Haters wa Jiji la Mbeya njooni hapa [Green City Home Sweet Home]

05cc106dbae35b03fd73f41f2bc94913.jpg
haya wenye jiji lao waje huku
 
Unasemaje hauna hadhi ya kuitwa jiji akati hata vigezo hujui, umekurupuka wewe
Ivi ni sehem gani Tanzania ambayo hakuna vumbi au ambapo mji mzima umejengwa vizuri kwa lami
Mkuu usilazimishe yai la chupa ya chai kupikia chipsi mayai.Mimi ni mnyakyusa pure na kwa sasa naishi Ituha.Narudia tena Mbeya haina hadhi ya kuitwa Jiji!
 
Mkuu usilazimishe yai la chupa ya chai kupikia chipsi mayai.Mimi ni mnyakyusa pure na kwa sasa naishi Ituha.Narudia tena Mbeya haina hadhi ya kuitwa Jiji!
Nitajie vigezo vinavyotumika Tanzania ili kuupa mji hadhi ya jiji
 
Njoo na ndugu wako, rafiki wako, jirani wako na uliosoma nao elimu ya awali, ya msingi na upili bila kuwasahau wa vyuo vya kati na vya juu.
Mkihamia Green City tutaacha kuongea lugha zetu pendwa ndani ya vyombo vya usafiri vya umma.
Vinginevyo LEKA TUJOBHEPO TUKA BHAJANGA OSWE!
KUKAJA KUNUNU MWEEEE
kuongea kikwenu c tatizo mkuu issue ni mtu wa siti ya mbele kupiga stori na wa siti ya nyuma tena kwa sauti kubwa yaan inakuwa kama mpo kilabuni vile ila mengineyo mko poa mkuu
 
Home Sweet Home

Mbeya ni mti wenye matunda acha upigwe mawe kuna baadhi ya watu wanajikuta tu wanaichukia mbeya ukimuuliza sababu hana au utaskia hamna mall, hamna maghorofa sijui hamna nini muulize babaako anayo iyo shopping mall, au unataka sehemu ya kupigia picha, ivi wanadhani kujenga mall ni kitendo cha kufungua zipu tu na kukojoa.

Mipango ya kujenga green city mall ipo na inaenda kwa hatua iyo rock city mall yenyewe imejengwa lini kama sio juzi tu ndo imezinduliwa.

Mnatakiwa mtambue Mbeya ilijengeka kitambo sana kabla hata aya mambo ya mipango miji hayajaanza watu walikua wanajimegea maeneo mitaa ya mwanjelwa, mabatini, simike na sehemu nyingine ambazo kwa kipindi icho zilikuwa zimechangamka. Saizi hayo maeneo ndiyo yanaonekana ya ovyo na sehemu ambazo zilikuwa zinaonekana mapori mfano New Forest, Iwambi, Isyesye kuna mpangilio mzuri wa majengo kwakua ni maeneo ambayo yamepangiliwa na mipango miji

Tena kuna mwingine utakuta anaishi kwenye nyumba ya udongo mkoani kwake uko afu anaanza kuidiss mby utaskia hamna nyumba nzuri mby. Ivi upo serious kweli?

Vile vile msisahau kuwa hii ni Tanzania tunaposema Mbeya ni jiji kwa level ya nchi yetu ni jiji tena kubwa sana limeiacha mikoa mingine mbali sana sana yani saaana. Sasa wewe unaesema Mbeya sio jiji uje na vigezo vyako vyenye maelezo sahihi kwanini sio jiji.

Mbeya sio kama mikoa mingine ambayo serikali inapeleka projects kubwa kwaajili ya kuiendeleza Bali mbeya inajengwa kwa kiasi kikubwa na wakazi wake.
Asante kwa maelezo yaliyo jitosheleza

Sent from my TECNO-W3 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom