Hamza Bendelladj "the smilling hacker"

Sisi huku huwa tunasubiri gunduzi zifanyike tutengenezewe tuje tutumie. Kazi yetu kubwa kufungua screw, bolts na nuts na kuchomelea. Hakuna tafuti zenye mashiko. Nilikuwa na mtaalamu mmoja wa Diesel engines toka U.S.A akinielezea tafiti zinazoendelea kupunguza emmisions ya NOx unapata picha tu huku hatutoboi.
 
Huyo yuko sawa sema tu ubongo wake uko very busy kiasi kwamba kwenda kuoga kwake ni westage of time.
Sku zote watu wenye uwezo mkubwa Sana , huwa hawako balanced, tulipokuwa skul kuna mwamba alikuwa anapiga A za physics na hesabu , na chemistry , jamaa aligonga A , A, A mpak Necta peke yake , ila Maisha yake jamaa kama hayuko Sawa hv , anaweza kaa wiki nzima hajaoga , na yupo rough rough tuu....
 
a

africa yetu
 
Huyo yuko sawa sema tu ubongo wake uko very busy kiasi kwamba kwenda kuoga kwake ni westage of time.
Naskia hata Isack Newton hakuwah kufanya tendo la ndoa, Aristotle naye alikuwa anatembea bila viatu , mi nahs huwa kuna vitu vinapungua ili kujalizia pengine , thus why kuna sehemu wanafanya mambo ambayo mtu wa kawaida hawezi
 
Kuna mwanasayansi mwingine anaitwa Peter Cavendish ni mtaalamu aligundua gravitational constant,G.
Katika umri wake wote hajawahi kumjua mwanamke na watu walikuwa hawamjui kitaani kwake
Naskia hata Isack Newton hakuwah kufanya tendo la ndoa, Aristotle naye alikuwa anatembea bila viatu , mi nahs huwa kuna vitu vinapungua ili kujalizia pengine , thus why kuna sehemu wanafanya mambo ambayo mtu wa kawaida hawezi
 
Anaitwa hamza Bendelladj alizaliwa 1988 nchini algeria

Huyu anajulikana kama miongini mwa mahacker wakubwa alifanikiwa kudukua akaunti za benki nyingi duniani na kuiba fedha zenye thamani zaid ya Trillion 1

Na pesa zote hizo alizitumia kuwapa watu wenye kipato cha chini alitoa misaaada sehemu nyingi zaidi palestina na africa.

Ulikuwa mchezo endelevu mpaka pale alipotangazwa na serikali ya marekani kuwa ni mdukuaji anayehitajika zaidi.

Alikamatwa na kufungwa huko marekani na muda wote alionekana akitabasamu.

Hamza alikuwa anajua lugha tano tofauti duniani na inasemekana alinyongwa hadharani lakini baadhi ya taarifa zinakanusha taarifa View attachment 1629690View attachment 1629691tunajifunza nini??
Watu wema hawatakiwi duniani....dunia inataka watu kama Trump.
 
Sku zote watu wenye uwezo mkubwa Sana , huwa hawako balanced, tulipokuwa skul kuna mwamba alikuwa anapiga A za physics na hesabu , na chemistry , jamaa aligonga A , A, A mpak Necta peke yake , ila Maisha yake jamaa kama hayuko Sawa hv , anaweza kaa wiki nzima hajaoga , na yupo rough rough tuu....
hahaha mkuu umetisha sanaa, huwa pia wanasema watu welaiokua vizuri darasani hawafanyi vizuri sana kwenye maisha kiuchumi...ila sina fact sanaa
 
Anaitwa hamza Bendelladj alizaliwa 1988 nchini algeria

Huyu anajulikana kama miongini mwa mahacker wakubwa alifanikiwa kudukua akaunti za benki nyingi duniani na kuiba fedha zenye thamani zaid ya Trillion 1

Na pesa zote hizo alizitumia kuwapa watu wenye kipato cha chini alitoa misaaada sehemu nyingi zaidi palestina na africa.

Ulikuwa mchezo endelevu mpaka pale alipotangazwa na serikali ya marekani kuwa ni mdukuaji anayehitajika zaidi.

Alikamatwa na kufungwa huko marekani na muda wote alionekana akitabasamu.

Hamza alikuwa anajua lugha tano tofauti duniani na inasemekana alinyongwa hadharani lakini baadhi ya taarifa zinakanusha taarifa View attachment 1629690View attachment 1629691tunajifunza nini??
Hamza hakunyongwa hizi picha ni photoshoped, hakuna sheria ya kunyonga wadukuaji. Alifungwa tu na baadae kesi yake ikawa siri. Kwanza Marekani hawanyongi hadharani kwa kuwapiga watu vitanzi kama Iran wakaning'iniza kwenye crane.
 
🤔🤔🤔
 
Ma genius wote lazima ukute ana disorder, sijui ndo husababisha kuwa na akili zaidi ya normal na maisha yao huwa ni ya ajabu ajabu sana hasa wa Tanzania mfano, Dr luis shika kid
 
0fd8e369bd0a48fbb1852d5f6bf90a00_18

"Siku ya tarehe isiyojulikana, lakini inaweza kuwa tarehe 21-02-2011 mpaka tarehe 24-02-2011 , tarehe kamili haifamiki na mahakama ya Grand Jurry katika wilaya ya Georgia and sehemu nyingine, Mtuhumiwa HAMZA BENDELLADJ aka Bx1 alisaidiana na kusababisha na wenzake wanaojulikana na wasiojulikana na Mahakama, kwa akili zake timamu na kwa hiari yake alidukua kompyuta bila kuruhusiwa na akapata taarifa kutoka kwenye kumpyuta inayolindwa kwa lengo la kujinufaisha kiuchumi"-Maneno hayo yakisema na hakimu mahakama ya Georgia chini ya Sally Quillian Yates

Mwishoni hukumu inatoka baada ya HAMZA BENDELLADJ kuwa na makosa 14 yaliyomtia hatiani huku akihukumiwa miaka 15 jela pamoja na mshirika wake aliyejulikana kwa jina la Aleksander Andreevich Panin aka Gribodemon kuhukumiwa miaka tisa jela.

JE HAMZA BENDELLADJ NI NANI?

1b33c319000005dc-3497928-image-a-83_1458257525323

Siku ya Ijumaa ya tarehe 3 June 1988 katika eneo la Tizi Ouzou, Kouba, nchini Algeria ndio DANIEL HAMZA BENDELLADJ elimu yake alisomea katika nchi yake ya Algeria na alikuwa na Stashahda ya Uhandisi wa Kompyuta, Lakini katika kuhitimu Stashahada yake aliwahi kufanya kazi ya Kompyuta maintainance kwa muda wa miaka mitatu. Jina lake la Code ni Bx1, pia waandishi wa habari walimpa jina la Smilling hacker kwa kuwa muda wote anatabasamu japokuwa alikuwa chini ya polisi.

Hamza alikuwa na mke pamoja na mtoto mmoja lakini haijulikani wanaishi wapi.

Baada ya kutoka kufanya kazi kama computer maintainance baadae Hamza alianza kazi ya kudukua (hack) kompyuta za mabenki mbalimbali na kuiba pesa za kusafirisha kwenye akaunti yake, Aliwezeje kufanya hivyo?

Hamza alitengeneza Trojan Horse Virus, ambapo alikuwa anaingia kwenye kompuyta yoyote ile na kuiba taarifa za watumiaji (username & password) baadae alikuwa na system ya ATS(Automated Transfer System-along Zues trojan) ambayo kazi yake ni kuhamisha pesa automatically mara moja tu atakapo ingia (account login).

Inahamika kuwa alifanikiwa kudukua benk na taasisi nyingine za kifedha jumla 217 na aliiba zaidi ya dola million mia tatu, lakini katika akaunti yake alikutwa na dola million kumi. Pia Hamza alikuwa ni moja ya unethical hacker (wadukuzi wasio na maadili) ambayo orodha ilitolewa na MICROSOFT kuwapa polisi wa Marekani.

MAISHA YA HAMZA
Hamza alikuwa anaishi katika Grand hotels lakini pia alikuwa anaishi maisha ya kifahari ambapo alikuwa anasafiri na ndege siti za first class. Baada ya kuanza kutafutwa na maaskari wa kimarekani Hamza alikuwa kila siku anafanya kazi ya kubadili IMEI namba ya simu yake aina ya Iphone na kubakia anonymous.

Hamza alikutana na rafiki yake mwenye asili ya kirusi Aleksander Andreevich Panin kwa kushirikiana wakatengeneza software iliyojulikana kama SPYEYE ambayo ilikuwa inaiba pesa, Pia alikuwa anawauzia wadukuzi (hackers) wengine na ilikuwa inatiumika kama BOTNET.

Nini BOTNET? Kwa lugha ya kompyuta bot maana kifupi cha ROBOT na net ni NETWORK kwahiyo botnet ni mtandao wa maroboti ambao unaunga idadi ya watu mfano kumi halafu wanakuwa controlled na server/computer moja.
Kirusi hiki cha SPYEYE inahaminika kilidukua na kuathiri zaidi ya kompyuta million hamsini. Lakini mpaka leo hii software ipo katika black market inauzwa kwa dola elfu kumi.

Kwa pamoja Hamza na rafiki yake Panin walikuwa na kundi la chini (underground group) ambalo ni kikundi cha hackers ambao ni unethical inaitwa Darkode.com, pia wawili hawa walijulikana kama legend katika dark world (rejea hapa kuhusu dark world).

PESA ZA HAMZA ZIKO WAPI?
Hamza aliiba taasisi karibu 217 lakini alikuwa na utajiri wa dola million kumi, pesa nyingi alikuwa anaopeleka Algeria, sehemu yenye vita Syria, Palestina nk kwahiyo yeye chache tu ndio alikuwa anatumia kati ya nyingi alizoiba..

KUKAMATWA KWA HAMZA

hacker-algc3a9rien-hamza-bendelladj-jpg

Hamza alikamatwa nchini Thailand katika uwanja wa ndege wa SUVARNABHUMI ambapo alikuwa na safari ya kutoka Malaysia kwenda Algeria, ambapo makubaliano kati ya Marekani na Thailand yalifanyika na kumpeleka Hamza mpaka nchini Marekani, ilikuwa vipi mpaka jamaa kukamatwa? Kuna ajenti wa alijifanya yeye ni underground hacker kwahiyo anataka kununua SPYEYE ndio alikuwa anaweza kuongea na Hamza na alifanikisha kukamatwa kwa Hamza.

Panin pia alikamatwa mwaka 2013 katika uwanja wa ndege wa Georgia International Airpot na wote kwa pamoja wakakutwa wapo chini ya polisi.

Baada ya kukamatwa HAMZA baadhi ya watu ambao wanamsapoti wali-hack website ya Air France pamoja na ile ya Virginia University, wakiwa wanashinikiza kuwa Hamza aachiwe huru, na katika mitandao ya kijamii kulikuwa na hashtag kama Freepalestine na ile ya FreeHamzaBendelladj, na vyuo vya nchini Algeria wanampongeza na kumsapoti huku wakimchukulia kama shujaa wao.

HAMZA AMENYONGWA?

Crist%25C3%25A2o

Hukumu ilikuwa inaonyesha kuwa Hamza ataenda jela kwa muda wa miaka 15, lakini baadae ukaja uvumi kuwa Hamza kanyongwa, Lakini balozi wa Marekani nchini Algeria alikanusha madai hayo na kusema kuwa kuna adhabu ya capital kwa kosa kama hilo kutokana na sheria za Marekani.
Yuko vizuri
 
Huyo mchizi anaweza kupiga hesabu kichwani muda unaotumika kuoga, hata kwa style ya Hugo Chavez (kuoga mwisho dakika 3 tu), halafu akaona muda unaofaa kabisa kuoga na kubalance shughuli zingine kwa ufanisi kabisa ni kuoga mara moja kwa mwezi.

Halafu kila anapopanga kuoga hiyo mara moja kwa mwezi, anasahau kwa sababu mambo muhimu zaidi yanajitokeza.

Yani mtu ana solve equation ya kuzuia asteroid la kuangamiza dunia nzima.

Yupo 95% katika solution.

Halafu hapo ndipo muda wa kuoga unapoangukia.

Lazima asahau kuoga!
 
Hamza Bendelladj - Smiling Hacker

Alikuwa kwenye orodha ya wadukuzi 10 bora wanaosakwa zaidi na Interpol na FBI.

Huenda hata wewe alishakuibia hela bila kujua

Mwaka 2010 huyu jamaa alifanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa na mtu yoyote.

Mwaka 2010 pale New York, USA Hamza alikuwa akiishi na Mama yake, maisha hayakuwa poa sana, Hamza alikutana na rafiki yake Aleksandr Andreivich, wakaamua kupanga tukio ili wapate pesa

Ooh yes tukio likatiki, waliweza ku-hack Banks 217 na jumla ya 60 million bank accounts.

Banks 217 kutoka nchi tofauti tofauti duniani, chukulia Bank Accounts Million 60

Ndani ya miezi kadhaa walipata $4 Billion, (Badili kwenda Tzs ) chakushangaza hawa jamaa walitoa zaidi ya dola milioni 280 kwa mashirika ya misaada barani Afrika na Palestina.

Hamza alizaliwa Mwaka 1988 huko Algeria-Africa na alikulia Africa ila baadae wakahamia USA, rafiki yake Aleksandr ni raia wa Russia.

WALITUMIA NINI KUIBA

Ooh hawa jamaa walikuwa ni Computer Programmers walikubaliana kutengeneza Software inaitwa "SpyEYE"

SpyEye ni Malware Software Botnet, kwa lugha rahisi ni VIRUS ambayo inaiba taarifa zote za kibenki (Password, user ID codes), na kufanya miamala kutoka Account moja kwenda nyingine

Baada ya kufanya wizi huo waliuza hiyo SpyEye Program kwa Hackers wengine huko US.

Baada ya miaka 3 ya msako wa FBI na Interpol, mwaka 2013 Hamza alikamatwa huko Thailand airport na aliitwa Smilling hacker kutokana na Tabasamu lake kwenye kila picha aliyopigwa baada ya kukamatwa

Alihukumiwa kifungo cha Miaka 15 jela kwa wizi wa $4Billion

KIKUBWA UHAI

IMG_20220221_070319.jpg
IMG_20220221_070315.jpg
 
Back
Top Bottom