Harusi ya Ajabu

I suggest JF awards you a PHD like Kikwete, Nchimbo, Mahanga, the list is endless in CCM!
 
Hii imetokea Sayari gani?

Na udaku wangu wote nisiipate? Kweli nazeeka vibaya!
Ah ah ah ah, mkuu, ukiona yanakupita ujue ndio bye bye ujana karibu uzee...! Ah ah ah ah.

Hii riwaya sio made in shigongo kweli!?
 
Kwa maendeleo haya Shigongo inabidi akae chonjo. Mayenga anakuja kwa kasi ya ajabu. Hadithi yake inatufundisha tusibariki ndoa na kukata keki mbili kwa wakati mmoja.
 
Ah ah ah ah, mkuu, ukiona yanakupita ujue ndio bye bye ujana karibu uzee...! Ah ah ah ah.

Hii riwaya sio made in shigongo kweli!?

Hata Shigongo hawezi kupika kitu ya namna hii.........!

Huu upishi sijawahi kuona tangu nizaliwe!

Hii ndio JF zaidi ya uijuayo mkuu!
 
Hiki kisa ni cha kweli na cha kusikitisha.

Ni asubuhi njema ,mipango ya harusi imekamilika na siku imewadia.Hawa(Mke na Mume) wanajiandaa kuelekea kanisani,kwa lengo la kufunga ndoa(au kubariki kama ilivyozoeleka kwani walikwishakaa kwa muda wa miaka miwili pamoja).

Ndoa imefungwa,tarumbeta na shamrashamra za kila mahali zinaoonekana,msafara wa magari na watu wa kila aina unaipamba harusi ile.Hatimaye muda wa kuingia ukumbini kwa maharusi unawadia,na kazi ya msema chochote (MC) inaanza rasmi.

Kama kawaida wageni kutoka ukeni na kuumeni wanakaribishwa,tukIo la kwanza ni kufungua champaigne kutakiana kheri na baraka.Kipindi chote hiki kuanzia asubuhi mpaka muda huo nyuso za maharusi zinaonesha tabasamu ya khali ya juu.

Ukawadia wakati wa kukata keki,hapa ndipo,sinema ya kusikitisha ilipoanza,kama mnavyojua staili ya ukataji wa keki inategemea na maandalizi,inasemekana bwana harusi aliomba kila mtu akate keki yake ila kwa wakati mmoja.MC katika kukoleza na kuchangamsha shughuli,akawaambia maharusi kunyanyua juu visu vyao na kuanza kuwahesabia: moja..........mbili..........tatu,ghafla!! sura ya bwana harusi inabadilika,MC anapohesabu kwa mara ya tatu,badala ya kukata keki,kisu cha bwana harusi kinatua kwenye tumbo la bibi harusi,utumbo wote nje.Historia ya maisha ya watu hawa inaishia hapa,historia imeandikwa hivyo.

Bwana harusi anaanza kulia na kulalama:"huyu mwanamke kazidi kwa usaliti,nimemkomesha..............!

RIP Bi harusi!!

My take: Visasi au ukimya ni bomu baya sana kwa wapendao>Vunja Ukimya, Zungumza na mwenzio.

Duh!!!!!!!!!! waliwekewa kisu cha kukata nyama kwa kweli duh!!!!! this is disastrous
 
story haikuishia hapo bado inaendelea.........

Mc akasema mlango wa ukumbi ufungwe ili bwana harusi asiweze kutoroka,kila mtu ukumbini alikuwa na hasira kali kwa tendo ambalo bwana harusi alikusudia kulifanya kwa mikono yake iliyozoea kutekeleza maovu yaliyokuwa yakiamrishwa na moyo wake wenye ukatili na ukosefu wa chembe za ubinadam.ukumbi uligeuka kama uwanja wa vita na kila roho iliyomo ndani ya ukumbi ilikuwa ikipanga jinsi ya kuiadibu roho ya binadamu mwenzao aliyefanya ukatili huo,kutokana na kulikuwa na vinywaji ndani ya ukumbi,sahani,glass,visu,chupa za bia hivo vifaa viligeuka kama silaha....bwana harushi kichwani mwake alikuwa akifikiria mbinu moja tu ya kutoroka ambalo wao hawakuligundua na yeye mwenyewe hakuwa na uhakika kama hiyo mbinu itamsaidia,mara ikatokea.............
Inaendelea
hdithi haiuziki mkuu, wewe unasema....kwa kosa alililokusudia kulifanya,mwenzio anasema utumbo nje.wapi na wapi.
 
hizi hadithi za kubembelezea machangudoa wapate usingizi au................?
 
Back
Top Bottom