Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,819
Sasa ni dhahiri kuwa, kuanzia mwezi Aprili katika mapumziko ya Pasaka, Mkuu wetu atakuwa na uhakika wa kwenda mapumzikoni kwa kutumia uwanja wa ndege mpya wa Chato, yaani Chato Airport.

Kwa sasa uwanja huo unaotegemewa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Aprili upo ktk kiwango cha vumbi na unaendelea kufanyiwa matengenezo hadi kiwango cha lami. Tayari ndege ndogo aina ya Beech Craft(King Air) mali ya kampuni binafsi ya TanzanAir imetua kwa mara ya kwanza ktk uwanja wa ndege wa Chato na hivyo kutoa uhakika kuwa sasa Chato inaenda kupokea ndege bila wasiwasi wowote.

Kwa mujibu wa taarifa,uwanja huo una kiwango cha "Aerodrome Reference Code 4D". Hizi "codes" hutolewa na ICAO (International Civil Aviation Organization) kulingana na ubora wa kiwanja kwa kuangalia aina ya ndege zinazoweza kutua, ukubwa wa ndege kwa maana ya uzito na upana wa mabawa.

Codes hizi zipo kuanzia 1A hadi 4F. Hivyo kwa kiwanja kuwa na Code 4D maana yake kimebakiza Code mbili tu kufikia kiwango cha mwisho cha ubora wa viwanja unaotambulika na ICAO.Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere "Code" yake ni 4E, hivyo uwanja wa Chato upo nyuma ya JNIA kwa "code letter" moja lakini upo sawa kwa "Code number" na JNIA kwa sababu vyote vipo kwenye "Code number 4".

Mfululizo wa "Aerodrome Reference Codes" huanza na 1A, 2B, 3C, 4D, 4E, 4F. Hivyo ni hakika sasa Chato Airport kwa kuwa na "Code 4D" inaenda kuwa moja kati ya viwanja vitatu venye kiwango bora Tanzania ikikaa nyuma ya Julius Nyerere na KIA. Uwanja wa Mwanza ni "Code 4D" hadi hapo ukarabati utakapokamilika utakuwa na sifa ya "Code 4E".

Hatuididimizi dhamira ya Mkuu kujenga kiwanja chenye ubora Chato, bali tunahoji kwa uelewa mdogo tu wa kanuni za Uchumi. Kwamba kiwanja hiki huko Chato kinaweza kuwa na matokeo chanya ya kiuchumi kama ambavyo wangeweza kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza?

Tunauhitaji Uwanja wa Mwanza kuliko ule wa Chato kwa sababu za kiuchumi ktk sekta ya Utalii. Tumekuwa tukilalamika sana kwa mbuga yetu ya Serengeti kukosa watalii wa kutosha kisa njia za usafiri kufika huko zilivyokuwa duni kushinda majirani zetu tunaopakana na mbuga ya Maasai Mara.

Uwanja pekee unaohudumia mbuga ya Serengeti kwa njia ya anga ni "Seronera Aistrip" ambapo huwa busy sana na huchukua ndege ndogo zenye abiria wasiozidi 50. Hii ndio moja kati ya "busiest Airstrip" kwa Tanzania.

Ili ufike Serengeti kupitia uwanja wa KIA unahitaji kutembea kilomita 284 kwa gari toka uwanjani, kwa kupitia uwanja wa ndege wa Arusha inakupasa utembee kwa gari umbali wa kama kilomita 226 wakati kwa kupitia Uwanja wa Mwanza,mtalii anatembea kilomita 166 hadi kufika geti la Ndabaka(?).

Kwa mahesabu hayo,kama ujenzi wa Uwanja wa ndege Serengeti ulishindikana,basi Uwanja wa ndege wa Mwanza ndio suluhisho la haraka ktk kuwafikisha watalii kwa urahisi ktk mbuga hiyo.Tukiusahau uwanja huo na kutazama zaidi ule wa Chato, tunaweza kuhoji dhamira hii ya maendeleo ktk kufika uchumi wa kati. Na kuhoji kwetu kusiababishe "hasira" kwa wenye mamlaka, bali ichukuliwe ni kama changamoto za raia kwa serikali yao.

Ukisefu wa usafiri wa uhakika na hasa ule wa njia ya anga, ndio unatukosesha mapato na kupunguza idadi wa Watalii ktk mbuga yetu ya Serengeti na hivyo wengi kuishia Maasai Mara.

Licha ya kuwa Serengeti ina ukubwa mara sita ya Maasai Mara,lakini bado "Vitanda" vya kupokea watalii katika hotel za Serengeti hivizidi 970 wakati wenzetu Maasai Mara ktk mbuga yao, kuna "Vitanda" zaidi ya 4,700. Hakika kupanga ni kuchagua.

Mpaka sasa Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania inamiliki viwanja vya ndege 58(ukijumlisha na Chato itakuwa 59),na wakati Uwanja wa ndege wa KIA ukiwa mikononi mwa Kampuni ya KADCO. TANAPA inamiliki karibu viwanja 26(Vingi vikiwa ni Airstrips),NCAA 2 na viwanja binafsi 93.

Katika hivi vya binafsi,vingi vinamilikiwa na wawekezaji toka nje ambao huvitumia kufanya udanganyifu ktk maliasili zetu.Uwanja wa ndege wa mgodi wa Geita(Mchauru) na Uwanja wa ndege wa Tishwa(HTSW) kule Loliondo unaomilikiwa na mtoto wa mfalme wa UAE ni moja kati ya viwanja vinavyopswa kutazamwa vizuri na serikali hii.

Uwanja huu wa Tishwa Loliondo ndio "unatisha", kwani huku ndege za familia ya mfalme hushuka moja kwa moja na kunyanyuka na mali nyingi. Umejengwa kiasi cha kuweza kutua na kuruka ndege kubwa.

Huu ndio uwanja ulio ktk eneo ambapo ukifika na kuwasha simu unakutana na meseji inasema "Dear Guest,Welcome to the UAE.Enjoy the best network coverage and other unmatched services only with Etisalat.Please use <+> or <00> before the country code for international calls.For directory services call 181,for availability of GPRS,MMS 3G roaming services call Etisalat Travellers help line 8002300 & for inquiries on Tourism,entertainment,shopping,etc call 7000-1-7000(Roaming rates apply).Have a pleasant stay in the UAE"

Labda wengine hatuna utaalamu wa Telecomunication, lkn kweli inawezakana hii kitu iingie tu kwenye simu yako wakati hujafanya "roaming". Haya ndio mambo ya TCRA kututoa tongotongo, sio zile mambo zao za .co.tz

Tunatakiwa tuwekeze ktk usafiri wa anga,lakini tuwekeza kimkakati na kwa faida za uchumi wa pamoja kama Taifa.Tukipewa sababu za kiuchumi zinazoupeleka uwanja wa ndege Chato wenye "Aerodrome Reference Code 4D" hatutakuwa na maswali.Tusipapata majibu yenye faida za kiuchumi,tutaendelea kuhoji hata tukiwa mafichoni.

Tukumbusha umuhimu wa Mwanza ktk kuihudumia Serengeti National Park, tutawakumbusha kuwa mlikuwa na mradi wa kujenge Uwanja wa ndege Serengeti,ila mkapambana na wanaharakati wa Ikolojia. Uwanja wa Serengeti ulipaswa kujengwa kati wa Kiwanja cha Ndege pale Mgumu.

Serengeti International Airport ilikuwa ni Code 4F, ilipaswa kuwa na runway ya mita 3,800 hadi mita 4,200.Mradi huo ulififia,sasa "tumefufukia" Chato na Uwanja wa "Code 4D".Je huku ndio kupanga na kuchagua??

Wakuu ukiyatafakari sana mambo ya nchi hii unaweza kuwa kichaa. Tuishukuru [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG], inatupa wasaa wa kuhoji haya nyuma ya "keyboard". Mambo haya enzi za Waziri wa Maliasili Aboubakari Mgumia yaliondoa maisha ya Ndugu Stan Katabaro. Tunapouanza mwaka mpya, tuzame katika sala na maombi. Ili wale wanaoomba tuwaombee kila siku,tusiwaombee tu wawe na afya njema..Bali walegeze mioyo ktk kuishughulikia mitandao kama mtandao wetu pendwa wa [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG].

Nawatakia Mwaka Mpya mwema. Ninafunga mwaka na "Chato Interantional Airport".... Panapo majaliwa hapo mwakani. Nitakuwa likizo huko kwetu porini.... Ciaoooo!!!!
 
Mkuu barafu you are speaking in tongues(aviation jargon) ila nimekuelewa as far as economics is concerned, siku hizi sisikii bwana yule akiomba aombewe, kashaonja vitamu...

Give them an inch they take a yard, give them a yard they take a mile... Tukiongea sana watamrudisha mkuu Melo Keko!!
 
Mnaweza kuweka uchambuzi mzuri sana ila ukakosa mashiko kwa kuwa tu una lengo la kiitikadi zaidi.

Mimi huwa najiuliza, je suppose tungechagua huko, kwa bahati mbaya sana umeshindwa kujiendesha wenyewe mkaamua kuturudishia walewale waliokimbia huku baada ya kukatwa je mngeweza kutujengea nchi kweli?, au mngeishia kuandika uchambuzi kama huu wakati mkishuhudia barabara ya Chalinze-Moshi ikiwekwa 4 ways, na kiwanja kama hicho cha chato kikijengwa Hai au Monduli?

Maana wenzetu wa upinzani mmekuwa mabingwa ya kuchambua msivyoviweza, mmekuwa wazuri theoretically but you are not practically oriented, mambo yenu mengi yanakwenda kinyume lakini kwa vile kafanya yule, basi you keep quite kama vile hamuoni huku ukisubiri uongee likifanyika upande wa pili.

Kaskazini ilijengeka mapema kwavile watu wa kaskazini walipata fursa, wakakumbuka kwao ili wapate kwenda mapumzikoni kila mwaka, sasa acha fursa zinapopatikana sehemu zingine basi wazitumie fursa hizo, huku mkiwa wavumilivu mkisubiri 2020 ,
 
Kipigi,

Wengine hatuongozwi na itikadi yoyote,ndio maana tunasifia na kutoa changamoto kwa nia njema.

Tulishangilia ujio wa Pangoboi katikati ya matusi na kashfa tele...Wakati huo hukutuona kama "wa kaskazini"!!Sasa tunahoji kwa staha na kwa nia njema unaamua kutupakazia "ukanda"

Mbona wengine hatutoki huko ulikokutaja?Hivi nani wa kuwekewa mshangao?Wewe unayeandika lugha ya kibaguzi au sisi tunaotoa changamoto?

Jenga hoja bila hisia za ukabila na ukada...Wengine hizo hatua tulishazipita!!Ndio maana tunapongeza na kukosoa kwa staha na nidhamu... Jifungue ktk minyororo ya ukada na ukanda, Utakuwa huru kiakili na kifikra
 
Mkuu barafu. Nikushukuru kwa kuanzisha mada.

Hilo la uwanja kujengwa chato binafsi sioni kwanini usijengwe huko. Labda kama ungeonyesha ni kwanini chato panastahili uwanja mdogo kuliko unaojengwa kuliko sababu ulizotoa.

Hoja yangu inahusu kuboresha uwanja wa Mwanza kuhudumia mbuga ya Serengeti.

Ki mantiki. Sehemu kubwa ya mbuga ya serengeti ipo mkoani mara na si zaidi ya kilometa 110 kwa barabara kutoka makao makuu ya mkoa hadi kuingia mbugani kwa kupitia barabara ya Musoma - Arusha na haifiki kilometa 70 kwa kupitia barabara ya Musoma - Mwanza. Mbuga hii ipo kwenye wilaya za Serengeti Tarime na Bunda. Ambapo Wilaya ya Serengeti inamiliki eneo kubwa zaidi.

Sehemu ndogoya mbuga hii iliyobaki ipo mkoani SIMIYU katika wilaya za Itilima na Bariadi. Mkoa wa mwanza ulikoma kumiliki mbuga hii baada ya kuanzishwa mkoa wa simiyu.

Mipango ya kujenga kiwanja cha ndege kuhudumia mbuga ya serengeti ni ya muda mrefu ambapo awali ilikuwa uwanja mkubwa wa kisasa ujengwe Musoma au Bunda ili kuhudumia mbuga hii. Na uwanja mdogo wa Mugumu uboreshwe. Eneo la uwanja lilibainishwa na juzi kati enzi za Utawala wa Kikwete lilipimwa upya. Mpango huu uliambatana na kuboresha air strip ya mugumu iwe na viwango vya sasa vya uwanja kama wa Arusha na pia kujenga barabara kutoka Musoma hadi Arusha.

Utekelezaji wake unapigwa figisu hadi leo ambapo hakuna kiwanja. Air strip wala barabara iliyojengwa. Sababu mojawapo ni hoja zilizotolewa na wana kaskazini kwamba bora kuijenga KIA ili ihudumie mbuga zote zilizoko kaskazini mwa nchi.

Uwanja wa KIA UKAJENGWA. Na tagu wakati huo mbuga ya serengeti ikajulikana kwamba ipo arusha kama ambavyo tunaambiwa mlima kilimanjaro upo nchini Kenya. Mkoa wa mara ukakosa mapato ya utalii kwa maana ya viingilio vya wageni mbugani na uwekezaji wa miundombinu kama taasisi za utalii mfano hoteli, vyuo majengi ya taasisi za umma nk. na miundombinu hii kwa wingi imeendelea kujengwa Arusha tangu wakati huo,na kuhalalisha mkoa wa arusha kumiliki mbuga ya Serengeti.

Awamu ya pili ya kujenga uwanja mkoani mara ni huo uwanja wa Serengeti ulioutaja kwenye andiko lako.

Hii ilikuwa zaidi inachochewa na maombi kutika kwa mwekezaji aliyewekeza pale Gurumeti.

Kama ulivyogusia. Uwanja huu pia haukujengwa kutokana na figisu za wanaharakati wa ndani na nje ya nchi. Ambapo jamaa zetu wa kaskazini waliungana na Wakanya kukwamisha ujenzi.

Hivyo badala ya kupugia debe uwanja wa Mwanza kuhudumia serengeti ungesema ukweli kwamba uwanja wa kuihudumia mbuga hii ujengwe ndani au karibu na mbuga hii. Nani ya mkoa wa mara au wa sumiyu.

Lengo hapa ni kuonyesha uhalisia. Sote tunakubali uwanja wa ndege wa mwanza unahitajika na ulitakiwa uwepo kabla ya ule wa KIA.

Suala la kuhudumia mbuga ya serengeti ama kutokea KIA au uwanja wa ndege wa Mwanza hakuta tofauti kubwa maana bado usafiri wa magari wenye kuchukua muda mrefu njiani utatumika.

Tuseme tu kwamba lazima kuwe na uwanja wa ndege wa kisasa unaokidhi mahitaji ya sasa na baadae NDANI YA MKOA WA MARA au MKOA WA SIMIYU ili kuihudumia hii mbuga.

Wenzetu wa-kenya wanajenga viwanja vya ndege vikubwa vilivyi katika umbali usiokuwa mkubwa ilimradi kuna sababu. Mfano angalia umbali wa viwanja vya Nairobi Kia na Taveta. Pia Nairobi Nakuuru Masai Mara na Kisumu. Au hapa Tanzania kuna Kia Arusha na Moshi.

Basi ni halali kujenga na kuboresha viwanja vya Mwanza Kigoma Simiyu Tabora Singida Shinyanga Chato Bukoba na MUSOMA kwa ukubwa tofauti kulingana na vigezo vya kiuchumi kijamii na kijiografia.

Msisitizo ni kwamba mbuga ya serengeti italeta faida kwa taifa hili kama serikali watanzania wote na wakazi wa mikoa ya Mara na Simiyu wataona umuhimu wa kuwekeza kwenye miundombinu ya kuihudumia mbuga hiyo. Kama maji barabara hoteli uwanja wa ndege nk. ndani ya mikoa husika.
 
Kipigi,

Naungana na wewe.

Pist yake kwangu imekosa mantiki pale aliposema uwanja wa chato usijengwe ili kuboresha wa mwanza wakati anatambua kwamba

1. Maboresho ya uwanja wa mwanza yanaendelea hadi sasa na ujenzi wa uwanja wa chato hauja athiri maboresho ya uwanja wa mwanza.

2. Kuna uhitaji wa kujenga uwanja wa ndege kuhudumia mbuga ya serengeti. Badala ya kupiga debe uwanja huo ujengwe ndani au karibu na mbuga hiyo anashadadia uwanja wa mwanza ndio uhudumie serengeti ilhali upo miles away.

Ni seme tu kwamba badala ya kulalamikia uwanja kujengwa chato. Tusifie na kudai ujenzi na uboreshaji wa viwanja vingine vingi tu vinavyohitajika kote nchini kulingana mahitaji ya sasa na ya baadae.

Lengo isiwe kukataa maendeleo yasiwepo eneo flani bali yapelekwe kwa wakati kulingana na mahitaji na faida zitakazopatijana.
 
Chato

Chato town, population = 17,508. Chato district population = 365,000

Economic activitiy = nothing significant apart from subsistence farming which depend on rain. Contributes less than 1 percent to the GDP.
Tourist attractions = none

At the same time Songwe airport, the main airport serving the southern highlands, an area with more than 5 mil people and also being the bread basket of Tanzania doesn't have runway lights till today!

Mwanza airport yenyewe upanuzi wake has been going on at such a slow pace for the past 2 years and at times even stalled!

We are willing to spend billions on someone's vanity project ambayo will generate nothing in return and adds little value, lakini tunaache sehemu where the money would have been better spent.

A small airport would have been fine, lakini sio kujenga an airport with a runway that could almost "rival" JNIA, at a town/district with a population lower than some suburbs in Dar.

Someone needs to look at themself in the mirror and reevaluate the choices they have been making so far.
 
Mkuu barafu. Nikushukuru kwa kuanzisha mada.

Hilo la uwanja kujengwa chato binafsi sioni kwanini usijengwe huko. Kabda kama tungeshauri ujengwe uwanja mdogo ambapo ndege kubwa zisingetua.

Hoja yangu inahusu kuboresha uwanja wa Mwanza kuhudumia mbuga ya Serengeti.

Ki mantiki. Sehemu kubwa ya mbuga ya serengeti ipo mkoani mara na si zaidi ya kilometa 110 kwa barabara kutoka makao makuu ya mkoa hadi kuingia mbugani kwa kupitia barabara ya Musoma - Arusha na haifiki kilometa 70 kwa kupitia barabara ya Musoma - Mwanza. Mbuga hii ipo kwenye wilaya za Serengeti Tarime na Bunda. Ambapo Wilaya ya Serengeti inamiliki eneo kubwa zaidi.

Mipango ya kujenga kiwanja cha ndege kuhudumia mbuga ya serengeti ni ya muda mrefu ambapo awali ilikuwa uwanja mkubwa wa kisasa ujengwe Musoma au Bunda ili kuhudumia mbuga hii. Na uwanja mdogo wa Mugumu uboreshwe. Eneo la uwanja lilibainishwa na juzi kati enzi za Utawala wa Kikwete lilipimwa upya. Mpango huu uliambatana na kuboresha air strip ya musoma iwe na viwango vya sasa vya uwanja kama wa Arusha na pia kujenga barabara kutoka Musoma hadi Arusha.

Utekelezaji waje unapigwa figisu hadi leo ambapo hakina kiwanja. Air strip wala barabara iliyojengwa. Sababu mojawapo ni hoja zilizotolewa na wana kaskazini kwamba bora kuijenga KIA ili ihudumie mbuga zote zilizoko kaskazini mwa nchi.

KIA IKAJENGWA. Na tagu wakati huo mbuga ya serengeti ijajulikana kwamba ipo arusha kama ambavyo tunaambiwa mlima kilimanjaro upo Kenya. Mkoa wa mara ukakosa mapato ya utalii kwa maana ya viingilio vya wageni mbugani na uwekezaji wa miundombinu kama taasisi za utalii kama vilehotelu vyuo majengi ya taasisi za umma nk na miundombinu hii kwa wingi imejengwa Arusha. Kuhalalisha mkoa wa arusha kumiliki mbuga ya Serengeti.

Awamu ya pili ya kujenga uwanja mkoani mara ni huo uwanja wa Serengeti ulioutaja kwenye andiko lako.

Hii ilikuwa zaidi inachochewa na maombi kutika kwa mwekezaji aliyewekeza pale Gurumeti.

Kama ulivyogusia. Uwanja huu haukujengwa kutokana na figisu za wanaharakati wa ndani na nje ya nchi. Jamaa zetu wa kaskazini waliungana na Wakanya kukwamisha ujenzi.

Lengo hapa ni kuonyesha uhalisia. Sote tunakubali uwanja wa ndege wa mwanza unahitajika na ulitakiwa uwepo kabla ya ule wa KIA.

Suala la kuhudumia mbuga ya serengeti ama kutokea KIA au uwanja wa ndege wa Mwanza hakuta tofauti kubwa maana bado usafiri wa magari wenye kuchukua muda mrefu njiani utatumika.

Suluhisho ni kuwa wakweli na badala ya kupigia debe serengeti kuhudumia kwa ndege zinazotua mwanza. Tuseme tu kwamba lazima kuwe na ueanja wa ndege wa kusasa unaokidhi mahitaji ya sasa na baadae NDANI YA MKOA WA MARA ili kuihudumia hii mbuga.

Mbona wakenya wanajenga viwanja vya ndege vikubwa vilivyi katika umbali usiokuwa mkubwa ilimradi kuna sababu. Mfano angalia umbali wa viwanja vya Nairobi Kia na Taveta. Pia Nairobi Nakuuru Masai Mara na Kisumu. Au hapa Tanzania kuna Kia Arusha na Moshi.

Basi ni halali kujenga na kubiresha viwanja vya Mwanza Kigoma Tabora Singida Shinyanga Chato Bukoba na MUSOMA kwa ukubwa tofauti kulingana na vigezo vya kiuchumi kijamii na kijiografia.

Msisitizo ni kwamba mbuga ya serengeti italeta faida kwa taifa hili kama serikali watanzania wote na wakazi wa mkoa wa mara wataona umuhimu wa kuwekeza kwenye miundombinu ya kuihudumia mbuga hiyo. Kama maji baranbata htele ueanja wa ndege nk. ndani ya mkoa hisika.
Bravo Mkuu,
Umeandika kitu ambacho ni mwiba kwa watu wengi, haswa hao jamaa wa Kaskazini.
Umeeleza ukweli wa figisu zinazopigwa kukandamiza Maendeleo katika maeneo husika kwa sababu za kibinafsi.
Nakupongeza kwa kuwa umeweza kuweka hili bandiko lako kiwepesi hata mama ntilie na dereva bodaboda anaweza kulielewa.

Kila mara huwa nawakumbusha jamaa zangu, kuna tofauti kati ya SIASA ZA KIHARAKATI na SIASA ZA KIZALENDO. Siasa za KIHARAKATI ni hatari sana katika Maendeleo ya Taifa Letu.
Kuna jamii/kanda Fulani wanafikiri wao wako entitled na kila kitu bora kuliko Jamii nyingine na Tanzania kwa Ujumla. Time has changed....let's dance with the tune.
Ciao.....
 
Back
Top Bottom