Hashimu Rungwe: Polisi wote ni CCM, tunahitaji tume huru ya Uchaguzi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,014
9,883
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashimu Rungwe, ametoa kauli inayotia msukumo kwa mchakato wa kuboresha demokrasia nchini Tanzania. Akizungumza katika mkutano wa wadau wa demokrasia ulioratibiwa na TCD hii leo, Rungwe amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika kwa uhuru na uwazi.

"Wananchi wanataka mtu aongee akiwa huru na sio mtu akiongea akadhibitiwa," Rungwe ameonyesha umuhimu wa kurekebisha sheria za uchaguzi kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa njia huru na haki. "Uhuru wa uchaguzi unategemea na uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu, sasa bila kurekebisha hizi sheria hakutakuwa na uchaguzi," ameongeza.

Ametoa wito wa kuanzishwa kwa tume huru ya uchaguzi ambayo haitakuwa na uhusiano na serikali au vyama vya siasa. "Tunapaswa kuunda tume ambayo haitakuwa na uhusiano na serikali. Wasiwe watu wanaotegemea kuteuliwa katika nafasi zozote katika serikali,".

Kwa mujibu wa Rungwe, ni muhimu kuwa na mchakato wa kuchagua wajumbe wa tume ambao hawana uhusiano wowote na serikali au vyama vya siasa. Hii itasaidia kuhakikisha kuwa tume inafanya kazi yake bila upendeleo na bila kuingiliwa na maslahi ya kisiasa.

Rungwe pia ameashiria umuhimu wa kujifunza kutoka kwa uzoefu wa nchi nyingine kama vile Zambia ambapo kulikuwa na tume huru ya uchaguzi. Amezungumzia umuhimu wa kuwa na tume huru itakayosimamia uchaguzi bila kuingiliwa na vyombo vya usalama au maslahi ya vyama vya siasa.

Suala la polisi kujihusisha na uchaguzi ameona inatia doa kwa kuwa amesema, polis wote ni CCM.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom