Tetesi: Hatimaye "Chato International Airport" kuzinduliwa rasmi mwezi Aprili

Mnaweza kuweka uchambuzi mzuri sana ila ukakosa mashiko kwa kuwa tu una lengo la kiitikadi zaidi.

Mimi huwa najiuliza, je suppose tungechagua huko, kwa bahati mbaya sana umeshindwa kujiendesha wenyewe mkaamua kuturudishia walewale waliokimbia huku baada ya kukatwa je mngeweza kutujengea nchi kweli?, au mngeishia kuandika uchambuzi kama huu wakati mkishuhudia barabara ya Chalinze-Moshi ikiwekwa 4 ways, na kiwanja kama hicho cha chato kikijengwa Hai au Monduli?

Maana wenzetu wa upinzani mmekuwa mabingwa ya kuchambua msivyoviweza, mmekuwa wazuri theoretically but you are not practically oriented, mambo yenu mengi yanakwenda kinyume lakini kwa vile kafanya yule, basi you keep quite kama vile hamuoni huku ukisubiri uongee likifanyika upande wa pili.

Kaskazini ilijengeka mapema kwavile watu wa kaskazini walipata fursa, wakakumbuka kwao ili wapate kwenda mapumzikoni kila mwaka, sasa acha fursa zinapopatikana sehemu zingine basi wazitumie fursa hizo, huku mkiwa wavumilivu mkisubiri 2020 ,
I see.

No wonder w're doomed.
 
Ndo maana serkali inapiga vita sana mtandao wa JF kwani wa najua kuna ni darasa la mapinduzi katika nyanja zote kiuchuni, siasa, elimu na kijamii pia, live long maxence
 
Mkuu barafu, iwapo serikali ingechukua hata nukta ya ushauri wako basi isingejuta kufanya hyo.

Mwanza is a Central of East African country! Kutoka Mwanza kufika Serengeti ni masaa yasiyozidi 2, hvyo kuwa na International airport mwanza hakika uchumi wa mwanza na nchi ungepaa Sana...maana wageni wengi wangetua na kwenda Masai zaidi kuliko hivi sasa sisi ndio vinara wa kwenda kupokea kwenye border ya isbania!!!
 
Heshima kwako barafu, andiko hili linafikilisha sana.

Najiuliza kwanini ile hotel ya mkulu aliyepita anayozushiwa pale Rock city tusingeijenga pale Serengeti national park!

Ubinafsi na akili za umimi zinatuponza sana na kutufanya tuendelee kuwepo hapa tulipo
 
nina umri wa miaka 73, nimetokea kwenye familia yenye watoto wengi sana , ila cha kuskitisha katika familia yetu ama ukoo wetu kwa ujumla hakuna hata 1 aliyewah kupanda ndege
 
barafu,

Hongera kwa mada yako.lakini usiwaaminishe watanzania kupitia mtandao na hizo code zinazoonesha level za viwanda vya ndege kuwa sasa kiwanja cha Chato kitakuwa na ubora baada ya kiwanja cha ndege cha Dar na Kilimanjaro.

Pamoja Maelezo mengi ambayo ni hisia hasi kwa utawala wa Rais Magufuli kuhusu huo uwanja wa chato huo uwanja ni muhimu tu kwa matumizi ya Rais akiwa ziara mkoani kwake na hata akiwa mapumziko ni nyumbani kwake. Hilo halina mjadala ndiyo maisha yanavyotakuwa kuwa.

Program ya viwanja vya ndege vingine nchi mzima IPO ktk bajeti ya Wizara ya Ujenzi ktk hatua mbalimbali za utekelezaji. Mfano Dodoma kimeboreshwa sasa na ndege kubwa zinatua sasa,Katavi uwanja ni mzuri sana umejengwa n.k

Naona macho na masikio yote umeyatoa kiwanja cha chato mkoa wa Geita ndiyo kinajengwa hivyo.
Mkuu baada ya miezi mitatu haiwezi kuwa nyuma ya Dsm na KIA...Lkn kwa mpangi wa muda mrefu,bila shaka utakubaliana na mimi itakuwa nyuma ya hivyo viwanja wakiwa sambamba na ule wa Mwanza.Sina nia ya kumpotosha mtu
 
barafu,

International airport inajengwa miezi mitatu hiyo sio kweli.Tusubr tàarifa rasmi
Huwezi kuwa na International Airport kwa miezi mitatu,lkn ni kweli kuwa "phase" mojawapo ya hatua ya kuwa na uwanja wa aina hiyo unaweza kukamilika kwa miezi hiyo.

Kumbuka hatua za mwanzo za Uwanja huu umeanza toka mwezi September...Hivyo hadi April itakuwa ni miezi karibu 07.

Mkuu Ngapulila kumi huanza na moja,na kuuzindua sio kuwa ndio utakuwa umekamilika..Hatua nyingine za kuuboresha zitaendelea.Asante
 
Sasa ni dhahiri kuwa, kuanzia mwezi Aprili katika mapumziko ya Pasaka, Mkuu wetu atakuwa na uhakika wa kwenda mapumzikoni kwa kutumia uwanja wa ndege mpya wa Chato, yaani Chato Airport.

Kwa sasa uwanja huo unaotegemewa kukamilika mwanzoni mwa mwezi Aprili upo ktk kiwango cha vumbi na unaendelea kufanyiwa matengenezo hadi kiwango cha lami. Tayari ndege ndogo aina ya Beech Craft(King Air) mali ya kampuni binafsi ya TanzanAir imetua kwa mara ya kwanza ktk uwanja wa ndege wa Chato na hivyo kutoa uhakika kuwa sasa Chato inaenda kupokea ndege bila wasiwasi wowote.

Kwa mujibu wa taarifa,uwanja huo una kiwango cha "Aerodrome Reference Code 4D". Hizi "codes" hutolewa na ICAO (International Civil Aviation Organization) kulingana na ubora wa kiwanja kwa kuangalia aina ya ndege zinazoweza kutua, ukubwa wa ndege kwa maana ya uzito na upana wa mabawa.

Codes hizi zipo kuanzia 1A hadi 4F. Hivyo kwa kiwanja kuwa na Code 4D maana yake kimebakiza Code mbili tu kufikia kiwango cha mwisho cha ubora wa viwanja unaotambulika na ICAO.Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere "Code" yake ni 4E, hivyo uwanja wa Chato upo nyuma ya JNIA kwa "code letter" moja lakini upo sawa kwa "Code number" na JNIA kwa sababu vyote vipo kwenye "Code number 4".

Mfululizo wa "Aerodrome Reference Codes" huanza na 1A, 2B, 3C, 4D, 4E, 4F. Hivyo ni hakika sasa Chato Airport kwa kuwa na "Code 4D" inaenda kuwa moja kati ya viwanja vitatu venye kiwango bora Tanzania ikikaa nyuma ya Julius Nyerere na KIA. Uwanja wa Mwanza ni "Code 4D" hadi hapo ukarabati utakapokamilika utakuwa na sifa ya "Code 4E".

Hatuididimizi dhamira ya Mkuu kujenga kiwanja chenye ubora Chato, bali tunahoji kwa uelewa mdogo tu wa kanuni za Uchumi. Kwamba kiwanja hiki huko Chato kinaweza kuwa na matokeo chanya ya kiuchumi kama ambavyo wangeweza kuboresha uwanja wa ndege wa Mwanza?

Tunauhitaji Uwanja wa Mwanza kuliko ule wa Chato kwa sababu za kiuchumi ktk sekta ya Utalii. Tumekuwa tukilalamika sana kwa mbuga yetu ya Serengeti kukosa watalii wa kutosha kisa njia za usafiri kufika huko zilivyokuwa duni kushinda majirani zetu tunaopakana na mbuga ya Maasai Mara.

Uwanja pekee unaohudumia mbuga ya Serengeti kwa njia ya anga ni "Seronera Aistrip" ambapo huwa busy sana na huchukua ndege ndogo zenye abiria wasiozidi 50. Hii ndio moja kati ya "busiest Airstrip" kwa Tanzania.

Ili ufike Serengeti kupitia uwanja wa KIA unahitaji kutembea kilomita 284 kwa gari toka uwanjani, kwa kupitia uwanja wa ndege wa Arusha inakupasa utembee kwa gari umbali wa kama kilomita 226 wakati kwa kupitia Uwanja wa Mwanza,mtalii anatembea kilomita 166 hadi kufika geti la Ndabaka(?).

Kwa mahesabu hayo,kama ujenzi wa Uwanja wa ndege Serengeti ulishindikana,basi Uwanja wa ndege wa Mwanza ndio suluhisho la haraka ktk kuwafikisha watalii kwa urahisi ktk mbuga hiyo.Tukiusahau uwanja huo na kutazama zaidi ule wa Chato, tunaweza kuhoji dhamira hii ya maendeleo ktk kufika uchumi wa kati. Na kuhoji kwetu kusiababishe "hasira" kwa wenye mamlaka, bali ichukuliwe ni kama changamoto za raia kwa serikali yao.

Ukisefu wa usafiri wa uhakika na hasa ule wa njia ya anga, ndio unatukosesha mapato na kupunguza idadi wa Watalii ktk mbuga yetu ya Serengeti na hivyo wengi kuishia Maasai Mara.

Licha ya kuwa Serengeti ina ukubwa mara sita ya Maasai Mara,lakini bado "Vitanda" vya kupokea watalii katika hotel za Serengeti hivizidi 970 wakati wenzetu Maasai Mara ktk mbuga yao, kuna "Vitanda" zaidi ya 4,700. Hakika kupanga ni kuchagua.

Mpaka sasa Serikali kupitia Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania inamiliki viwanja vya ndege 58(ukijumlisha na Chato itakuwa 59),na wakati Uwanja wa ndege wa KIA ukiwa mikononi mwa Kampuni ya KADCO. TANAPA inamiliki karibu viwanja 26(Vingi vikiwa ni Airstrips),NCAA 2 na viwanja binafsi 93.

Katika hivi vya binafsi,vingi vinamilikiwa na wawekezaji toka nje ambao huvitumia kufanya udanganyifu ktk maliasili zetu.Uwanja wa ndege wa mgodi wa Geita(Mchauru) na Uwanja wa ndege wa Tishwa(HTSW) kule Loliondo unaomilikiwa na mtoto wa mfalme wa UAE ni moja kati ya viwanja vinavyopswa kutazamwa vizuri na serikali hii.

Uwanja huu wa Tishwa Loliondo ndio "unatisha", kwani huku ndege za familia ya mfalme hushuka moja kwa moja na kunyanyuka na mali nyingi. Umejengwa kiasi cha kuweza kutua na kuruka ndege kubwa.

Huu ndio uwanja ulio ktk eneo ambapo ukifika na kuwasha simu unakutana na meseji inasema "Dear Guest,Welcome to the UAE.Enjoy the best network coverage and other unmatched services only with Etisalat.Please use <+> or <00> before the country code for international calls.For directory services call 181,for availability of GPRS,MMS 3G roaming services call Etisalat Travellers help line 8002300 & for inquiries on Tourism,entertainment,shopping,etc call 7000-1-7000(Roaming rates apply).Have a pleasant stay in the UAE"

Labda wengine hatuna utaalamu wa Telecomunication, lkn kweli inawezakana hii kitu iingie tu kwenye simu yako wakati hujafanya "roaming". Haya ndio mambo ya TCRA kututoa tongotongo, sio zile mambo zao za .co.tz

Tunatakiwa tuwekeze ktk usafiri wa anga,lakini tuwekeza kimkakati na kwa faida za uchumi wa pamoja kama Taifa.Tukipewa sababu za kiuchumi zinazoupeleka uwanja wa ndege Chato wenye "Aerodrome Reference Code 4D" hatutakuwa na maswali.Tusipapata majibu yenye faida za kiuchumi,tutaendelea kuhoji hata tukiwa mafichoni.

Tukumbusha umuhimu wa Mwanza ktk kuihudumia Serengeti National Park, tutawakumbusha kuwa mlikuwa na mradi wa kujenge Uwanja wa ndege Serengeti,ila mkapambana na wanaharakati wa Ikolojia. Uwanja wa Serengeti ulipaswa kujengwa kati wa Kiwanja cha Ndege pale Mgumu.

Serengeti International Airport ilikuwa ni Code 4F, ilipaswa kuwa na runway ya mita 3,800 hadi mita 4,200.Mradi huo ulififia,sasa "tumefufukia" Chato na Uwanja wa "Code 4D".Je huku ndio kupanga na kuchagua??

Wakuu ukiyatafakari sana mambo ya nchi hii unaweza kuwa kichaa. Tuishukuru [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG], inatupa wasaa wa kuhoji haya nyuma ya "keyboard". Mambo haya enzi za Waziri wa Maliasili Aboubakari Mgumia yaliondoa maisha ya Ndugu Stan Katabaro. Tunapouanza mwaka mpya, tuzame katika sala na maombi. Ili wale wanaoomba tuwaombee kila siku,tusiwaombee tu wawe na afya njema..Bali walegeze mioyo ktk kuishughulikia mitandao kama mtandao wetu pendwa wa [HASHTAG]#Jamiiforums[/HASHTAG].

Nawatakia Mwaka Mpya mwema. Ninafunga mwaka na "Chato Interantional Airport".... Panapo majaliwa hapo mwakani. Nitakuwa likizo huko kwetu porini.... Ciaoooo!!!!
Mkuu hayo ya economics baadaye!! Ila naona walau arusha mnajengewa six ways... .tazara mnajengewa flai ova...

sasa wacha tukuze nanusafiri wa ndani...heko kwa magufurii...namwomba akajenge na bukoba international airport pale onukajunguti maana watu wa pwani hawajui watu wa mpakani wanavo teseka na usafiri.

Heko kwa magufuri.
Wakola waitu. Owawe kachumita naiwe olelembya. Kasinge. Mweite.
 
Uwanja umeshajengwa, mvimbe mpasuke mtajijua wenyewe.

Watetea mafisadi na wabaguzi wakubwa nyinyi( malofa)
Aiseee ungekua angalau na akili ya kumbu kumbu hata asilimia moja usingethubutu kumuita barafu hilo jina kama ni mtetea mafisadi!
Jaribu kuangalia thread za nyuma za huyu mtu!
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni
 
Mkuu Eudorite na Kipigi ni bahati mbaya tunataka kuupeleka mjadala kwenye hoja za "Ukada" na "Ukanda"...Hebu tubaki njia kuu

Miaka ile wakati Edward ni Waziri Mkuu,aliipigia sana chapuo ule mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege pale Mugumu,lkn watu wa ikolojia wakaupinga,na ktk kuupinga walisema Edward anataka uwanja huo sababu ana hotel yake ndani ya Mbuga na karibu na kiwanja hicho.

Sasa leo tena wengine mnasema watu wa "kaska" walipinga ujenzi wa uwanja ili usiwe shindani na KIA?
 
Kipigi,

Naungana na wewe.

Pist yake kwangu imekosa mantiki pale aliposema uwanja wa chato usijengwe ili kuboresha wa mwanza wakati anatambua kwamba

1. Maboresho ya uwanja wa mwanza yanaendelea hadi sasa na ujenzi wa uwanja wa chato hauja athiri maboresho ya uwanja wa mwanza.

2. Kuna uhitaji wa kujenga uwanja wa ndege kuhudumia mbuga ya serengeti. Badala ya kupiga debe uwanja huo ujengwe ndani au karibu na mbuga hiyo anashadadia uwanja wa mwanza ndio uhudumie serengeti ilhali upo miles away.

Ni seme tu kwamba badala ya kulalamikia uwanja kujengwa chato. Tusifie na kudai ujenzi na uboreshaji wa viwanja vingine vingi tu vinavyohitajika kote nchini kulingana mahitaji ya sasa na ya baadae.

Lengo isiwe kukataa maendeleo yasiwepo eneo flani bali yapelekwe kwa wakati kulingana na mahitaji na faida zitakazopatijana.

Mimi sikubaliani na wewe kabisa. Inawezekana unatoka Chato na una akili mgando kama ndugu yako. Huwezi kufikiria kujenga uwanja wa ndege wenye kiwango cha 4D Chato labda uwe mwandawazimu. Kwa mtu makini huwezi kuwaza hivyo, after all Chato sio makao makuu ya Mkoa wa Geita ili angalau upate sababu ya kujenga viwanja vya ndege kila mkoa tukianzia na Chato. Chato ni kijiji tu sawa na vijiji vingine. Hivi ndege inaenda kutua Chato kutafuta nini?

Mtu kufanya maamuzi kama hayo lazima awe na akili kama za Paul Kagame wa Rwanda au za Nkurunziza wa Burundi otherwise huwezi, ni aibu na inatia kinyaa.
 
Tatizo lenu mmelewa ulevi wa madaraka, kama suala ni kupata upendeleo mngeanza na mambo ya msingi kwenu kama ugonjwa wa mnyauko wa migomba, awasaidie research na suluhisho mngeondokana na njaa kali mliyonayo sasa.

Basi la Sabuni au Lushanga kwenda Chato halijazi abiria nauli chini ya elfu kumi mtajaza ndege nyie? Tumieni upendeleo huu wa raisi kutoka kwenu awasaidie vya maana sio white elephants.

Hakuna mmiliki wa ndege Chato, hakuna kiwanda zaidi ya ginnery ya ushirika, hakuna hata Hotel pale zaidi ya tule tu Lodge tuchafu nani apande ndege kwenda Chato mtukufu akitoka. Mwanakijiji wa Ilyamchele atapanda ndege?
Wacha kubabaisha watu bwana. Unahisi wale wanao kwenda mleba au biharamuro ama geita ama katoro ama kahama watalazimika kutumia mabasi..

Usisemehe mifuko yavwenzio kama Nina hela wenzako wanazo. Na habari ya viwanda na hayo mengine yatakuja.
 
Back
Top Bottom