Hasheem awaponda viongozi wa kikapu Tanzania

TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
11,514
11,277
NYOTA wa mchezo wa kikapu wa Tanzania, anayecheza katika ligi ya NBA ya Marekani Hasheem Thabeet amesema viongozi wa mchezo huo nchini wasimtumie kama ngazi kwani mafanikio aliyoyapata ni juhudi zake binafsi.

Hasheem aliliambia gazeti moja la kila siku nchini kwamba ameshangazwa na viongozi wengi kumtumia yeye kama daraja kwa kujidai kuwa ndio waliomsaidia hadi hapo alipofikia wakati si kweli.

''Nadhani kuna watu wanataka kujinufaisha kwa kusema wamenisaidia kwa ajili ya uchaguzi wa chama chao, lakini si kweli. Nashangaa baadae wengine wamenifuata hadi Marekani na kudai kuwa wametumwa kunipongeza alisema."

Hashim alikuwa akimaanisha baadhi ya viongozi waliomfuata huko kwa madai wametumwa na Rais Kikwete kwa kuwa amekuwa akimtembelea mara nyingi na kumpa moyo.

Akizungumzia kuhusu mchezo huo nchini, Hashim alisema mpira wa kikapu utachukua miaka mingi kufikia mafanikio kwa kuwa viongozi hawana nia ya kusaidia wachezaji.

''Watu wanaohusika ndio wanafanya mchezo huu ushindwe kuendelea kwani tangu niondoke nchini hadi sasa, hali ni ileile hakuna maendeleo, hata viwanja viko katika hali ileile,'' alisema.

Alitahadharisha kuwa kutokana na hali hiyo itakuwa vigumu kwa Mtanzania mwingine kupata nafasi kama yake kwa hapa nchini bila ya kujipeleka mwenyewe kwa juhudi zake, “labda mmoja katika milioni moja sijui kama itatokea,'' alisema

Click here for source.

8D6U1496.JPG

wachezaji wa mpira wa kikapu
 
kapata shavu anaanza kubwabwaja

Nyie wadandiaji, mnapoambiwa ukweli hampendi mnaishia kulaumu kuwa anabwabwaja. Kazaneni na nyie muone kama ni rahisi kufikia alipofikia mwenzenu; mmezoea kunyonga kuchinja hamuwezi!!
 
kapata shavu anaanza kubwabwaja

Stories around here are the kid has no offensive or shotting skills, the only thing going on for him at this point is his height and there is a saying you can't teach height it is a God given gift. Expectations are he may improve with time, until then he better walk the walk than talk the talk.
 
Hasheem Give young people strategies,

wajengee hisia ya kutambua uwezo wao na siyo kuwaponda au kuongea siasa.

Tell them what to do! Hawawezi kwenda marekani wote waeleze wafanye nini?.

Ongea kwa option ya mmoja mmoja
 
this boy should come up plan b for sure, sio kujisifia na kusema "kule marekani blah blah" kila anachoulizwa, when you say viwanja vibovu hakuna wa kuweza kwenda marekani kama yeye ni ulimbukeni, mbona yeye kaenda na ubovu huo huo? aangalie wenzie, dikembe mutombo kafanya development kubwa sana kwao, kajenga viwanja vingi vya basket ball na mpaka hospital, patric vieira baada ya kuona kwao soccer maendeleo si mazuri sana kajenga academy kule senegal, rio ferdinand anajenga academy uganda, hata wa hapa kwetu na vihela vyao vidogo wanatafuta jinsi ya kusaidia, mtemi ramadhani na boniface mkwasa wana academy yao, kipingu ana ya kwake etc.

so huyu dogo angekuja na plan b kama anataka kuona maendeleo sio kuponda tu.
 
Ni utamaduni wetu tuliojijengea kurukia kila tunachokiona kinaelea. Wape ukweli wao Hasheem kisha elezea mikakati uliyotumia kufika hapo ulipo. Siku zote jambo jema hupongezwa na huigwa!
 
Stories around here are the kid has no offensive or shotting skills, the only thing going on for him at this point is his height and there is a saying you can't teach height it is a God given gift. Expectations are he may improve with time, until then he better walk the walk than talk the talk.
its not news
Grizzlies new what sort of players he is and thats what they wanted, he is gonna improve over time like every body else...

one good thing about him, he knows when somebody is trying to take advantage of his new found fame. go and tell your friends at ministry of sports and nba tz association wasijivunie kitu ambacho hawajapanda...
 
this boy should come up plan b for sure, sio kujisifia na kusema "kule marekani blah blah" kila anachoulizwa, when you say viwanja vibovu hakuna wa kuweza kwenda marekani kama yeye ni ulimbukeni, mbona yeye kaenda na ubovu huo huo? aangalie wenzie, dikembe mutombo kafanya development kubwa sana kwao, kajenga viwanja vingi vya basket ball na mpaka hospital, patric vieira baada ya kuona kwao soccer maendeleo si mazuri sana kajenga academy kule senegal, rio ferdinand anajenga academy uganda, hata wa hapa kwetu na vihela vyao vidogo wanatafuta jinsi ya kusaidia, mtemi ramadhani na boniface mkwasa wana academy yao, kipingu ana ya kwake etc.

so huyu dogo angekuja na plan b kama anataka kuona maendeleo sio kuponda tu.

Give him a break ebo!! yani hata mechi ya kwanza hajacheza mshaanza kumpangia nini cha kufanya?
 
this boy should come up plan b for sure, sio kujisifia na kusema "kule marekani blah blah" kila anachoulizwa, when you say viwanja vibovu hakuna wa kuweza kwenda marekani kama yeye ni ulimbukeni, mbona yeye kaenda na ubovu huo huo? aangalie wenzie, dikembe mutombo kafanya development kubwa sana kwao, kajenga viwanja vingi vya basket ball na mpaka hospital, patric vieira baada ya kuona kwao soccer maendeleo si mazuri sana kajenga academy kule senegal, rio ferdinand anajenga academy uganda, hata wa hapa kwetu na vihela vyao vidogo wanatafuta jinsi ya kusaidia, mtemi ramadhani na boniface mkwasa wana academy yao, kipingu ana ya kwake etc.

so huyu dogo angekuja na plan b kama anataka kuona maendeleo sio kuponda tu.

Hiyo mifano yako ipo tafauti sana. Hao jamaa unaocompare na Hasheem wameanza siku nyingi sana. Wameshajijenga kimaisha, jina nk. Hasheem ndiyo kwanza kaanza kucheza Pro. Basketball, mpe muda.
 
Nae hasheem hana lolote atulie asiwe mwanasiasa uchwara kuponda wenzake....aombe support na awe mshikanao basii aianze beef yasiyo maana....
 
Hasheem, kwa wewe uliyepata bahati ya kufika hapo ulipo unatakiwa kutoa mfano kwa hao viongozi wanaopenda ujiko badala ya maendeleo. Kutoa misaada si lazima uwe kiongozi, mfano ni Dikembe Mutombo amefanya mengi mazuri nchini kwao. Hivyo wewe pale utakapokuwa na uwezo huo unaweza kutoa changamoto kwa kusaidia kwa lolote lile. Mfano mchango wowote kusaidia kukuza mchezo huo hata kwenye mashule ya msingi au sekondari.

Watu au makampuni mengine huko USA wanaweza kuamua kuja kuwekeza kwenye michezo au biashara mbalimbali kama wewe utakuwa balozi mzuri wa nchi yako kupitia fani yako. Kwa kufanya hivyo unaweza ukawa sehemu ya mpango wa Taifa wa Kupunguza Umaskini Tanzania kwani wakiwekeza Tanzania watakuwa wame-create AJIRA.
NAKUTAKIA KHERI NJEMA.
 
Nae hasheem hana lolote atulie asiwe mwanasiasa uchwara kuponda wenzake....aombe support na awe mshikanao basii aianze beef yasiyo maana....

Hizo beef za kujitafutia si nzuri, Hasheem bado ni mtoto mdogo sana, hajajua ubaya wake.

Angalau angesubiri ajiimarishe, hajacheza hata mechi moja anatafuta beef na watu wa michezo nchini mwake.
 
Back
Top Bottom