Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Waziri Mkuu ametoa amri kwamba katika kipendi cha miezi miwili serikali yote iwe imehamia Dodoma.
Japokuwa suala la kuhamia Dodoma limekuwa la muda mrefu, lakini kutoa miezi miwili Wizara ziwe zimehama ni kufanya kazi kutumia nguvu ya siasa badala ya lojiki (lack of rational thinking), hasa ukizingatia mambo yafuatayo;
Na cha ajabu, Waziri Mkuu anasema kwamba "hatuchezi mchezo wa siasa hapa, tutapitisha sheria katika Bunge mwezi Septemba kufanya suala la kuhamia Dodoma liwe rasmi" (we are not playing politics here...we will pass legislation in parliament in September to make the move to Dodoma official)
Sasa suala la kujiuliza ni kwamba, kama sheria itafikishwa Bungeni Septemba, siku zote hizi suala la kuhamia Dodoma halikuwa rasmi? Na kama sheria ya kuhamia Dodoma itapelekwa Bungeni Septemba, kwa nini Waziri Mkuu anatoa amri juu ya jambo ambalo bado si rasmi kisheria?
Hivi kwa nini viongozi wetu wanadhani kila jambo linahitaji amri kama za kijeshi ili litekelezwe? Je, kutoa amri bila kufikiria athari za kisosholojia na kiuchumi (socio-economic impacts) sio ubwana ambao tuliupinga kwa muda mrefu sana? Frankly, I was expecting much better from my prime minister than this kind of reckless leadership style.
Ushauri wa bure kwa Waziri Mkuu Majaliwa ni kwamba nguzo na nguvu ya taifa lolote iko katika muungano wa kifamilia. Unapovunja familia unavunja nguvu ya taifa. Huko nyuma empire ya Roma ilivunjika kwa sababu ya mvunjiko wa kifamilia. Kwa hiyo hili suala linahitaji utaratibu mzuri, gradual relocation implementation labda katika kipindi cha mwaka mzima, likifanyika kwa kuhamisha wafanya kazi katika kila wizara kwa awamu kulingana na impact zao katika kuendesha Wizara. Sio kuwaambia watu funga virago ondoka nenda Dodoma haraka. La sivyo utaona barua nyingi za kujiuzuru kazi au hata mivunjiko katika familia. Na watu wa ubalozi je, au umeamua serikali yote itakuwa Dodoma na wao wabaki Dar?
Na vyama vya wafanyakazi iweje viko kimya katika hili?

- kuhamishia serikali Dodoma ni zaidi ya waziri na katibu mkuu (ambao wengi wana nyumba tayari Dodoma) kuhamia Dodoma. Wizara ni watu
- kuhamishia serikali Dodoma inatia ndani kuhamishia ofisi zote za ubalozi kwenda Dodoma (je nao unawapa miezi miwili?)
- kuna suala la kupata majengo na vyumba vya ofisi kwa wafanya kazi
- kuna suala la malipo ya kuhamisha wafanya kazi na vyombo vyao
- kuna suala la kuhamisha furniture, computer za ofisini toka Dar kwenda Dodoma
- kuna suala la kusuka mfumo wa mawasiliano katika ofisi mpya huko Dodoma
- kuna suala la wafanyakazi kupata sehemu za kukaa huko Dodoma
- kuna suala la kutatua mambo yanayohusu familia, kama mke au mume ndie anaehama, au kama mke na mume wote ni wafanya kazi hapa Dar wataathiriwaje na kuhama huku
- kuna suala la watoto wa wafanyakazi hawa walioko mashuleni hapa Dar kuhamia Dodoma
- kuna suala la baadhi ya familia kutatua suala la nyumba zao watakazoziacha Dar
- kuna suala la kuwaandaa watu kisaikolojia kuhusu kuhama badala ya kuwahamisha kama vile tuko kwenye state of emergency
- kuna suala la kuimarisha usafiri wa treni kati ya Dodoma na Dar, ikiwezekana treni za kwenda kasi, kwa kuwa Dar bado itabaki kuwa centre of business na kutakuwa na safari nyingi sana kati ya Dodoma na Dar. Hata viza za kusafiria tutafuata Dodoma. Kufikiria kwamba tutatumia barabara ya Dodoma kama ilivyo ni kuamua kuua watanzania huenda mamia kila mwezi - madereva wetu wa mabasi tunawafahamu - kichaa kapewa rungu. Barabara hii ilishatuulia waziri mkuu, Sokoine.
- nk