Harambee ya Tv Imani Ilikuwa si Habari?

Status
Not open for further replies.
Mwenzio Malaria sugu alikuja na thread yake ya "itv ina ubaguzi wa kidini" ikafungwa muda si mrefu, bahada ya kuonekana inaanza kuhatarisha amani na mshikamano tuliokuwa nao ndani ya JF. na wewe naona unaanza hayohayo. Hivi hamna kingine cha kuandika humu zaidi ya habari zinazoashiria udini?
Hawa wanapewa vichwa na wale wanaojibu thread zao... dawa yao ni kuwapotezea tu
 
Bornvilla,
Nasikitika kwa kilichotokea. Naamini kuna somo la kujifunza kwenye jambo hili.
1. Press ilialikwa kwa ujumla wake?
2. Mialiko ilipitaje?
3. Je, ni vyombo vyote vya habari vilialikwa au kulikuwa na ubaguzi wa vyombo kualikwa?
4. Je, Kuitangaza habari hii kungeisaidiaje jamii ya waandaaji?

Ningependa kuondoa hisia za udini hapa kwenye forum ya wasomi na wasio wasomi. Tunapotaka kuleta udini ni lazima tuwe na hoja tusije kuwa kama wale wasemao "sisi tunaonewa sana" lakini ukimuuliza unaonewaje, hana hoja ya msingi.

Nimekuwa nikisikia hoja ya kuonewa na kuwa na umoja miongoni mwa waislamu kwenye kila jambo na nadhani hii ni strategy zaidi kuliko uhalisia. Ningependa kuomba jamii ya wasomi wa Kiislamu kufuatilia mambo haya na kuelimisha waislamu kuondoa hoja zisizo na mashiko za kuonewa bila ya kuwa na ushahidi na vigezo vya kweli vya kuonewa ndipo Uislamu utakapojijengea heshima kwenye jamii. Malalamiko peke yake hayatawasaidia waislamu kutoka mahali walipo.

Nimesikia mara nyingine wakidai elimu wakristo tu ndiyo wanaopewa kipaumbele na waislamu wanataka haki sawa hata kama hawako competent...hakuna mtu anayepaswa kuchaguliwa kwa dini yake bali kwa comepetencies zake. Akina mama wakati mwingine nao wanalia tunaonewa lakini ukifuatilia wako nyuma mbali sana kwenye competencies na wanasiasa uchwara wakawasikiliza na kuwa viti vya bure bungeni na huko hawana cha maana wanachochangia.
Huu ni uhuni.

Najua kuna jamii kubwa sana ya waandishi wa habari waislamu ambao wangepewa fursa ya kufika kwenye harambee hiyo wangeandika tu, jichunguzeni ndugu zangu kabla hamjaandika hoja dhaifu za kuonewa kwenye jamii ya watu wanaofikiri na ikazidi kuwashushia hadhi.

Ni ushauri tu.
 
Mmepeleka malalamiko yenu kwa maandishi kwa vyombo husika au kama kawa na mambo yetu ya kulalamika!Na je vyombo hvyo vilialikwa?Kama hawakualikwa kwanini waipe kiupaumbele?Au ule mtindo wetu mwingine dhanifu,kwamba watakuwa wanajua tu!Na je wahusika wa harambee wametoa tamko kuhusu ishu hii?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom