Hata kama mkeo na watoto unawapenda usisafiri nao kwenye gari moja; wahenga waliishi muda mrefu kwa kukwepa haya

Wazee wa zamani waliona mbali sana kifikra kuhusu maisha. Awakuruhusu watoto wao watumie chombo kimoja cha usafiri, wakae pamoja au kuambatana mara kwa mara; waliogopa kuteketeza familia at once.

Leo hii imekuwa fashion kwa ndugu kusafiri pamoja, tunapotumia chombo kimoja cha usafiri upo uwezekano mkapotea kwa pamoja. Chukueni taadhari; kawia ufike.

Poleni wote mliowahi kupoteza ndugu kwenye ajali au majanga ambayo endapo tungetenganisha wana familia may be baadhi wangekuwa hai leo
Huu sio ushauri, ni SHERIA
 
Maisha maisha....hayajawahi kueleweka 100%.

Unawaambia nin wanao lala nyumba moja...yaani Baba, mama na watoto wote? Kuna majanga ya Moto...sawa chances za kutokea ni ndogo ila si zero chance.

Leo nimeona habari...dingi kaukumiwa maisha jela...kisa kalawiti mtoto wake WA kiume WA kuzaa...hapa waweza Kuta mama alilinda Sana watoto wake dhidi ya watu Baki...majiran na ndugu WA karibu...
 
Uaishi Mtwara, kwenu Bukoba, mmechukua likizo na mnapaswa kusafiri mwezi wa 12, una ki VANGUARD chako cha mkopo, hapo mtafanyaje?
Kanuni Huwa haibadiliki.....ni eidha Yeye aende hiyo likizo na baadhi ya watoto na Si na watoto woote na Sisi Wengine tutasubiri Next likizo
 
Kanuni Huwa haibadiliki.....ni eidha Yeye aende hiyo likizo na baadhi ya watoto na Si na watoto woote na Sisi Wengine tutasubiri Next likizo

Mkuu Mtongwe,

Tahadhari ni lazima kuchukua....lakini kifo hakikimbiliki ukifika wakati wake Mkuu....Labda wazazi wangu waliniathiri, nimesafiri mno na familia yangu, nikiwa na maana mke na watoto wangu, lakini hata nikiwa mtu mzima tumesafiri sana na ndugu zangu wa kuzaliwa, misiba, harusi na hata kusamilia ndugu....na hata kuvinjari tu! Labda niseme tu, licha ya tahadhari, ulinzi wa Mwenyezi Mungu umekuwa juu yangu.

Na kwa upande wangu binafsi, kuendesha gari ni kama hobby, miaka ya nyuma tukiboreka na mke wangu, ni kuchukua watoto siku ya Weekend, Mnatoka Mbezi ya barabara ya Bagamoyo, mnaenda hadi Pungu Kajiungeni, mnapinda kulia na kuendelea hadi kuja kutokea Kigamboni, vuka pantoni kurudi Mbezi, au Mbezi, unaelekea Bagamoyo, Msata, Chalinze na kurudi Dar...just for fun. Njiani mnanunua maembe, mananasi, mihogo kutokana na msimu.....imeacha kumbukumbu kwa wanangu. Safari za Dar hadi Morogoro nimezifanya mara nyingi, ni streach ambayo inabidi uwe mwangalifu mno mno. Nimepoteza rafiki yangu katika kipande cha Dar/Moro....lakini haikuzuia njaa yangu ya kuendesha.

Sijawahi ogopa kuwa barabarani na familia! Ikifika siku kuondoka Imefika....ukiogopa sana unaweza shindwa furahia maisha! Ni mafupi sana anyway!.
 
Wee mm naenda likizo niache kwenda na wanangu kwenye gari yao wakapande bus. Cha msingi ivunje safari kwa km 500 kila sikuusisafiri moja kwa moja tumia siku 2 ama 3 kama ni mbali sana

Hilo ni sawa Mkuu kama hauna haraka, nikiwa mdogo Mzee wangu alikua akifanya hivyo, Tunatoka Moshi tunalala Dodoma, naikumbuka sana Dodoma Hoteli nikiwa na miaka 7, tukitoka hapo tunaenda Iringa, Mzee anaonana na rafiki zake, siku moja au mbili tunaelekea Mbeya. Hiyo ilikuwa ni ni miaka ya nyuma, na gari ilikuwa Volkswagen, lakini naamini leo labda Mzee wangu angelikuwepo asingefanya hivyo.

Lakini nakubaliana kabisa kuivunja safari, unasafiri ukiwa relaxed, inasaidia kupunguza uchovu!
 
Haya mawazo ya ufukara wa akili. Mawazo ya kuamini miujiza na ushirikina. Hoja ya mkleta mada ipo sahihi lakini umeamua kuleta ushirikina wako bila sababu.
Mimi na wewe tunaishi dunia mbili tofauti, so please be humble..! Na uamini dunia unayoishi wewe.
 
Takadiri huwezi kuiepuka. Sote tunapanga ndani ya mipango ya Mungu,ikitokea mipango yetu imeendana na yake, basi hapo tumetiki. Ikitokea kinyume chake, hajali haikingiki.
Ama kifo ni uhakika kuliko uhai,na ni kifo pekee ndio kithibitisho cha kwamba tulikuwa hai.
 
Hili lizingatiwe sana dunia hii haiko fair watu wanawindana kama Simba na swala. Safari yako usiage sana watu wasio wa muhimu INASAIDIA.
Huko sahihi kabisa. Yani watu tunawindana utadhani wanyama. Cha kuogopesha adui humfaham kwa kuangalia tu machoni.

Ila yote ni kumkabidhi Mungu maisha yako.
 
Kweli pia watu wasiache kusoma visomo vikali kama albadeer wanaponusurika katika kila jambo inasaidia kufagia maadui wabaya.
 
Umemena, uzi wa busara, kuna jamaa akienda shamba kutoka mjini, anaendesha gari yake ndogo na mke anapanda basi. Safari ndefu huwa husafiri bila kuwa na familia, hata basi sio kupanda basi moja kwa pamoja.
 
Wazee wa zamani waliona mbali sana kifikra kuhusu maisha. Awakuruhusu watoto wao watumie chombo kimoja cha usafiri, wakae pamoja au kuambatana mara kwa mara; waliogopa kuteketeza familia at once.

Leo hii imekuwa fashion kwa ndugu kusafiri pamoja, tunapotumia chombo kimoja cha usafiri upo uwezekano mkapotea kwa pamoja. Chukueni taadhari; kawia ufike.

Poleni wote mliowahi kupoteza ndugu kwenye ajali au majanga ambayo endapo tungetenganisha wana familia may be baadhi wangekuwa hai leo
Ni mkweli mkuu, sitasahau siku hiyo tumekodi gari binafsi kwa ajili ya kwenda Kula Christmas Kama familia, tulipata ajali mbaya sana... Dada zangu wa wili Walikufa . R.I.P 😭😭😭😭
 
Kwa hali ya mafuriko ya sasa, naona sio salama ndugu kukaa mkoa mmoja
 
Back
Top Bottom