Harakati zipi zina Tija: UAMSHO au M4C?

MPIGA ZEZE

JF-Expert Member
May 16, 2011
2,539
2,296
Mimi ni mpenzi sana wa mienendo ya kisiasa nchini Bongoland. Ninatumia jina Bongoland makusudi kutokana na hoja yangu hii hapa chini:

Katika miaka ya hivi karibuni (miwili, mitatu iliyopita) kumeibuka vuguvugu la 'harakati za ukombozi'. Vuguvugu ambazo ninaweza kuzianisha katika aina tatu:

(a) Wazanzibari wanataka kujikomboa kutoka mikononi mwa ‘mkoloni' Tanganyika (rejea mihadhara ya UAMSHO na kauli za viongozi kama akina Seif, Jussa, Mzee Moyo, nk);
(b) Walalahoi wa Tanganyika wanataka kujikomboa kutoka katika ‘mfumo wa kifisadi' wa CCM (rejea CDM's M4C); na
(c) Waislamu (wa Tanganyika na Unguja) wanataka kujikomboa kutoka katika makucha ya ‘mfumo-Kristu' ambao umeasisiwa na kudumishwa na CCM chama ambacho kimekuwa madarakani tokea uhuru na ambacho wao wenyewe ni mojawapo ya ngome zake kuu!! (Rejea kauli za akina Sheikh Ponda et al).

Ni harakati ipi ina tija na ipi ambayo saa yake ya kuleta ukombozi imekaribia?
 
Hao uangusho na wenzao hawana tija yoyote zaidi ya kupigia upatu pesa za mabwana zao toka Uarabuni. Hivi ulitegemea warundi kama Ponda wawe na nia njema na Tanzania? Ni kweli Tanzania ina matatizo lakini huwezi kuiita mkoloni wa Zanzibar.

Kwani tuliwaita au walituomba tuwahifadhi baada ya kugundua kuwa kama tusingefanya hivyo sultani angerejea na kuwapindua na kuwachinja. Wanaotaka kuvunja muungano ni mabaki ya waarabu ambayo yanapatikana Pemba. Waswahili halisi hawataki kusikia kuvunjika muungano. Hao wana uangusho weusi unaowaona wamewekwa kinyumba kimawazo na hao wanaojiona washirazi zaidi ya waswahili. Si warejee kwao waone watakavyoitwa watumwa?

Pia Tanzania hakuwezi kuwa na mfumo Kristu iwapo hao waislamu wa uangusho wanaweza kuhubiri upuuzi wao na rais muislam mwenzao akawanyamazi. Mie naona kama kuna mfumo Islam so to speak ingawa yote miwili haitusaidii.

Tulidai uhuru kama Tanzania na si kama wadini au uangusho.
 
Uamsho wao wanahubiri kujitenga tu,bt M4C kuwa pamoja na kudai chetu,so nafikiri M4C ni nzuri sana.
 
Uamsho ni harakati za kijinga/kipumbavu! zinaongozwa na watu wenye akili za mgando.
 
Back
Top Bottom