Hatimaye EU wakubali kutoa Sh. 860 billioni za maendeleo

Inatakiwa tuwe tayari kwa kibano, nchi yoyote haiwezi kuendelea kwa kutegemea misaada. TUkikosa misaada wananchi wakakosa huduma tutapata akiri ya kuweza kujua nani haswa anakwamisha maendeleo ya Mtanzania.

Watanzania wataweza kutoa haki ktk hili lakini hawa wanaoendelea kuleta misaada wanazidi sana sana kuwanufaisha watu ambao wanaziweka mifukoni na mwisho wa siku kuzitumia vibaya tusiweze kupata maendeleo.

Lazima hata viongozi wakose mahala pa kuchota fedha za bure hili wasipate pesa za kununua kura kwa wananchi wa kawaida. Na hata wakipata wananchi wawe tayari wameisha fikia wakati wa kujua nini maana ya uchaguzi hili waweze kutoa haki ya kupiga chini viongozi waliosoma jinsi ya kuwa MAFISADI na wasioweza kutatua matatizo ya wananchi.
 
The right move but bit to late, wakitusaidia tutashinda ufisadi na kukomesha kuone watu wenye ushaidi na kuwambambikia kesi bila sababu ya msingi.
 
Mimi binafsi naona kama kibano kimeshaanza, na nimekulia enzi za Nyerere wakati sabuni ya Foma ilikuwa kama almasi pamoja na colgate! So no problem, bring it on! Lakini naomba baada ya dhiki kweli tupate faraja. Je Morani, wewe uko tayari kwa ajili ya kibano hiki?

Sus....., hapo ndipo pake haswaaa.... Kumbuka wakati wa kupata colgate za magendo kama ulivyosema, pia si unakumbuka wakati wa maduka ya kaya na kununua vyakula muhimu (mchele, sukari, mafuta etc) kwa kutumia daftari?? Hii ilikuwa ni mapema miaka ya 80, then tukapata ule msimu wa Mzee Ruksa mambo yalipowa kila kitu mpaka TV zilikuja nchini, then ilikuwa dhiki (up to early 80s) faraja ikaja (late 80s to 90s). Kibaya ni kwamba ile faraja tuliishia kuiharibu kwa kuifanya iwe ya wenye nafasi/uwezo!!!

Binafsi kama niliweza vumilia dhiki wakati ule, why not now? Nipo tayari Mkuu!! Ila naendelea kujiuliza kama hii haitakuwa kama ile faraja ya early 90s ambayo tuliishia kuiharibu (uongozi/tamaa/ubinafsi??)
 
Iyo feza ikikosekana watakaoumia ni raia ,kwani MaCCM magogo na Magome wao tayari wanamiliki migodi na miradi ya serikali ambayo haihitajii misaada kutoka nje,si hasha ukasikia kesho yake wanarapu na kusema kama misaada hiyo ni kwa masharti ya kuwakamata wenzetu bora ibakie huko huko.
Lakini wananchi watapata tabu sana kwani hali ya maisha itabadilika kwa kasi,kwa upande mwengine itasaidia sana upinzani kwani wananchi wataonja joto la kuwatandikia mafisadi mazulia na kuwapokea kama mashujaa,maana wale wananchi waliofanya masherehe wamewashangaza hata hao wanaotoa misaada ,vipi wahujumu Uchumi wanapokelewa kama wafalme ,ndio nao wamezidisha kukaa mbali na watu wasiojijua.
Pia watu wa vijijini ambao wakiona mashule na mabarabara yanajengwa wanazani ni kutokana na nguvu za CCM yaani hawaelewi kabisa kama feza ile sio inayotokana na hazina ya Taifa bali ni misaada kutoka kwa wafazili ,hawafahamu kama feza ya hazina ni ile inayoliwa na vigogo na makunguni wakubwa wakubwa.Hili joto linastahili kufika kila kona ya Tanzania ili wavijiji waingie akili.
 
Unajua Mwiba ukianza kutawala watu wenye njaa sana wakati wewe unaendelea kutanua basi huwe tayari kuweka uzio hili wasiweze kukufikia hila mwisho wa siku mambo yanaweza kukuwia mabaya.

Jinsi maisha ya wananchi yatakavo zidi kuwa mabaya ndivyo watawala watakavyokuwa wanakosa amani. Wakati wa nyerere watu tulifunga mikanda maana alikuwa ni kiongozi wa watu(mwadirifu). Leo hii uadirifu hakuna hivyo wananchi wakianza kukosa matumizi kwa sababu ya kuwa na viongozi wasioweza either kuwashughulikia Mafisadi au viongozi wenyewe ni mafisadi hujue tunaelekea kwenye uwanja mzuri sana.

Yaani tunatoka uwanja wa taifa wa zamani(wa vumbi) kuingia katika uwanja wa taifa wa kisasa. Hujue tutakuwa tunaelekea katika kuzamisha gurudumu la viongozi MAFISADI.

Hawa hawakosi misaada kwa kulinda maslahi ya taifa hila watakosa misaada kwa kulinda na kutetea ufisadi ambao wananchi itatakiwa tuwashughulikie pia.
 
Heshima mbele.... Kuna ndugu aliwahi kusema, "Ni bora kupata kibano kwa kipindi kifupi ili upate starehe/raha ya muda mrefu au kwa vizazi vijavyo".

Swali ni, Je tupo tayari kupokea kibano kwa ajili ya mabadiliko???
Hata tusipokitaka si kipo tu ndugu yangu? Maana hata wakitupa wafadhili vipesa vyao bado wanazifisadi! sasa hiki si kibano pia? kwa hiyo tupo katika kibano jamaa yangu.
 
Waziri wa Fedha atoka mikono mitupu kwa wafadhili
*Waendelea kuzuia fedha zao za bajeti 2008/09
*Wanataka kibano kwa mafisadi wa EPA, BoT


Na Boniface Meena


NCHI 14 wahisani zinazochangia bajeti ya serikali, jana zilishindwa kueleza ni lini zitaanza kutoa fedha walizoahidi kwenye bajeti ya mwaka 2008/09 kwa kile walichosema wanasubiri hatua kuchukuliwa dhidi ya wahusika katika kashfa mbalimbali za ufisadi.


Jana wafadhili hao walikutana na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, jijini Dar es Salaam katika moja ya mikutano yao na serikali kujadili maendeleo yatakayowawezesha kuamua kutoa fedha, lakini hawakutamka ni lini hasa watatoa fedha ambazo zimeahidiwa kwenye bajeti ya mwaka huu.


Taarifa ya maandishi kwa gazeti hili kutoka kwa Mwenyekiti wa kundi la wafadhili hao 14 ambaye pia ni Balozi wa Denmark nchini, Bjarne H. Sorensen, ilisema: "nathibitisha kwamba kundi la nchi wafadhili lilifanya mkutano na Mheshimiwa Mkulo, Waziri wa Fedha na Uchumi.


"Mkutano huo ni sehemu ya mikutano ya kawaida na mijadala ya tunayofanya na Mheshimiwa Waziri, ambako hujadili na kuangalia maendeleo muhimu yatakakayotupa fursa ya kuamua ni lini tutaanza kutoa fedha kwa bajeti ya 2008/09."


Kutokana na kauli ya wahisani hao, inaonekana bado wanaendelea kuiminya serikali hadi itakapochukua hatua zilizopendekezwa dhidi ya watuhumiwa wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA); ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).


Msimamo huu unakwenda sambamba na kauli waliyotoa wakati wakiridhia kusaidia katika bajeti ya mwaka huu, wakisema:


"Kabla ya kutoa fedha kusaidia bajeti tunatazamia kupokea taarifa zaidi za utekelezaji wa namna serikali inavyopambana na tuhuma za rushwa, kuboresha utawala, na utekelezaji wa mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) yaliyohusu ukaguzi wa hesabu za Benki Kuu ya Tanzania kwa mwaka wa fedha wa 2005/06."


Waziri Mkulo jana aliulizwa juu ya mkutano wake na wafadhili na maamuzi waliofikia, alisema kuwa mambo waliyokubaliana ni mazuri na yanakwenda vizuri.


�Mambo yamekwenda vizuri lakini ni vizuri ukawasiliana na Balozi wa Denmark kwani ndiye atakayetoa msimamo wa tuliyokubaliana ili kuondoa kwamba waziri kasema hivi balozi kasema vile,� alisema Mkulo.


Wafadhili hao wameahidi kuchangia asilimia 34 kwenye bajeti ya mwaka huu ya Sh 7.2 trilioni, hali ambayo inaiweka serikali kwenye wakati mgumu kama hazitatolewa kwa wakati kwani ndizo zinategemea kuendesha miradi ya maendeleo.


Mara ya mwisho wafadhili kuibana serikali katika bajeti yake ni wakati wa utawala wa Rais wa awamu ya pili ya Ali Hassan Mwinyi, waliokataa kufadhili Tanzania kutokana na serikali kushindwa kukusanya kodi kiasi cha Sh bilioni 70 wakati huo.


Makusanyo ya kodi serikalini wakati huo, yaani 1995, ilikuwa ni Sh 28 bilioni kwa mwezi. Kiasi kikubwa cha kodi ambazo hazikukusanywa ilikuwa ni misamaha ya ovyo ya kodi pamoja na wafanyabiashara wakubwa kukwepa kodi. Hali hiyo ilidhibitiwa baada ya Rais Benjamin Mkapa kuingia madarakani
 
Wito kwa wafadhili:

Ni kwamba msitoe pesa hata kidogo kwa serikali yetu ya Tanzania. Tanzania si nchi masikini kama mnavyoelezwa. Tanzania tuna pesa na malighafi za kutosha sana. Hatuhitaji msaada wa pesa hata kidogo.

Cha maana kwa sasa ni kumueleza Mkulo akusanye pesa ya EPA, Richmond, kumshauri Kikwete kupunguza safari, na kuacha kuwanunulia viongozi magari ya kifahari hiyo inatosha kabisa kukidhi mahitaji ya bajeti yetu.

Mimi kama mwananchi mwenye uchungu na nchi yangu naomba tusipewe msaada huo wa pesa kwani utatuletea mabaraa tupu badala ya kutuletea mema.

Tumechoka kuonekana wapumbavu na viwete, tumeshapewa misaada mingi sana lakini misaada hiyo imekuwa chanzo cha matatizo ndani ya nchi yetu. Watanzania hatuhitaji misaada ya pesa nadhani tunahitaji misaada ya ushauri na utaalamu jinsi gani ya kuendelea kwa kutumia rasilimali zetu tulizokuwa nazo.

Ni kichekesho kikubwa waziri wetu wa fedha anakwenda kuomba pesa kwa wafadhili kiasi ambacho hakizidi kile kilichoibiwa katika skendo la EPA.

Huu ni upumbavu na ujinga. Samahani wana JF kwa lugha hii.
 
Heshima mbele.... Kuna ndugu aliwahi kusema, "Ni bora kupata kibano kwa kipindi kifupi ili upate starehe/raha ya muda mrefu au kwa vizazi vijavyo".

Swali ni, Je tupo tayari kupokea kibano kwa ajili ya mabadiliko???


Nadhani Watanzania wengi wataunga mkono maamuzi ya wafadhili kutotoa pesa zao maana wanaofaidika na pesa hizo ni mafisadi tu, hivyo hata zikikosekana Watanzania walio wengi hawataona tofauti kubwa maana tayari wanaishi maisha ya dhiki kubwa.
 
Hakuna sababu za wao wafadhili kutupa pesa kama pesa zinatumiwa na hao wachache.

Na madai yao ni ya msingi sana uwezi kumpatia mtu hela aka misuse.
 
Chonde chonde wafadhili, msitoe pesa hizo hata kidogo. Msidanganywe na Serikali ya Tanzania kwamba eti hatuna pesa. Pesa tunazo lakini hatujui kupanga matumizi yetu (priority) na wizi umekithiri mno.

Viongozi wetu ni wezi wa kutisha, wamekuwa wakijunufaisha wao zaidi kuliko nchi ingawa wamekuwa wakitumia jina la Tanzania kuombea misaada hiyo.

Hii ni sawa na Baba kuomba mkopo ama msaada kwa jina la familia kwamba haina chakula ama ada za shule kumbe Baba huyo anamalizia mapesa ya msaada na mikopo kwenye kunywa pombe na kiti moto huku familia nyumbani haijui chochote kuhusu misaada na mikopo hiyo.

Ndugu wana JF tupige debe sana kuwaomba hawa wafadhili wasitoe pesa hizo kabisa.
 
Waungwana itakuwa si vibaya tukiandika barua kwa nchi zote za wafadhili kuwaunga mkono katika uamuzi wao wa kutotoa pesa ili kusupport budget ya 2008/2009 mpaka hapo wahusika wote na ufisadi wa EPA watakapotajwa hadharani na hatimaye kufunguliwa mashtaka.
 
Waungwana itakuwa si vibaya tukiandika barua kwa nchi zote za wafadhili kuwaunga mkono katika uamuzi wao wa kutotoa pesa ili kusupport budget ya 2008/2009 mpaka hapo wahusika wote na ufisadi wa EPA watakapotajwa hadharani na hatimaye kufunguliwa mashtaka.

Hili ni wazo zuri sana. Wana JF kwa pamoja tunaweza kuandika barua na kuzifikisha kwa wafadhili ili kuomba ili suala lifanyike hivi tunavyotaka. (NO MISAADA KWA TANZANIA MPAKA PESA ZA EPA ZIRUDI NA WAHUSIKA KUCHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA)

Mzee Mwanakijiji na Invisible mnasemaje kwa hili?
 
Date::9/18/2008
Hatimaye EU wakubali kutoa Sh860bilioni za maendeleo
Boniface Meena
Mwananchi

NCHI 14 washirika wa maendeleo katika Mpango wa Kuchangia bajeti ya Tanzania (GBS) wamepanga kuipatia serikali Sh860bilioni (sawa na Dola 750milioni za Marekani) kwa ajili ya mwaka wa fedha 2008/09 ambayo ni sawa na asilimia 12 ya bajeti yote ya serikali.

Kiwango hicho ni pungufu kwa asilimia 22 ukilinganisha na asilimia 34 ambazo washirika hao waliahidi kutoa katika bajeti nzima ya serikali ambayo ni Sh7.2 trilioni.

Uamuzi wa kutoa msaada huu umetokana na mazungumzo ya karibu baina ya washirika wa maendeleo pamoja na Serikali ya Tanzania, mazungumzo yaliyochukua miezi tisa baada ya kashfa za ufisadi kuwafanya wasitishe kuanza kutoa fedha hizo za msaada kwenye bajeti ya Serikali ya Tanzania.

Balozi wa Denmark nchini, Bjarne H Sorensen, ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa kundi la nchi 14 washirika wa GBS, alisema jana kuwa washirika wote wa mpango huo wamethibitisha kutoa mchango wao kwa mwaka huu wa fedha.

"Hii inadhihirisha kuheshimu ahadi zetu kwa maendeleo ya Tanzania," alisema balozi huyo. "Serikali ya Tanzania imeimarisha usimamizi katika Benki Kuu pamoja na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya maofisa wanaohusika.

"Uchunguzi juu ya suala la EPA umefikia hatua nzuri, ikiwa ni pamoja na kuweza kurejeshwa kwa baadhi ya fedha zilizochukuliwa na kuwagundua wahusika. Serikali imetuhakikishia kuwa uchunguzi utaendelea mpaka kufikiwa kwa hitimisho kamili.


"Tanzania imepata maendeleo muhimu. Lakini hakuna shaka kwamba changamoto bado zipo. Tutazitilia mkazo changamoto hizi wakati washirika wa GBS na serikali kwa pamoja tutakapotathmini maendeleo yaliyofikiwa katika mkutano utakaofanyika Novemba mwaka huu."

Aisema washirika hao wanataka kufanya kazi na serikali na asasi za kiraia ili kupata fursa za kukuza uchumi, na kuhakikisha kwamba Watanzania walio masikini zaidi wananufaika na mpango huo.

Pia alisema: "Uwajibikaji wa ndani ni kitu muhimu sana. Na katika jambo hili tumetiwa moyo na mchango unaotolewa na vyombo vya habari, asasi za kiraia na Bunge katika kuendeleza uwajibikaji.

“Mpango wa GBS unaipatia Serikali uwezo na motisha katika kuimarisha uwezo wake wa kubuni, kutekeleza na kufanikisha mipango yake ya maendeleo kwa muda mrefu na njia endelevu zaidi. Tutaendelea kufanya kazi pamoja na serikali kwa ukaribu ili kuhakikisha kuwa malengo na vipengele vya GBS vinaendelezwa,” aliongeza Sorensen.

Washirika wa maendeleo ambao wako kwenye mpango huo wa GBS ni Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Canada, Denmark, Kamisheni ya Nchi za Ulaya, Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Uholanzi, Norway, Sweden, Uswisi, Uingereza na Benki ya Dunia.

Wakati washirika hao wakiridhia kutoa fedha hizo, serikali jana ilipokea kiasi cha Sh216 bilioni kutoka serikali ya Uingereza, ikiwa ni sehemu ya mpango wa GBS.

Akizungumza na waandishi wa habari, waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema serikali ya Uingereza ni moja ya nchi 14 washirika ambao husaidia bajeti kuu ya Tanzania kwa ajili ya kusaidia maendeleo.

Alisema misaada hiyo huenda moja kwa moja kwenye bajeti ya taifa na kuiwezesha serikali kutoa fedha katika sekta za maendeleo zilizopewa kipaumbele na kufanikisha Mkakati ya Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi Tanzania (Mkukuta)

Taarifa ya maandishi kwa gazeti hili ya Julai 19 kutoka kwa Sorensen, ilithibitisha kwamba kundi la nchi hizo washirika lilifanya mkutano na Mkulo, ikiwa ni sehemu ya mikutano ya kawaida na mijadala wanayofanya na serikali hujadili na kuangalia maendeleo muhimu yatakayotoa fursa ya kuamua ni lini fedha hizo zianze kutolewa kwa bajeti ya mwaka 2008/09.

Katika taarifa hiyo, ilionekana kuwa washirika hao walikuwa wanasita kutoa fedha zao kusubiri hatua kuchukuliwa dhidi ya mafisadi, hasa katika sakata la wizi wa fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ufisadi ndani ya Benki Kuu ya Tanzania na taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

Msimamo huu ulikwenda sambamba na kauli waliyotoa wakati wakiridhia kusaidia katika bajeti ya mwaka huu, waliposema: "Kabla ya kutoa fedha kusaidia bajeti hii, tunatazamia kupokea taarifa zaidi za utekelezaji wa namna serikali inavyopambana na tuhuma za rushwa, kuboresha utawala bora na utekelezaji wa mapendekezo ya CAG yaliyohusu ukaguzi wa hesabu za Benki Kuu ya Tanzania kwa mwaka wa fedha wa 2005/06."

Wafadhili hao waliahidi kuchangia asilimia 34 ya bajeti ya mwaka huu ya Sh7.2trilioni, hali ambayo iliiweka serikali kwenye wakati mgumu kama fedha hizo zisingetolewa kwa wakati kutokana na fedha hizo kutegemewa kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mara ya mwisho washirika hao kuibana serikali katika bajeti yake ilikuwa wakati wa utawala wa serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa chini ya Rais Ali Hassan Mwinyi. Katika kipindi hicho, washirika hao walikataa kufadhili Tanzania kutokana na serikali kushindwa kukusanya kodi kiasi cha Sh70bilioni kwa wakati huo.

Wakati huohuo, serikali ya Marekani imesema Tanzania itahatarisha misaada yake kutoka nchini humo kama itagundulika kwamba misaada hiyo inatumika vibaya au kuishia katika mifuko ya viongozi mafisadi.

Akizungumza katika semina iliyoandaliwa na ubalozi wa Marekani nchini na kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Blue Pearl iliyo kwenye jengo la Ubungo Plaza, balozi wa Marekani nchini, Mark Green alisema wamarekani wanaisaidia sana Tanzania katika mambo mbalimbali, lakini iwapo watagundua kwamba misaada hiyo inatumika vibaya au kuishia katika mifuko ya viongozi mafisadi, watasitisha.

“Sisi ni wakarimu sana, lakini si wapumbavu kama Rais George Bush alivyosema wakati alipoitembelea Tanzania Februari mwaka huu kwamba 'hatutoi fedha zetu kwa mataifa ya kifisadi,'” alisema Green.

Alisema juhudi za Serikali ya Tanzania katika kupambana na ufisadi zinaonekana na imeifanya nchi kupata jina zuri katika jumuiya ya kimataifa, ikiwa kama mwanzilishi wa kweli wa vita dhidi ya ufisadi.

Alifafanua kuenea kwa programu za Mifumo ya Kufuatilia Matumizi ya Umma (PETS), kumesaidia sana katika kuipatia Tanzania jina zuri mbele ya jumuiya ya kimataifa.

“PETS inawafanya watumishi wa Umma kukumbuka kwamba kuna watu wanawaangalia na sio viongozi tu, bali watu wa kawaida na imewasaidia Watanzania wa kawaida kujiamini kwamba serikali yao inalinda maslahi ya walio wengi na si ya mtu mmoja mmoja,” alisema Green.

Alieleza kwamba katika hatua za awali za PETS wametoa mafunzo kwa zaidi ya waandishi 280 wa habari katika kuandika habari za uchunguzi, kutoa vifaa na mafunzo ya kupambana na ufisadi pamoja na kumsaidia mnunuzi mkuu wa vitu vya serikali katika kufanya ukaguzi wa manunuzi ndani ya mashirika mbalimbali ya kiserikali.

Katika hatua hiyo ya awali ambayo itamalizika mwishoni mwa mwezi huu alisema bila ya shaka kazi hiyo itaendelezwa na wale waliopatiwa mafunzo hayo.
 
Hivi ndivyoninavyoipenda serekali yangu ya TANZANIA wamewezawapiga magoli wahisani na pesa zinatolewa kwa ulani hongera sasa kazi nikurudi kwa wananchi na kuwalaza chali tuendelee na mchakato wamaisha
 
Narudia tena na tena na tena, hatuhitaji michango hii katika maendeleo yetu.Tunachohitaji ni kujipanga vizuri ili tu 'take off.'
 
Upokeaji wa misaada ni laana ya aina yake tuliyoshindwa kuipigia ramri, mwishowe kitafikia kizazi cha nne tokea uhuru laana hii ikiwa bado nasi!!
 
Back
Top Bottom