond ingejadiliwa bungeni, hatua zaidi zingechukuliwa kwa mafisadi na wahujumu uchumi waliohusika," alisema Mnyika ambaye pia ni Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA.

TANESCO wanena
Wakati huo huo, TANESCO imesema kuwa hakuna hukumu yoyote iliyotolewa na Mahakama Kuu kuamuru shirika hilo kuilipa Dowans dola za Marekani milioni 96.

Taarifa iliyotolewa jana jioni na ofisi ya uhusiano ya TANESCO, ilisema kuwa kilichoamriwa na Mahakama Kuu ni kwamba Mahakama Kuu haina mamlaka ya kusikiliza utekelezaji wa hukumu ya ICC, hivyo mamlaka hayo yapo katika Mahakama ya Rufaa.

"Kwa sasa TANESCO imepeleka ombi la kuzuia utekelezaji wa hukumu ya Mahakama ya ICC kwenye Mahakama ya Rufaa Tanzania na hatimaye kuendelea na taratibu za kukata rufaa," ilisema taarifa hiyo.

 
Back
Top Bottom