Halmashauri za miji na wilaya zaongoza kwa mishahara mizuri

Makupa

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
5,032
2,554
Wakuu inaaminika ya kwamba watanzania wanaofanya kazi kwenye halmashauri zetu za miji na wilaya ndio wanaolipwa vizuri ukilinganisha na taasisi nyingine za serikali.

Kutokana na malipo kuwa mazuri ni vigumu sana kusikia kutoka kwa mfanyakazi wa halmashauri kuwa anatafuta kazi sehemu nyingine. Je kwa nini taasisi nyingine za serikali zisiige halmashauri zetu?
 
workshop fake nyingi na wizi mwingine na si mishahara. huko before CAG walikuwa wanafaidi lakini kwa sasa wamekoma japo wengi hawaogopi bado.
 
Mleta post hii ni mchokozi! Unataka kufunua miradi hewa na marupurupi hewa ya kule eeh!?
 
Naona wachangiaji sio watuumishi wa halmashauri maarufu serikali za mitaa. Mi ni mwajiriwa wa SM. huku mishahara mizuri asikweleze mtu. Wengi wanahamia toka mashirika na serikali kuu. Kwetu kuzuri!
 
mshahara mzuri labda kama ni mtumishi wa muda mrefu sana c chini ya miaka 15,ila kwa freshers,ni maumivu tu na usiombe kama ukiwa idara isiyokuwa na michongo mingine ya mkwanja,utaliaa ukwasi
 
Mishahara ya watumishi wa halmashauri, watumishi wa wizara na watumishi wa ofisi za wakuu wa mikoa wanapata mishahara inayolingani kulingana na vyeo vyao kuanzia ambazo ni TGOS A,B,C kwa watumishi wa opershen service na TGS A,B,C,D na kuendelea kwa hiyo si kweli kwamba watumishi wa halmashauri wanapata mishahara mikubwa kuliko watumishi wa hidara nyingine za serikli.

Kiukweli watumishi wa serikali wanaopokea mishahara mikubwa n wale wa mashirika ya umma au wakala ambao mishahara yao inatofautiana kila idara kadri ambavyo mrajisi haizna na katibu mkuu utumishi wanavyopitisha viwango vya mishahara kwa hizo idara. Navyofahamu mimi watumishi wa taasisi za BOT,TRA,TANAPA,TPDC nk ndio wanapata mishahara mikubwa kuliko watumishi wengine hususani wa halmashauri na wizara.

Ukweli ni kwamba watumishi wengi wa halmashauri ni wabadhilifu sana wa fedha ndio maana hata ktk repoti ya CAG ofisi za halamashauri ndizo zinaongoza za kwa hati chafu. Na kwa taarifa ya muanzisha thread tutaona watumishi wengi wa halmashauri wanapelekwa mahakamani na PCCB kutokana na ubadhirifu wa fedha za umma
 
Ni wizi mtupu huo na si mishahara kuwa mikubwa kuliko taasisi zingine kama Bot, Tra, taccra, euwra,Tanroad, bandari na maeneo mengine
 
TGS D hizi hizi au zimembadilika,miye niko huku Machochwe,Mtendaji wa Kata mbona sijaona huo mshahara mzuri au ni kwa wale walio Makao Makuu ya Halmshauri?
 
TGS D hizi hizi au zimembadilika,miye niko huku Machochwe,Mtendaji wa Kata mbona sijaona huo mshahara mzuri au ni kwa wale walio Makao Makuu ya Halmshauri?
Sema ukweli bwana, kesi zisizo na kichwa na kuwaweka watu ndani hadi mpate kwanja wa kujaa mifuko miwili ! Na katika Halmashauri, kuhamisha mamilioni kutoka akaunti ya maendeleo kwenda akaunti binafsi ! PCB na CAG kugeuza halmashauri shamba la bibi! :smow:
 
Back
Top Bottom