Harusi ya Ajabu

mayenga

JF-Expert Member
Sep 6, 2009
4,118
1,966
Hiki kisa ni cha kweli na cha kusikitisha.

Ni asubuhi njema ,mipango ya harusi imekamilika na siku imewadia.Hawa(Mke na Mume) wanajiandaa kuelekea kanisani,kwa lengo la kufunga ndoa(au kubariki kama ilivyozoeleka kwani walikwishakaa kwa muda wa miaka miwili pamoja).

Ndoa imefungwa,tarumbeta na shamrashamra za kila mahali zinaoonekana,msafara wa magari na watu wa kila aina unaipamba harusi ile.Hatimaye muda wa kuingia ukumbini kwa maharusi unawadia,na kazi ya msema chochote (MC) inaanza rasmi.

Kama kawaida wageni kutoka ukeni na kuumeni wanakaribishwa,tukIo la kwanza ni kufungua champaigne kutakiana kheri na baraka.Kipindi chote hiki kuanzia asubuhi mpaka muda huo nyuso za maharusi zinaonesha tabasamu ya khali ya juu.

Ukawadia wakati wa kukata keki,hapa ndipo,sinema ya kusikitisha ilipoanza,kama mnavyojua staili ya ukataji wa keki inategemea na maandalizi,inasemekana bwana harusi aliomba kila mtu akate keki yake ila kwa wakati mmoja.MC katika kukoleza na kuchangamsha shughuli,akawaambia maharusi kunyanyua juu visu vyao na kuanza kuwahesabia: moja..........mbili..........tatu,ghafla!! sura ya bwana harusi inabadilika,MC anapohesabu kwa mara ya tatu,badala ya kukata keki,kisu cha bwana harusi kinatua kwenye tumbo la bibi harusi,utumbo wote nje.Historia ya maisha ya watu hawa inaishia hapa,historia imeandikwa hivyo.

Bwana harusi anaanza kulia na kulalama:"huyu mwanamke kazidi kwa usaliti,nimemkomesha..............!

RIP Bi harusi!!

My take: Visasi au ukimya ni bomu baya sana kwa wapendao>Vunja Ukimya, Zungumza na mwenzio.
 
Mh wapi hii ilitokea??
Magazeti ya Shigongo yametega kamera kwenye kumbi zote hawakuipata hii?
 
Kama ni kweli, basi mume ameonyesha udhaifu mkubwa. Ukitaka kumwadhibu mtu kwa raha zako lazima ushuhudie anavyovuvia kwa uchungu baada ya kumuadabisha..hapo ndo utabaki roho kwatu!!! si kuua kinyama kiasi hicho. Labda kama bw. alikuwa Mkurya ama nyarukolo wa zamani!
 
Story haikuishia hapo bado inaendelea.........

MC akasema mlango wa ukumbi ufungwe ili bwana Harusi asiweze kutoroka,kila mtu ukumbini alikuwa na hasira kali kwa tendo ambalo bwana harusi alikusudia kulifanya kwa mikono yake iliyozoea kutekeleza maovu yaliyokuwa yakiamrishwa na moyo wake wenye ukatili na ukosefu wa chembe za ubinadam.Ukumbi uligeuka kama uwanja wa vita na kila roho iliyomo ndani ya ukumbi ilikuwa ikipanga jinsi ya kuiadibu roho ya binadamu mwenzao aliyefanya ukatili huo,kutokana na kulikuwa na vinywaji ndani ya ukumbi,sahani,glass,visu,chupa za bia hivo vifaa viligeuka kama silaha....Bwana Harushi kichwani mwake alikuwa akifikiria mbinu moja tu ya kutoroka ambalo wao hawakuligundua na yeye mwenyewe hakuwa na uhakika kama hiyo mbinu itamsaidia,mara ikatokea.............
INAENDELEA
 
Excellent! you are violating my copy right!,you are feeding me with your own words which in my opinion does not contemplate with my intention,you have accorded me with the treatment I do not deserve.I initially put it squarely and casually that,this is the true story.This is against copyright laws!!!!

Back
Top Bottom