Hamad Rashid kuanzisha chama kipya!

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,684
20,440
Aliyekuwa mbunge wa Wawi ambaye jana amevuliwa uanachama wa CUF, Mh. Hamad Rashid Mohamed, ametangaza wazi kwamba anaanzisha chama kipya na amewataka wanachama wa CUF kurudisha kadi zao, na kwamba wawe tayari kujiunga na chama chake kipya kinachokuja muda si mrefu !

Source: Mlimani TV, Elimu Kwanza
 
Wapinzani watamalizana na kuzikana wenyewe kwa wenyewe. Anyway kikianzishwa chama kingine yanaweza kuwa yametimia aliyoyasema mwandishi MAYAGE! yetu masikio.
 
Uroho wa Madaraka utawamaliza viongozi wa upinzani pamoja na vyama vyao. Wanajali tu maslahi yao binafsi
 
mimi ntakua wa kwanza,nasubiri kupata taarifa rasmi,hiki kinaweza kuwa chama cha kidemokrasia cha kweli maana hamad rashid kutokana na sakata hili atakua amekomaa hatothubutu kuwa mbakaji wa demokrasia ndani ya chama na ntamueleza wazi sio lazima awe mwenyekiti yeye,baada ya kupata usajili aitishe uchaguzi wa ndani haraka na kila mwanachama awe huru kugombea,ntamsaidia kukifanya kiwe chama cha kupigiwa mfano kwa ukomavu wa demokrasia ya ndani ya chama...
 
kaul yake alisema ataanzisha chama,
unadhan kuna Demokrasia,wakat ataanzisha?
 
kaul yake alisema ataanzisha chama,
unadhan kuna Demokrasia,wakat ataanzisha?

Hiyo nilimchallenge hapa na personal pia,nikamshauri aachane nayo na wengi kama mimi ambao ni waumini wa demokrasia hatujaona chama kilicho democratic kiukweli na tunakisubiri tunaomba kianzie kwenu,akanielewa ni mtu msikivu sana.
 
Ameshangaa kuona amri ya mahakama ikivunjwa na kikao kilichokuwa na Makamu wa Rais pamoja na watu wengine ambao ni wanasheria. Mnamo saa tatu na nusu mahakama jijini Dar iliamuru kusimamishwa kwa kikao hicho, lakini maofisa makao makuu ya CUF Dar wakakataa kupokea barua kutoka kwa karani wa mahakama. Mwanasheria wake (Hamad) akaamua kumtumia Hamad amri ya mahakama kwa njia ya e-mail huko Zanzibar kilipokuwa kikifanyika kikao cha Baraza Kuu, na Hamad akaiprint na kumpatia Katibu Mkuu (Maalim Seif), lakini either Seif hakuitoa/kutangaza kwenye kikao au alitangaza ikapuuzwa kikao kikaendelea. Kabla ya watuhumiwa wote 14 kumalizika kuhojiwa, maamuzi ya yakatolewa chap chap dhidi ya watuhumiwa wachache (nadhani wanne) ili walau ijulikane Hamad amefukuzwa, halafu ndio wengine waliobaki wakaendelea kuhojiwa !!

Hayo ni matamshi ya Hamad alipokuwa akiongea kwa simu LIVE pale mlimani TV asubuhi hii
 
Aanzisha chama ua anapanga kuanzisha chama ?
Ni yale yale tu. Mtu anapowaambia wafuasi wake na wa CUF kwa ujumla warudishe kadi zao kwa kuwa chama kipya kinakuja, huoni hapo tayari mchakato umeanza?
 
Mwehu huyo! Ana uroho wa madaraka. Alishawahi kuwa waziri mambo ya ndani,mkewe anaroho mbayaa! Eti shamba boi au mfanyakazi wa nje akiomba maji ile glass alonywea anaivunja kwa madai imenywewa na kafiri! Ovyoo!
 
Aliyekuwa mbunge wa Wawi ambaye jana amevuliwa uanachama wa CUF, Mh. Hamad Rashid Mohamed, ametangaza wazi kwamba anaanzisha chama kipya na amewataka wanachama wa CUF kurudisha kadi zao, na kwamba wawe tayari kujiunga na chama chake kipya kinachokuja muda si mrefu !

Source: Mlimani TV, Elimu Kwanza

mpaka anaingia kaburini hicho chama hakitasajiliwa.:yawn:
 
Maalim seif anajua kabisa kuwa HR ataruhusiwa na mahakama kuendelea kuwa mbunge. Lengo lake ni HR akose mdomo wa kusemea kwenye chama na miguu ya kutembea akiwa mwana chama. so HR atabaki kuwa mbunge wa mahakama huku akiwa si chochote kwenye chama, na malengo ya HR kuwa katibu mkuu yameishia jana
 
Back
Top Bottom