Hapana, hapana, hapana! Tulipofikia ni hatari...

MWananyati

Senior Member
Feb 3, 2011
160
53
  1. huku madaktari wamegoma
  2. huku daktari kiongozi anatekwa na kuteswa vibaya kiasi cha kutaka kutolewa roho
  3. huku waziri mkuu anasema liwalo na liwe kwa huu mgomo wa madaktari
  4. huku spika anaruhusu mbunge kusema 'kama wapo wenye uchungu na nchi, waende wakazae'

Tunapelekwa wapi na serikali hii?
Rais Kikwete tulijua kuwa utakua mlinzi wetu pindi uingiapo madarakani
Umegeuka uchungu kwa kizazi cha Watanzania
Unashindwa hata kupanua mdomo na kusema 'sitaki hiki'
Unashindwa hata kutumia madaraka yako kusema 'polisi sasa mmezidi'
Unaishia kuwatisha wabunge wa CCM kuwa wasipounga mkono bajeti utalivunja bunge kila mtu afe kivyake
Ulisema utasimamia demokrasia na utawala wa sheria. yapo wapi hayo?
ulisema wewe ni tegemeo la watanzania - sijui ni watanzania gani hao wanaokutegemea

Tuache, tuendelee kufa, ila Yupo Yule atendae haki, sie ambaye Twamtumaini. Ataishikisha adabu hii serikali

Amemlinda dr Ulimboka ili udhalim wa serikali yako uonekane waziwazi


ndio, atatusimamia yeye.

Your days are numbered
Pinda
JK and Co
Soon, not very far
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom