Hata kama mkeo na watoto unawapenda usisafiri nao kwenye gari moja; wahenga waliishi muda mrefu kwa kukwepa haya

Watu wana safiri kama kumbikumbi
Wanajazana familia nzima kwenye noah sjui prato alphard
Njia nzima ni kuhappy miziki na mitungi...

Ova
 
Hizi ni juhudi zetu wanadamu hasa tunapofikwa na mambo magumu na yenye kuumiza mioyo yetu....

Lakini kiimani kila mja ataondoka kwa wakati wake.....na wakati wake ukifika haijalishi mko pamoja au mpo mbali mbali bali ataondoka......kila mja ataishi na kurudhukiwa kwa kadri alivyokadiriwa.......kuanzia uhai mpaka ridhiki.......

Hekima na busara sio kuogopa kifo bali ni kujiandaa na maisha baada ya kifo kwa kuyazingatia maarisho yake na kukaa mbali na aliyoyakataza.....

Mungu atujaalie mwisho mwema kwenye maisha yetu.......

IJUMAA KAREEM......
Mkuu vyema kumuamini na kumtumainia Mungu na kuomba Dua lakini hii isikufanye ukaacha kuishi kwa misingi tahadhari ya Dunia kumbuka Mungu ndiye aliyeweka hio misingi ya Dunia sio kuomba tu na kujiachia.

Omba Mungu then fanya juhudi zako za kibinadamu.

Anayemuomba Mungu tuepushe na ajari na tupe umri mrefu then akafanya Kama kilichoandikwa kwenye Mada ni Bora zaidi kuliko aliyeomba Mungu the same na akapanda gari moja na familia....Toka nizaliwe sijawai sikia familia iliyokufa kwa mkupuo wakiwa sehemu tofauti ila daily nasikia taarifa za kufa familia nzima kwa incidence Kama hizi.
 
Treni ni salama zaidi kwa familia,barabara zetu siyo salama kabisa,ni nyembamba,leseni za udereva kutolewa kiholela.Wewe unaweza kuwa dereva mzuri lakini dereva mwenzako siyo makini anahama njia anakufuata.Treni ni bora sana kwa mikoa yenye mtandao wa reli.
Watu wajinga kweli. Dawa unamkwepa tu na ujinga wake.
 
Pana vyakula navyo huweza teketeza familia nzima mfano sumu kuvu,au mjusi katumbukia kwenye chakula msijue mkapikia humo humo ni hatari kuacha mboga wazi.
Meli mv bukoba na spices pia zimemaliza familia nzima

Hivi hawa mijusi wa majumbani ni kweli wana sumu au ni story tu za vijiweni?

-Sumu kuvu nayo ni hatari.

Poleni sana familia ya Msuya.
 
Ajali ya MV spice islanders ndio iliua wanafamilia wengi, watu wengi walipoteza watu wa familia moja kwa mpigo. Kuna jamaa nilikutana nae yeye alifariki mke wake na wtt watatu. Kuna nyumba mpk leo pemba zimefungwa hazina wakaazi baada ya familia nzima kufariki kwenye ile ajali.

Refer ile ajali ya mtt Anna aliepoteza wazazi wake wawili na ndugu zake watatu. So sad.

Ila ndio hivyo kuna wakati mazingira yanalazimisha kusafiri kwa pamoja. Na kumuomba Mungu
 
Pana vyakula navyo huweza teketeza familia nzima mfano sumu kuvu,au mjusi katumbukia kwenye chakula msijue mkapikia humo humo ni hatari kuacha mboga wazi.
Meli mv bukoba na spices pia zimemaliza familia nzima
Hata ajali za moto nazo jee!!! Kuna mwaka watu 9 wa familia moja waliteketea kwa moto usiku mmoja.

Mwaka 2003 jirani yangu alipoteza mume na wtt wa kuwazaa wawili pamoja na mtt wa shemegi yake. So sad

Kuna ule mwaka zanzibar umeme ulizimwa kama miezi mitatu ivi, kuna familia walikufa watu wanne baada ya kulala na generator ndani, wamevuta hewa ya sumu
 
Mkuu vyema kumuamini na kumtumainia Mungu na kuomba Dua lakini hii isikufanye ukaacha kuishi kwa misingi tahadhari ya Dunia kumbuka Mungu ndiye aliyeweka hio misingi ya Dunia sio kuomba tu na kujiachia.

Omba Mungu then fanya juhudi zako za kibinadamu.

Anayemuomba Mungu tuepushe na ajari na tupe umri mrefu then akafanya Kama kilichoandikwa kwenye Mada ni Bora zaidi kuliko aliyeomba Mungu the same na akapanda gari moja na familia....Toka nizaliwe sijawai sikia familia iliyokufa kwa mkupuo wakiwa sehemu tofauti ila daily nasikia taarifa za kufa familia nzima kwa incidence Kama hizi.
Asante kwa maneno yako mazuri.....
 
Kanuni yangu ni kutokutumia chombo kimoja Cha usafiri na mke wangu kipenzi..........hata likitokea watoto wetu wasikose wa kuwasimamia

Japo Naamini kifo hakiepukiki na Siku yako au zenu zikiwa zimefika mtaunganishwa na mauti bila kujali umbali mliopo
Mkilala nyumba moja mjitahidi kutengana na vyumba likitokea la kutokea msije mkaacha wtt wenu yatima
 
Lakini uzembe wakati mwingine ukawa wa Gari lingine na sio wewe. Lipo tukio la msabato mmoja alikuwa muhadhiri Moro miaka 20 iliyo pita ilitokea maaeneo ya urafiki basi lilihamia upande wake

Nakubali kabisa Mkuu, barabarani nazo ni changamoto kubwa. Kwa wenzetu ajali nyingi zinapunguza kwa kuwa na miundombinu yenye kuzingatia watumiaji wa barabara na wingi wake.

Barabara nyingi ambazo tungezifananisha na barabara kuu zetu, ni Dual Carriage, Hakuna kabisa kupishana! Ajali kama hii haiwezi kutokea kwenye barabara za Interstates US......Ukilala au ukisinzia utatoka barabarani tu! Anyway somo ni kuchukua tahadhari tu tunapokuwa katika vyombo hivi vya moto.
 
Back
Top Bottom