Hamas: kumekucha Viongozi wetu wapo majumbani mwao, na si mahospitalini.
Wanapanga mikakati ya kuwamaliza Israel.Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema madai ya utawala wa Kizayuni kwamba viongozi wa harakati hiyo wapo katika njia za chini ya ardhi ya hospitali ya Al -Shifa katika Ukanda wa Ghaza ni ya upotoshaji.
Msemaji wa jeshi la utawala ghasibu wa Kizayuni amedai kuwa viongozi wa Hamas wapo katika njia za chini ya chini ya ardhi ya hospitali ya Al Shifa huko Ghaza.
Msemaji wa Hamas amejibu madai hayo ya utawala wa Kizayuni kwamba viongozi wa Hamas wapo katika njia za chini ya ardhi katika hospitali huko Ghaza kwa kusisitiza kuwa: Adui Mzayuni kwa kutoa madai haya anajaribu kuinua ari ya jeshi lake kwa kutoa simulizi hizo za uwongo.
Msemaji wa Hamas ameongeza kusema kuwa: Madai haya ni ya upotoshaji na ya uwongo. Viongozi wote wa Hamas wapo maumbani mwao na si mahospitalini. Msemaji wa Hamas amebainisha kuwa: Utawala ghasibu wa Kizayuni unawashambulia kwa mabomu watoto na wanawake, na muqawama unaendelea kuongoza vita kwa nguvu zote.
Afisa huyo wa Palestina ameongeza kuwa: Jeshi la Kizayuni linashambulia miundombinu ya Ukanda wa Ghaza khususan nyumba na hospitali.
Inaonekana kuwa utawala wa Kizayuni kwa kutoa madai haya yasiyo na msingi unataka kukariri jinai ya al-Maamadani katika hospitali ya Al-Shifa.
Tarehe 17 Oktoba Wapalestina zaidi ya 500 waliuawa shahidi katika shambulio la bomu la utawala wa Kizayuni katika hospitali ya Al-Maamadani huko Ghaza; ambapo kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo vya habari, idadi ya watu waliouawa inafika 1,000.