Hapa huwa najiuliza ni wapi tunapokosea Watanzania? Uongozi wa aina ipi tunaohitaji kufanya kazi pasipo kushurutishwa?

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
2,011
4,165
Our late president JPM alikuwa Chapakazi sana kwa hili nampongeza sana kwa wakati ule alipopokea kijiti kutoka kwa JK alikimbia sana na wakati kwenye kuinua nchi upande wa nyezo za uchukuzi na kuipa nchi nafasi nyingine ya kuingia mikataba yenye uhai hata hivi leo bado zinaendelea kufanya biashara nyingine za uzalishaji baadhi ya maligafi..

Hapa kwenye hili credits zake nyingi sana Tatizo lilianza tupale alipokuwa na chuki na wanachama wenzie ndani na hata kwa wale wanachama wa vyama vingine pinzani hili swala hili limempotezea sana heshima kama Kiongozi mkuu katika nchi...Huwa nikikumbuka baadhi ya life moments zake kwakweli kuna sauti naiskia ndani ya fikra zangu iki Sema ANAEJIKWEZA HUSHUSWA, WAKWANZA ANAWEZA KUWA MWISHO, MPANDA NGAZI HUSHUKA..

Hakika nilijifunza mengi sana kwenye uongozi wake na pia nilichukizwa na matendo yake mengi sana ila ukichunguza baada ya kuondokewa na aliekuwa Mchapakazi sana kuna wale viongozi waliokua wakitimiza wajibu wao kwa weledi mzuri pamoja idara zote kwa ujumla sasa zimerudi tena kufanya hovyo sana katika nyanja zote za utoaji huduma kwa wananchi wake na jamii kwa ujumla, Hapa huwa najiuliza wapi tunapokosea watanzania au ni aina gani ya kiongozi tunahitaji ili tufanye kazi pasipo kushurutishwa?
 
Our late president JPM alikuwa Chapakazi sana kwa hili nampongeza sana kwa wakati ule alipopokea kijiti kutoka kwa JK alikimbia sana...
Maslahi DUNI ndio shida kubwa katika Nchi hii.

Kama mtumishi anastaafu anapewa 40M halafu mwanasiasa anapewa 200M ndani ya miaka 5 tu, kama ni wewe ungefanya hiyo kazi? NI VILE WENGI WETU TUNA NJAA NA HATUNA JINSI.

Profesa chuo anastaafu anapewa 100M ndani ya miaka 3 tu kwishaaa anaanza kuomba part time.

HATA HIVYO WATUMISHI WA NCHI NI WAVUMILIVU SANA.
 
Back
Top Bottom