Hamad Rashid kuanzisha chama kipya!

HR ni mwanasiasa, mwacheni afanye siasa. Kumuita mroho wa madaraka ni kumkosea heshima, yeye anafanya siasa....madaraka ndio matunda yake. CUF imekufa, mwacheni aibue harakati zingine mpya Zanzibar.

Namuunga mkono.
 
Aliyekuwa mbunge wa Wawi ambaye jana amevuliwa uanachama wa CUF, Mh. Hamad Rashid Mohamed, ametangaza wazi kwamba anaanzisha chama kipya na amewataka wanachama wa CUF kurudisha kadi zao, na kwamba wawe tayari kujiunga na chama chake kipya kinachokuja muda si mrefu !

Source: Mlimani TV, Elimu Kwanza

Kwa tunaomfahamu Hamad Rashid. hana uwezo huo kwani kwa tuliowahi kufanya nae kazi tunajuwa kabisa yeye ni mtendaji zaidi na sio mwanasiasa.

Ok, yetu macho. Naona atakuwa mwelekeo ule ule wa Bi Naila Majid Jidawi.

 
Paukwa PAKAWA,UKISTAJABU YA MUSSA UTAONA YA FILAUNI.Hii ndio demokrasi ya Kiafrika unadhani Afrika ingekuwa na Demokrasia Mugabe ,Museveni na taipu zao tungeshawasahau.Mungu ilaani Africa.
 
Haya yote yanakuja kwa kuwa Hamad Rashid kukosa kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, kweli madaraka matamu, maadamu huna tena zile stahiki ulizokuwa unazipata ndio yote haya.

Pole Hamad ndio hautasikika tena zaidi ya kuwa mbunge wa mahakama mpaka 2015 utakapozikwa rasmi kwani huko Wete wanahiitaji CUF, kuliko unavyohitajika kama Hamad Rashid. Kama unakumbuka walikumwaga katika kura za maoni lakini maalim Seif akakubeba.
 
.......mkuu Tindikali ni kweli, huyu jamaa aanze kujilaumu yeye binafsi kwanza, then atafute mchawi (kama yupo maana mimi naamini mchawi ni yeye mwenyewe), nasema hivi kwa maana alianzia chokochoko bungeni alipopoteza nafasi ya uongozi wa kambi ya upinzani, akashindwa, sasa akataka ukatibu mkuu wa CUF (naamini ameshindwa), katika hali ya kawaida ni binadamu wachache sana wanaoweza kuvumilia kile alichokuwa anafanya HR ndani ya CUF; yeye bila kuongoza hana raha, basi aanzishe chama chake awe kiongozi, wala asikimbilie mahakamani kwa sababu anapoteza muda wake
jamaa ananikera huyu, ye anadhani kaja duniani kuongoza wengine tu?
 
Hii itakuwa move nzuri kwa CDM kama lowasa ataachana na magambaz na kuunda chama kingine ambacho kitawahusisha hawa waliofukuzwa kwenye vyama vyao.
Inafahamika lowasa anawafuasi wengi ndani ya ccm kitu ambacho kitaiyumbisha na kuijenga cdm maradufu na ndio maana mpaka leo dhana ya kujivua gamba ime prove failure.
 
HR needs to assess his options carefully and play his cards pretty well la sivyo atakuwa amefulia moja kwa moja katika medani ya siasa; akianzisha chama kingine cha siasa, atakuwa anagawa kura za pemba na kupunguza nguvu ya CUF - this will play very well in CCM's favour, so anaweza asiwekewe mizengwe ya usajili kama ilivyokuwa kwa CCJ; akienda mahakamani, anaweza kupoteza muda mwingi sana na hakuna guarantee kwamba atapata haki anayotarajia
 
sijaona mnazungumzia uhalali wa amri ya mahakama kuu bara kutumika zanzibar. kule ni jurisdiction nyingine

na kuna mahakama kuu kule hiyo amri ya mahakama KUU BARA haiwezi kua binding kwa zanzibar.ninachojua amri ya mahakama ya Rufaa ndio peke yake inatumika kote kote na sio mahakama kuu ya bara since kikao kilikaa zanzibar. kwa hivo mkutano wa CUF ULIKUWA NA KILA SABABU YA KUENDELEA NA KIKAO CHAO KWANI HIYO AMRI HAIWEZI KUWA ZUIO KWAO n HATA WAOMBAJI WA ZUIO WALIJUA MKUTANO UNAFANYIKA ZANZIBAR WALIPASWA KUOMBA ZUIO KTK MAHAKAMA KUU ZANZIBAR.

Ameshangaa kuona amri ya mahakama ikivunjwa na kikao kilichokuwa na Makamu wa Rais pamoja na watu wengine ambao ni wanasheria. Mnamo saa tatu na nusu mahakama jijini Dar iliamuru kusimamishwa kwa kikao hicho, lakini maofisa makao makuu ya CUF Dar wakakataa kupokea barua kutoka kwa karani wa mahakama. Mwanasheria wake (Hamad) akaamua kumtumia Hamad amri ya mahakama kwa njia ya e-mail huko Zanzibar kilipokuwa kikifanyika kikao cha Baraza Kuu, na Hamad akaiprint na kumpatia Katibu Mkuu (Maalim Seif), lakini either Seif hakuitoa/kutangaza kwenye kikao au alitangaza ikapuuzwa kikao kikaendelea. Kabla ya watuhumiwa wote 14 kumalizika kuhojiwa, maamuzi ya yakatolewa chap chap dhidi ya watuhumiwa wachache (nadhani wanne) ili walau ijulikane Hamad amefukuzwa, halafu ndio wengine waliobaki wakaendelea kuhojiwa !!

Hayo ni matamshi ya Hamad alipokuwa akiongea kwa simu LIVE pale mlimani TV asubuhi hii
 
sijaona mnazungumzia uhalali wa amri ya mahakama kuu bara kutumika zanzibar. kule ni jurisdiction nyingine

na kuna mahakama kuu kule hiyo amri ya mahakama KUU BARA haiwezi kua binding kwa zanzibar.ninachojua amri ya mahakama ya Rufaa ndio peke yake inatumika kote kote na sio mahakama kuu ya bara since kikao kilikaa zanzibar. kwa hivo mkutano wa CUF ULIKUWA NA KILA SABABU YA KUENDELEA NA KIKAO CHAO KWANI HIYO AMRI HAIWEZI KUWA ZUIO KWAO n HATA WAOMBAJI WA ZUIO WALIJUA MKUTANO UNAFANYIKA ZANZIBAR WALIPASWA KUOMBA ZUIO KTK MAHAKAMA KUU ZANZIBAR.

Na cha kushangaza zaidi aliweka pingamizi na yeye alikuwa humo humo katika kikao alichokipinga.

maajabu hayo.

Mh hamad Rashid ameingizwa choo cha kike

 
aanzishe chama ili zanzibar wawe na chama cha upinzani cuf ni ccm tu
 
Mwehu huyo! Ana uroho wa madaraka. Alishawahi kuwa waziri mambo ya ndani,mkewe anaroho mbayaa! Eti shamba boi au mfanyakazi wa nje akiomba maji ile glass alonywea anaivunja kwa madai imenywewa na kafiri! Ovyoo!

ya kweli haya?
 
Back
Top Bottom