Hassan Ngoma Clouds 360 tafuta kazi nyingine, uchambuzi umekushinda

Kama ameanza kujipendekeza kwa CCM ajue kuwa huku mitaani ipo laana dhidi ya matendo ya CCM kea

hako kajamaa
Hassan ngoma ni mwanachama wa chadema na wote clouds wanajua hilo na kipindi Tundu lisu kapigwa Risasi aliamua kujitoa mhanga kumtetea Lisu lakini Ruge akamsimamisha kazi na mikwara mingiine ya chini kwa chini, , nadhani kaamua kujitoa fahamu kuipenda CCM kwenye Tv ili apewe ukurugenzi, katibu Tawala na Ukuu wa Wilaya lakini moyoni ni chadema, kwa kuwa JF ni jukwaa kubwa akipita humu lazima atajifunza kitu.
Ukishakuwa mwandishi wa chombo huru hupaswi kuonesha hisia zako kwa chama chochote otherwise angekuwa anafanyia Tanzania daima au Gazeti la uhuru

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Halafu shida ya hawa jamaa wa 360, huwa wanaongelea vitu kijuu juu mno, tena wakati mwingine kwa kupotosha kabisa. mfano kuna kichwa cha habari kwenye gazeti. watasoma kichwa cha habari tu, halafu wataanza kuulizana wao kwa wao, kwanini alifanya hivi, kwa nini asifanye vile? sasa ukija kusoma hiyo habari, unakuta kile walichokuwa wanaulizana, tayari kimeelezwa vizuri tu mle ndani. sasa nadhani wanafanya makusudi kupotosha ili wauponde upinzani na kuushangaa, wakati maelezo mazuri ya kile kilichofanyika yapo kwenye gazeti. kwa hiyo wanajadili mambo yasiyokuwepo na wanatumia nafasi hiyo kuuponda upinzani. ni mbinu chafu kabisa.

Njia nyingine wanayotumia, kama kuna tukio kubwa linalohusisha upinzani na serikali au vyombo vya serikali, na ambalo halijakaa vizuri kwa serikali, utaona wanatumia muda mwingi kufanya utani kuhusu vitu vya mtaani ambavyo havina maana kabisa. basi watapiga domo weee, wakisoma kichwa cha habari cha taarifa hiyo, wanaiacha bila comments. Hii ni namna ya kuwafanya watu wabaki kwenye non-issues.

angalau Magic Radio, akina Kibwana Dachi, huwa wanajaribu, japo siku hizi ni waoga baada ya kupigwa faini mara kadhaa na kufungiwa pia.
 
Mtamlaumu bure... Kwa sasa wengi ni waongo mdomoni lakini mioyo yetu inajuwa ukweli
 
Ashakum siyo matusi ila hawa clouds nao sijui hawa baadhi ya watangazaji wao wanawaokotaga wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni matokeo ya walikoanzia na kujilazimisha kuwa wasikostahili. Nijuavyo, Clouds ilianza kama Talk Radio. Talk radios hutegemea utaalamu wa watu wanaowaalika ktk mijadala. Tatizo la hawa jamaa wamejifanya kama ni wanahabari serious kushindana na TBC au BBC au VOA au zingine ndani ya nchi ambao wana utaalaamu na taaluma.

Clouds walistahili kuwa ni waunganishaji na welevu wa kutafuta watu wenye weledi ktk mijadala yao. Ubaya wao wanakomaa wenyewe kujadili mambo wasiyoyafahamu. Ni aibu maana hizi siyo enzi za sauti nzuri ya utangazaji, ni enzi za taaluma ya utangazaji. TUwavumilie tu maana bahati mbaya mitaani ndo wanaonekana wanapendwa na kusikilizwa, wakijisemea hayo ya kijiweni.
 
Ni jambo la hatari kumuweka mtu kuchambua mambo katika radio au Television inayotazamwa na watu wengi hasa vijana wakati mtu huyo eitha hauwezi uchambuzi (uwezo Wa IQ mdogo) au analamba miguu ya upande mmoja kwa matarajio binafsi.

Leo kwa mara nyingine tena nimemsikia akichambua na wenzake kuhusu yanayoendelea Uganda na issue ya kesi ya Mbowe na wenzake Kisutu.

Hakika nimemshangaa kwa kuonyesha kwake wazi kuwa anaunga mkono yatendwayo kwa wapinzani kwenye issue hizo na kuwa wao ni wakorofi.

Badala ya kulamba miguu ili upate uteuzi kama yule mwingine ambaye tayati Halmashauri ya Mbulu imeshamshinda uende tuu ukatafute kazi nyingine unayoimudu vizuri kuliko kupotosha jamii hasa vijana wanao tazama sana Clouds TV

Sent using Jamii Forums mobile app

Hassan kapata Division four mtihani wa taifa wa foum four. unatajai nini hapo kama si pumba na matapishi.
 
Acha husda dogo namfuatilia sana, anaweza saaaaana anajua, ukute ni wivu mnafanya nae kazi clouds hlf unaleta umbeya hapa, jipange
 
Mambo ya JF kila mtu high IQ kila mtu kasoma kumbe wengine wasukuma mikokoteni. Me nadhani muache kuangalia Clouds mfungue TVs zenu mtangaze mnsyotaka nyinyi kusikia masikioni mwenu
 
Mambo ya JF kila mtu high IQ kila mtu kasoma kumbe wengine wasukuma mikokoteni. Me nadhani muache kuangalia Clouds mfungue TVs zenu mtangaze mnsyotaka nyinyi kusikia masikioni mwenu
Mjinga ni mjinga tu hata awe Rais wa nchi kwani watu si wanaoana matendo yake? Huyo Hassan kuonesha udhaifu mkubwa kiasi cha kusemwa si dhambi Mbona watu wasiwaseme hao coo partners wake. Ajirekebisha au kama hatoweza basi asiifanye hiyo kazi haiwezi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom