Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Hii tabia yakuvutia mambo mazuri nyumbani kwa mtawala ipo siku yataligawa taifa, tutaanza kuchaguana kimakabila na kikanda kwa maana mkikosa mtu maendeleo hayaji.
Enewei huku Tanga tunasubiri upanuzi wa Bandari Itabidi tufanye jambo Shemweta nae aingie nyumba kubwa.
 
Nimesoma mada kwa marefu na mapana yake,bahati mbaya wapo baadhi ya wachangiaji wana viwango vidogo sana vya uchangiaji.Hatuna namna ya kuwaondoa labda mods wangeweza kusaidia.

Mfano mleta mada kaeleza vizuri kwanini ujenzi wa uwanja CHATO ni kukosa mwelekeo,anakuja mtu utadhani kalazimishwa kuchangia "Eti kwani Chato ipo Sudani" mwingine mbona KIA ilipojengwa Bomang'ombe kulikuwa na nini.Unabaki kushangaa na kujiuliza maswali kibao ni jinsi gani shule,college... vimezalisha watu wa hovyo kwa kiwango hiki.Watu hawapendi kushughulisha bongo zao wanasema hovyo hovyo.

Nirejee kwenye mada.

Mosi,Ujenzi wa uwanja wa CHATO ulikuwepo katika mipango tangu mwanzo au uliibuka baada ya Dr Magufuli kuchaguliwa ?.Katika ilani ya CCM ujenzi wa viwanja vya ndege kiwanja cha ndege cha Chato kipo ?.

Pili,Ujenzi wa uwanja wa ndege unaambatana na sababu za kiuchumi,kijamii,kiusalama na nk.Kabla ujenzi haujaanza mambo yote yalingatiwa au tuliamua kwakuwa Rais anatoka eneo hilo,ikiwa ni hivyo maana yake tutakuwa tunafanya maamuzi kwa kuangalia maeneo wanakotoka viongozi na si kuangalia sababu za kiuchumi ?.

Tatu,Suala la kujenga miundombinu based on wanakotoka viongozi si jambo geni Afrika.Ukisoma historia ya kijiji cha Yamoussoukro alichozaliwa kiongozi wa mwanzo wa taifa la Ivory Coast Mh Felix Houphouet Boigny ambacho baadae kiligeuzwa makao makuu ya serekali badala ya Abdjan.Mh Felix Houphouet Boigny alianza na ujenzi wa kanisa kubwa dunia Basillica of our Lady of peace,ujenzi wa uwanja wa ndege wenye uwezo wa kutua ndege aina ya Concord (Afrika wakati huo vilikuwa viwili tu Gbadolite na Yamoussoukro Airport) na majengo ya kisasa kwaajili ya shughuli za kiserekali.Ukienda kule Zaire sasa Congo aliyekuwa Rais wake Marehemu Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga hakuishiwa vituko alijenga uwanja wa ndege mkubwa kuliko wowote Afrika wakati huo Gbadolite International Airport,Jumba la starehe na miundombinu ya kisasa kijiji alichozaliwa leo ni mahame kabisa hakuna kinachoendelea kwakuwa wakati wa ujenzi hawakuzingatia masuala ya uchumi,jamii,usalama na nk.

6ac1e86b-e8c1-4fca-9315-6ec69282701c-2060x1236.jpeg

9d5f02a2-ede1-4780-a3ed-4caab3e01c40-2060x1297.jpeg

Control tower ilivyosasa.

32c0ddd8-e5eb-4fa4-b6c0-3805d94c844a-2060x1236.jpeg

6d73d197-4957-470f-a8d8-759750857478-2060x1236.jpeg

c0bbd0b0-921c-429e-890d-9012e63bdd67-2060x1267.jpeg

Baadhi ya majengo yamegeuzwa madarasa.

5bc122d3-6dfb-4be9-9371-ce6cdced7cc0-2060x1297.jpeg

Hotel ya kifahari leo haina wageni hata kiduchu.

15e1b139-0e60-47ee-b399-42e6abd8eb0d-2060x1280.jpeg

Hata Mbuzi hawapatiki.

be82b6c0-d5ec-404a-89db-9ea00f76fbdf-2060x1373.jpeg

Bwawa la kuogelea lilivyo sasa.

846cec32-beba-4019-bfba-d759a5705dba-2060x1236.jpeg

a30f0956-7897-40fc-8669-34d79a0a2bda-2060x1236.jpeg

Ulevi wa madaraka ulivyoteketeza mabilioni ya fedha za walipa kodi katika uwekezaji wa kijinga.
hahaha. Chato utakuwa mkoa muda si mrefu patachangamka kupita ARUSHA.
 
Aisee kumbe rafu zilianza kitambo sana.
Kaka mtenda akitendewa huwa inauma sana- WAKASKAZINI wameumiza sana wa kanda zingine. hebu fikiri inakuwaje mradi wa kilimo cha mpunga uweke Lower Moshi kule ambapo hata wali hawajui kuupika badala ya Msoga wanakokula wali kila siku- Sababu WAKASKAZINI ndio walikuwa makatibu wakuu wa wizara, hazina nk nk- KUTESA kwa zamu
 
Raisi ana akili nyingi sana sasa kwa sababu hamjui malengo yake ku ujenga ule uwanja pale si, kwasababu ni kwake, lengo lake kubwa ni kuwabana wezi wa dhahabu yetu, ni kwamba ndege zote zinazotua migodini itakua marufuku na viwanja vyote vidogo vidogo migodini vitafugwa
Kaka hapo umezidisha chumvi; kwa taarifa yako hakuna ndege kutoka hivyo viwanja vidogo vidogo inaruhusiwa kuruka nje ya anga ya Tanzania BILA KUPITIA viwanja vikubwa
 
Ndugu yangu Eudorite,
Hivi barafu anaupigia chapuo Uwanja wa Mwanza au alichosema ni kwamba, ikiwa hapakuwa na namna ya kujenga Serengeti basi option ingekuwa ni kujenga Mwanza badala ya Chato! Sehemu ya thread yake ni hii:Ingawaje umeleta habari za ukanda; nitangulie kusema kwamba, binafsi sina maslahi yoyote ama iwe na Kanda ya Kaskazini ambayo hamuishi kuisemanga na wala kanda ya Ziwa!

But on top of that, sina hata maslahi kwenye siasa za upinzani haidhuru hata kama wengine wanaweza kuona hivyo kwavile huwa napinga mambo mengi. Hata hizo Bombadier ambazo ndugu yangu barafu anaziunga mkono; mimi nimeanza kuzipinga since Day 1 na nitaendelea kuzipinga japo kwa sasa! Na si hivyo tu, nilianza kupinga ununuzi wa ndege tangia enzi za JK!!!!

Lakini pamoja na yote hayo, barafu yupo sahihi kwa 100%.

Kama umemsoma vizuri best option kwake ni Serengeti and not Mwanza!

Lakini ikiwa hapana namna ya kujenga Uwanja wa Serengeti, basi best option kwa sasa ni Mwanza kwa sababu ndio shortest economical distance to Serengeti lakini sio Chato unless kama unataka kutuambia ni rahisi zaidi kufika Serengenti kutokea Chato kuliko kutokea Mwanza!

That's one but second, hata kama ingekuwa ni rahisi zaidi kufika Serengeti kutokea Chato kuliko Mwanza; bado hiyo peke yake haiwezi kuwa decisive criteria ya kufikia maamuzi ya kuchagua Chato badala ya Mwanza!

Moja ya mambo ambayo wachumi watahoji; is Chato economically viable compared to Mwanza? Kwamba, fine... ni rahisi Watalii kutokea Chato kuliko Mwanza... ni hilo tu?! Watalii wana msimu wake... je, wakati wa offseason uwanja utaendelea kutumika?!

Hapo nimejaribu kuupendelea Uwanja wa Chato kwamba utakuwa unahudumia watalii (you know it's impractical) lakini pamoja na yote hayo, bado tunaona hatari ya kuwa underutilized wakati wa offseason.

Ukweli huo hapo juu ndio unajibu hoja yako kwamba huoni ni kwanini Uwanja usijengwe Chato! Sababu ni moja tu, Chato hawana uchumi wa ku-utilize international airport throughout the year! As of now, Chato Airport haiwezi kuendeshwa economically... NO WAY!

I hate to say this but ukweli ni kwamba, ingawaje Chato Airport is too big even to kule kwetu Mafia; lakini ni bora Mafia ungeweza kutumika throughout the year hata kama ungetumiwa na ndege ndogo compared to Chato!!
kuna barabara inajengwa pale kutokea Chato mpaka Serengeti mwendo wa nusu saa tu
 
Sasa ni dhahiri kuwa, kuanzia mwezi Aprili katika mapumziko ya Pasaka, Mkuu wetu atakuwa na uhakika wa kwenda mapumzikoni kwa kutumia uwanja wa ndege mpya wa Chato, yaani Chato Airport.

Kwa sasa uwanja huo unaotegemewa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Aprili upo ktk kiwango cha vumbi na unaendelea kufanyiwa matengenezo hadi kiwango cha lami. Tayari ndege ndogo aina ya Beech Craft(King Air) mali ya kampuni binafsi ya TanzanAir imetua kwa mara ya kwanza ktk uwanja wa ndege wa Chato na hivyo kutoa uhakika kuwa sasa Chato inaenda kupokea ndege bila wasiwasi wowote.

Kwa mujibu wa taarifa,uwanja huo una kiwango cha "Aerodrome Reference Code 4D". Hizi "codes" hutolewa na ICAO (International Civil Aviation Organization) kulingana na ubora wa kiwanja kwa kuangalia aina ya ndege zinazoweza kutua, ukubwa wa ndege kwa maana ya uzito na upana wa mabawa.

Codes hizi zipo kuanzia 1A hadi 4F. Hivyo kwa kiwanja kuwa na Code 4D maana yake kimebakiza Code mbili tu kufikia kiwango cha mwisho cha ubora wa viwanja unaotambulika na ICAO.Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere "Code" yake ni 4E, hivyo uwanja wa Chato upo nyuma ya JNIA kwa "code letter" moja lakini upo sawa kwa "Code number" na JNIA kwa sababu vyote vipo kwenye "Code number 4".

Mfululizo wa "Aerodrome Reference Codes" huanza na 1A, 2B, 3C, 4D, 4E, 4F. Hivyo ni hakika sasa Chato Airport kwa kuwa na "Code 4D" inaenda kuwa moja kati ya viwanja vitatu venye kiwango bora Tanzania ikikaa nyuma ya Julius Nyerere na KIA. Uwanja wa Mwanza ni "Code 4D" hadi hapo ukarabati utakapokamilika utakuwa na sifa ya "Code 4E".

Hatuididimizi dhamira ya Mkuu kujenga kiwanja chenye ubora Chato, bali tunahoji kwa uelewa mdogo tu wa kanuni za Uchumi. Kwamba kiwanja hiki huko Chato kinaweza kuwa na matokeo chanya ya kiuchumi kama ambavyo wangeweza kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza?

Tunauhitaji Uwanja wa Mwanza kuliko ule wa Chato kwa sababu za kiuchumi ktk sekta ya Utalii. Tumekuwa tukilalamika sana kwa mbuga yetu ya Serengeti kukosa watalii wa kutosha kisa njia za usafiri kufika huko zilivyokuwa duni kushinda majirani zetu tunaopakana na mbuga ya Maasai Mara.

Uwanja pekee unaohudumia mbuga ya Serengeti kwa njia ya anga ni "Seronera Aistrip" ambapo huwa busy sana na huchukua ndege ndogo zenye abiria wasiozidi 50. Hii ndio moja kati ya "busiest Airstrip" kwa Tanzania.

Ili ufike Serengeti kupitia uwanja wa KIA unahitaji kutembea kilomita 284 kwa gari toka uwanjani, kwa kupitia uwanja wa ndege wa Arusha inakupasa utembee kwa gari umbali wa kama kilomita 226 wakati kwa kupitia Uwanja wa Mwanza,mtalii anatembea kilomita 166 hadi kufika geti la Ndabaka(?).

Kwa mahesabu hayo,kama ujenzi wa Uwanja wa ndege Serengeti ulishindikana,basi Uwanja wa ndege wa Mwanza ndio suluhisho la haraka ktk kuwafikisha watalii kwa urahisi ktk mbuga hiyo.Tukiusahau uwanja huo na kutazama zaidi ule wa Chato, tunaweza kuhoji dhamira hii ya maendeleo ktk kufika uchumi wa kati. Na kuhoji kwetu kusiababishe "hasira" kwa wenye mamlaka, bali ichukuliwe ni kama changamoto za raia kwa serikali yao.

Ukisefu wa usafiri wa uhakika na hasa ule wa njia ya anga, ndio unatukosesha mapato na kupunguza idadi wa Watalii ktk mbuga yetu ya Serengeti na hivyo wengi kuishia Maasai Mara.

Licha ya kuwa Serengeti ina ukubwa mara sita ya Maasai Mara,lakini bado "Vitanda" vya kupokea watalii katika hotel za Serengeti hivizidi 970 wakati wenzetu Maasai Mara ktk mbuga yao, kuna "Vitanda" zaidi ya 4,700. Hakika kupanga ni kuchagua.

Mpaka sasa Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania inamiliki viwanja vya ndege 58(ukijumlisha na Chato itakuwa 59),na wakati Uwanja wa ndege wa KIA ukiwa mikononi mwa Kampuni ya KADCO. TANAPA inamiliki karibu viwanja 26(Vingi vikiwa ni Airstrips),NCAA 2 na viwanja binafsi 93.

Katika hivi vya binafsi,vingi vinamilikiwa na wawekezaji toka nje ambao huvitumia kufanya udanganyifu ktk maliasili zetu.Uwanja wa ndege wa mgodi wa Geita(Mchauru) na Uwanja wa ndege wa Tishwa(HTSW) kule Loliondo unaomilikiwa na mtoto wa mfalme wa UAE ni moja kati ya viwanja vinavyopswa kutazamwa vizuri na serikali hii.

Uwanja huu wa Tishwa Loliondo ndio "unatisha", kwani huku ndege za familia ya mfalme hushuka moja kwa moja na kunyanyuka na mali nyingi. Umejengwa kiasi cha kuweza kutua na kuruka ndege kubwa.

Huu ndio uwanja ulio ktk eneo ambapo ukifika na kuwasha simu unakutana na meseji inasema "Dear Guest,Welcome to the UAE.Enjoy the best network coverage and other unmatched services only with Etisalat.Please use <+> or <00> before the country code for international calls.For directory services call 181,for availability of GPRS,MMS 3G roaming services call Etisalat Travellers help line 8002300 & for inquiries on Tourism,entertainment,shopping,etc call 7000-1-7000(Roaming rates apply).Have a pleasant stay in the UAE"

Labda wengine hatuna utaalamu wa Telecomunication, lkn kweli inawezakana hii kitu iingie tu kwenye simu yako wakati hujafanya "roaming". Haya ndio mambo ya TCRA kututoa tongotongo, sio zile mambo zao za .co.tz

Tunatakiwa tuwekeze ktk usafiri wa anga,lakini tuwekeza kimkakati na kwa faida za uchumi wa pamoja kama Taifa.Tukipewa sababu za kiuchumi zinazoupeleka uwanja wa ndege Chato wenye "Aerodrome Reference Code 4D" hatutakuwa na maswali.Tusipapata majibu yenye faida za kiuchumi,tutaendelea kuhoji hata tukiwa mafichoni.

Tukumbusha umuhimu wa Mwanza ktk kuihudumia Serengeti National Park, tutawakumbusha kuwa mlikuwa na mradi wa kujenge Uwanja wa ndege Serengeti,ila mkapambana na wanaharakati wa Ikolojia. Uwanja wa Serengeti ulipaswa kujengwa kati wa Kiwanja cha Ndege pale Mgumu.

Serengeti International Airport ilikuwa ni Code 4F, ilipaswa kuwa na runway ya mita 3,800 hadi mita 4,200.Mradi huo ulififia,sasa "tumefufukia" Chato na Uwanja wa "Code 4D".Je huku ndio kupanga na kuchagua??

Wakuu ukiyatafakari sana mambo ya nchi hii unaweza kuwa kichaa. Tuishukuru [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG], inatupa wasaa wa kuhoji haya nyuma ya "keyboard". Mambo haya enzi za Waziri wa Maliasili Aboubakari Mgumia yaliondoa maisha ya Ndugu Stan Katabaro. Tunapouanza mwaka mpya, tuzame katika sala na maombi. Ili wale wanaoomba tuwaombee kila siku,tusiwaombee tu wawe na afya njema..Bali walegeze mioyo ktk kuishughulikia mitandao kama mtandao wetu pendwa wa [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG].

Nawatakia Mwaka Mpya mwema. Ninafunga mwaka na "Chato Interantional Airport".... Panapo majaliwa hapo mwakani. Nitakuwa likizo huko kwetu porini.... Ciaoooo!!!!
Mkuu hongera. Toka uzungumze stories za mbuzi kula almasi na mikiki mikiki yake. Nakuambia ukweli hata wale makomando wa Uhuru niliona wanadanganya kuwa ni makomando zaidi yako. [HASHTAG]#jamii[/HASHTAG] forum# happy new year
 
OTE="Brigedia Chan-ocha, post: 19084321, member: 213307"]Mkuu Barafu baada ya kuleta ile habari ya kwanza ya Uwanja wa NDEGE WA CHATO niliona nifuatilie sababu za Ujenzi wa huo Uwanja na umuhimu wake...

Findings....

Nimeelezwa kuwa, Rais Magufuli amejenga Uwanja huo CHATO ili aweze kuziteka nchi za RWANDA, BURUNDI, na UGANDA, Kwamba, Ndege za kutoka mataifa hayo zitatua CHATO INT. AIRPORT, halafu abiria watapanda Gari zao kutoka CHATO hadi MWANZA ambapo watapanda tena NDEGE kwenda wanapopataka ndani au nje ya nchi, (SIJUI NI AKILI GANI ILIYOTUMIKA HAPA) nimeelezwa kwamba, Rais Magufuli anataka kujenga DARAJA La BUSISI ili kurahisisha usafiri huo wa wageni kuja Mwanza kutoka CHATO INT. AIR.

Nimeelezwa kuwa, Mpango wa Magufuli ni Kuutenganisha mkoa wa GEITA Na CHATO hapo baadae, hivyo anaandaa mazingira ya kushawishi ugawaji wa MIKOA Hiyo, na makao makuu ya mkoa wa CHATO yatakuwa eneo moja linaitwa RUSUNGU hivi kama sijakosea jina, nakubali nirekebishwe maana nimesahau jina lake kwa usahihi.

Nimeelezwa kwamba, Eti CHATO kuna Mbuga ya WANYAMA binafsi ya RAIS Magufuli ila sijawa na uhakika na hili...

Kwa kifupi, hata kama Chato walikuwa na uhitaji wa uwanja wa ndege siyo sasahivi jamani, wewe fikiria, Plan zipo kwenye vitabu miaka mingi juu ya ujenzi wa viwanja kama MWANZA, MUSOMA Nk. lakini hadi sasa hakuna kilichofanyika kwenye viwanja hivyo, ila hiki cha chato ndo kiwe Urgent?[/QUOTE]
Kwanini kisinge jengwa Bukoba!!??
 
Unafiki nao ni approach ya ushindi kama si usalama.

Ningefurahi kama uwanja ungejengwa Geita ili kurahisisha mawasiliano ya kiuchumi katika kanda ile ukizingatia wingi wa heka heka za wafanyabiashara wa madini katiak eneo lile.

Ninaomba iwe kaam ilivyo siku zote isije kesho tukaanza kuulizana mchawi wa raslimali za umma na matumizi mabaya ya madaraka.
Geita unaijua? wapi utajenga uwanja wakati imezungukwa na milima, halafu watu walivyosongamana utamhamisha nani na umpeleke wapi? Mbona hamuulizi uwanja wa shinyanga uko ibadakuli km 50 kutoka shinyanga mjini.
 
Kwahiyo rasilimali fedha sio tatizo hivyo tujenge tu viwanja vya ndege kila mahali au unamaanisha nini?
Soma tena. Nimeandika kama kutakuwa na umuhimu wa kufanya hivyo.

Tunapinga ujenzi wa uwanja wa chato pasipo kutoa sababu za maana ndiyo sababu kuna ubishani hapa.

Sababu za idadi ya watu na za kiuchumi zina walakini kwani watakaotumia uwanja huo su wakazi w chato pekee.

Mchumi makini lazima aangalie na shughuli za kiuchumi zilizopo jirani na uwanja huo. Kwa sasa na baadae. Hapo ndipo tunapaswa kujadili.
 
Kuna kaharufu kaubinafsi hapa,watanzania tusipokuwa macho kwa mara ya kwanza tunakwenda kumuzalisha Mugabe wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom