Halotel ni kiboko kwa internet speed

ukitaka kupata internet ya tigo vizuri lazima unapokaa pawe na mwinuko kidogo itakayokuwezesha kupata mawimbi vizuri,Mimi nakaa mbagala,mahala nilipokuwa naa mwanzo kulikuwa ni uswazi halafu kupo kama chini hivi na internet ya tigo ilikuwa ni mtihani kwa kwel ila tangu nihamishe makazi lakini ni huku huku mbagala ila kuna kamwinuko kidogo nimesahau kutumia zantel mana haifikii tigo kwa speed ndomana nasema hvyo
 
Kesho ntapita ofisi zao pale Posta. Nimeona watu wengi wako Halotel sasa hivi. Airtel, Voda na Tigo watasubiri sana
 
Hizo bundle za halotel na price zake zimekaaje kwa anayejua?
1e202764bf2b28cca8714bffaa0760fa.jpg
 
Kwa hapa kimara ninakoishi aisee halotel Inakera. Internet kila muda ni E tu siifaidi kabisa kila niwapo nyumbani
 
Kuna wengine ni mawakala wa hii mitandao mibovu hawataki appreciate Halotel.hata kama hutaki kuwakubali Halotel cc tunaenjoy huku hiyo mitandao ya zamani tumeshaisahau zamani.
 
Halotel hawana mpinzani,


Lakini ikishafika saa tano usiku kuna baadhi ua vitu kama kucheza video online na kucheki mechi inazingua,lakini huwezi fananisha na mtandao wowote tanzania
 
Helotel ni kiboko ya mitandao yote. Hamieni huko. Tigo 4G ni kimeo wala haifai. Wanazuga watu tu
 
Hawa jamaa wakileta 4g si ndo itakuwa balaaa
Uh, mimi nipo hapa kimara, dsm mitaa ya kuelekea bonyokwa, lkn network yao inasoma edge 'E'. Hii siyo mara ya kwanza naiona ila imekuwa hivyo tangu kitambo tu. Lakini nikiwa nje kidogo ya kimara network huwa ni H+ mara nyingi. Sasa sijui huku kimara kuna shida gani? Customer care tuambieni kulikoni huku kwetu?
 
Kwa hapa kimara ninakoishi aisee halotel Inakera. Internet kila muda ni E tu siifaidi kabisa kila niwapo nyumbani
kimara sehemu gani, mi naishi mbezi mwisho ila nikiwa naenda posta all the way ni h+
 
Natumia tigo LTE lakini haina tofauti na 3G ipo slow sana mchana na jioni.. Usiku sana alfajiri ndio i akuwa na speed kidogo.. Itabidi nijaribu halotell
Tigo LTE ni uongo mtupu. Utakuta line inasoma 3G na iko slow kuliko. Mpango mzima ni Halotel. Sijui walikuwa wapi siku zote mpaka tukaibiwa na makampuni mengine
 
Back
Top Bottom