Halima Mdee: Mwenendo wa hali ya Uchumi na majibu dhaifu ya Serikali

Zeni2017

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
1,247
532
Kwa wenzetu topiki za aina hii hujadiliwa kwenye vyombo vya habari na wasemaji kutoka vyama vyote na hata wasio na vyama.

Kumuachia msemaji wa chama kimoja aseme halafu anataka msemaji wa serikali ajibu ndio mwanzo wa vurugu. Yaani hapo nimebaki hoi. Mtu kajiita waziri kivuli. Anawashukuru vyombo vya habari kumfikishia ujumbe. Sasa hiki ni kikao cha bunge, ni kampeni ya uchaguzi au ni kitimutimu cha upinzani na serikali?

CNN, MSNBC, FOX, na wengineo hawaishiwi habari kwa sababu topiki za namna hii wanazirusha na wanapata maoni ya wasemaji bila ya vurugu za kitaifa.

Mambo mengine ya Tanzania ni ya Tanzania. Sijawahi kusikia popote duniani waziri kivuli akihutubia taifa.

=======


CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MWENENDO WA HALI YA UCHUMI NA MAJIBU DHAIFU YA MSEMAJI WA SERIKALI
___________________________________
Ndugu Waandishi wa Habari;

Leo tumewaita hapa pamoja na mambo mengine ni kuendelea kusisitiza kauli yetu juu ya hali mbaya ya uchumi wa taifa letu tangu serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli iingie madarakani mwishoni mwa mwaka 2015.

Vilevile tutazijibu hoja za msemaji wa serikali hoja kwa hoja ili kuweka kumbukumbu sawa na tunawataka watanzania wapime nani mkweli na nani ni wa kupuuzwa katika jambo hili.Aidha tunaitaka serikali ijibu hoja zetu ambazo zimetokana na taarifa za BOT kuwa uchumi wetu unayumba au kuporomoka ukilinganisha na miaka ya nyuma.

MAJIBU JUU YA HOJA ZA SERIKALI NI KAMA IFUATAVYO;

#01. Kwamba uchumi wa Dunia umepata mtanziko na kuwa kufikia April,2016 umekuwa kwa asilimia 3.1 ikilinganishwa na asilimia 3.5 mwaka 2015.

JIBU:

Msemaji wa serikali ameandika takwimu za uongo hasa anaposema kuwa uchumi wa Dunia ulikuwa kwa asilimia 3.5 mwaka 2015 na akiwa amenukuu taarifa ya Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania.

Kwa mujibu wa tamko la sera ya fedha 2016/17 lililotolewa na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania ,Februari 2017, ambalo lilitathimini mwenendo wa utekelezaji wa Sera ya Fedha katika kipindi cha nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2016/17 ilieleza kuhusu mwenendo wa uchumi wa Dunia.

“………..Uchumi wa Dunia ulikuwa kwa wastani wa asilimia 3.1 mwaka 2016, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.2 mwaka 2015” (uk 05)
Msemaji wa serikali alitoa wapi takwimu za ukuaji wa asilimia 3.5 za mwaka 2015 ?

#02 Kwamba mfumuko wa bei uliongezeka katika nchi za Marekani,Japan na Uingereza.

JIBU: Ni kweli kuwa kulingana na taarifa za mwelekeo wa hali ya kiuchumi wa dunia iliyotolewa na IMF Januari , 2017 ilionyesha kuwa mfumuko wa bei katika nchi zilizoendelea ulitarajiwa kuongezeka na kufikia wastani wa asilimia 1.7 mwaka 2017.

Aidha taarifa hiyo ya IMF ilionyesha kuwa wastani wa mfumuko wa bei katika nchi zinazoibukia kiuchumi na zile zinazoendelea unatarajiwa kubakia katika wastani wa asilimia 4.5 mwaka 2017.

Tunamuuliza msemaji wa serikali Tanzania hapo iko kwenye kundi lipi maana kwenye mfumuko wa bei tulikuwa asilimia 5.4 kwa hiyo hatupo miongoni mwa zile nchi zinazoibukia wala zinazoendelea kwani zenyewe mfumuko wa bei ni asilimia 4.5 kwa mujibu wa IMF.

#03 Kwamba Makusanyo yameongezeka kutoka wastani wa TZS BILIONI 925 kwa mwaka 2015 hadi TZS TRILIONI 1.069 kwa mwaka.

JIBU : Ni kweli kuwa kwa mujibu wa Takwimu za TRA makusanyo ya kodi yameongezeka kwa kiwango ambacho serikali inatangaza , hili ni ongezeko la TZS BILIONI 144 kwa mwezi.

Ongezeko hili limefikiwa baada ya serikali kuongeza kodi zifuatazo;

i. VAT kwenye huduma zote za utalii.

ii. Kuongeza tozo kwenye Mafuta ya Petroli ,Diseli na Mafuta ya Taa
iii. Kodi kwenye miamala ya simu.

iv. Kodi kwenye miamala yote ya Benki
v. Kodi ya mapato katika hisa au hati fungani zitakazokuwa katika DSM stock market.

vi. Kuongeza viwango vya usajili wa magari kutoka shilingi 150,00 hadi shilingi 250,000 kwa kila gari

vii. Kuongeza viwango vya usajili wa pikipiki kutoka shilingi 45,000 hadi shilingi 95,000 kwa kila pikipiki
Swali la msingi la kujiuliza ni je hili ongezeko la makusanyo ya serikali limeweza kuwanufaisha vipi wananchi?
Maswali yafyatayo yanahitaji majibu:

a. Serikali ambayo inajitapa kuwa imeongeza makusanyo ya mapato yake mbona imeshindwa kuwapandisha madaraja na kuwaongezea Mishahara wafanyakazi wake tangu iingie madarakani?

b. Serikali iliyoongeza makusanyo ya mapato yake mbona imeshindwa kuajiri watumishi wapya tangu ilipoingia madarakani? Na hata waliopo bado imeshindwa kuwalipa madeni yao?

c. Mbona serikali imeshindwa kuwalipa wazabuni wa ndani na wengine wanafilisika kutokana na serikali kushindwa kuwalipa kwa wakati?

d. Kama kweli makusanyo yameongezeka kwa kiwango hicho kwa mwezi na serikali haijaajiri wafanyakazi wapya badala yake imewaondoa zaidi ya wafanyakazi 10,000 kwa hoja za vyeti feki , imepunguza safari za ndani na nje, imekuja na hoja ya kubana matumizi, mbona deni la taifa linaongezeka mara dufu ? Haya makusanyo ya nyongeza yanakwenda wapi?

#04 Kwamba kwa mujibu wa Farihisi ya Uwekezaji Afrika iliyotolewa na QUANTUM GLOBAL RESEARCH LAB ya Uingereza ya mwaka huu Tanzania ni ya kwanza katika EAC kwa kuvutia wawekezaji.

JIBU: Kwenye hili serikali imeendelea kusema uongo na au kupotosha umma kwa makusudi , kwani kwa mujibu wa taarifa hiyo ya mwezi Mei, 2017 ukurasa wa 15 &16 nchi za Afrika zimeorodheshwa na Tanzania sio ya kwanza kwa upande wa Afrika Mashariki bali ni ya pili baada ya Kenya. Tanzania ni ya 5 wakati Kenya ni ya 2 na Uganda ni ya 6 katika kuvutia wawekezaji Afrika.

Sababu kubwa iliyoifanya Tanzania na Uganda kuwa katika nafasi za juu zilizotolewa na Farahisi hiyo ni kutokana na ugunduzi wa mafuta na gesi uliogundulika katika nchi hizi.

#05 Kwamba Julai ,2016 hadi Machi ,2017 biashara 7,277 zilifungwa , hata hivyo katika kipindi hicho biashara mpya 224,738 zilisajiliwa.

JIBU : Serikali imekiri kuwa ni kweli sekta binafsi inaangamia kama ambavyo tulisema kwenye tamko letu na hiki ni kiashiria kuwa uchumi umetikiswa , lakini serikali inajificha kuwa kuna biashara zimesajiliwa ila haisemi kama zimeanza . Unaweza ukasajili biashara lakini ikashindikana kuanza operations .Serikali ituambie ni aina gani ya biashara zilizosajiliwa na zilizofungwa maana unaweza kukuta zilizosajiliwa thamani yake ni robo ya zilizofungwa , kwani hata Baba na Mama lishe wanatakiwa kusajili biashara zao siku hizi.

#06 Kwamba bajeti ya wizara ya Afya imeongezeka na hasa kwenye dawa kutoka Bilioni 30 mwaka 2015/16 hadi bilioni 251 kwa mwaka 2016/17

JIBU : Kwa mujibu wa taarifa za wizara ya afya zilizowasilishwa kwenye kamati ya Bunge (Randama) Mpaka mwezi Machi 2017, wizara ilikuwa imepokea shilingi 314.673 Bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo kiasi ambacho ni sawa na asilimia 40 tu ya fedha zote zilizokuwa zimetengwa na Bunge.
Kwa hiyo hoja sio kiwango kilichopitishwa kwenye bajeti bali ni kiasi gani halisi kilifikishwa wizarani ? Je ? kuna uhakika gani kuwa zilizotengwa sasa zitapelekwa?

#07 Kwamba miradi ya Kinyerezi I imeshakamilika na Kinyerezi II utakamilika mwakani.

JIBU: Miradi yote hii ilianzishwa na serikali ya awamu ya nne na fedha zake zilitafutwa wakati huo na mikataba yake ilisainiwa wakati huo, kwa mfano mradi wa Kinyerezi I tulichukua mkopo kutoka African Development Bank (ADB) wa shilingi Bilioni 400 na ulizinduliwa tarehe 23 Octoba, 2015
Kinyerezi II mradi utagharimu jumla ya dola za Marekani 334 milioni na unagharimiwa kwa asilimia 85 za mkopo kutoka serikali ya Japani na asilimia 15 kutoka serikali ya Tanzania.

Mkataba wa mkopo kutoka Benki ya SMBC na JIBIC ulisainiwa Machi,2015. Kinyerezi III &IV miradi hii miwili inafanywa kwa ubia (PPP) baina ya TANESCO na Makampuni kutoka China.

#08 Kwamba mikopo elimu ya Juu mwaka 2016/17 zilitengwa shilingi bilioni 483 na bajeti ya sasa 2017/2018 zimetengwa shilingi Bilioni 427.

JIBU:Hapa naipa serikali pongezi kwa ujasiri wa kukiri kuwa Mikopo elimu ya juu imepungua wakati idadi ya wanafunzi wahitaji imeongezeka.

Serikali inaposhindwa kugharimia elimu ya vijana wake na wakati huo inasema uchumi umeimarika haiwezi kueleweka , maana kipaumbele cha nchi maskini ni kuwekeza katika elimu ili ipate wataalamu wa kutosha kuwakwamua katika umaskini huo.

Tusitegemee Rasilimali za asili tu bali lazima sasa tuwekezekwenye elimu ili tuweze kuuza huduma .

#09 Kwamba Tanzania ni imara ,yenye amani na furaha tele.

JIBU: Inawezekana kabisa kuwa picha iliyowekwa ya marais wastaafu pamoja na rais wa sasa ndio wenye furaha lakini wananchi hawana furaha kwa sababu hawawezi kununua chakula kwa ajili yao na familia zao .
Tunaitaka serikali ijibu hoja na sio kuibua hoja zake yenyewe na kuanza kujijibu na bila haya wanakosea hata kujibu hoja zao wenyewe.

*Hitimisho*

Bila uwepo wa demokrasia na utawala wa sheria uchumi utazidi kuyumba .Uchumi wa zama hizi (Kibepari) kamwe hauwezi kuendeshwa kwa matamko ya viongozi na wateuliwa wao.

Bunge ni lazima liisimamie serikali kuu na Halimashauri zipewe mamlaka kamili ya kusimamia maeneo yao bila kuingiliwa na serikali kuu.

Limetolewa leo tarehe 02 Agosti, 2017

……………
Halima James Mdee (MB)
Waziri Kivuli wa Mipango, Fedha na Uchumi.
 
Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe (Chadema) amesema hoja zilizotolewa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazijajibiwa na Msemaji wa Serikali, Dk Hussein Abbas badala yake anatoa takwimu za uongo.

Waziri Kivuli wa Mipango, Fedha na Uchumi, Halima Mdee ameitaka Serikali kujibu hoja kuhusu kuporomoka kwa uchumi katika utawala wa Rais John Magufuli badala ya kuwadanganya wananchi.

Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe (Chadema) amesema hoja zilizotolewa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazijajibiwa na Msemaji wa Serikali, Dk Hussein Abbas badala yake anatoa takwimu za uongo.

Amebainisha hoja mbalimbali zinazohitaji majibu kuwa ni Serikali kueleza kwanini kilimo kimeporomoka na itoe mpango mkakati wa kuinua kilimo nchini.

Pia, amehoji kushuka kwa uchumi wa benki ambazo hazitoi mikopo kwa wafanyabiashara.
"Tulichokuwa tunakizungumza juzi ndiyo hicho wamekizungumza jana watu wa TPSF. Serikali imeondoa fedha zake kwenye benki za biashara na kwenda kuzifungia BOT. Huku kwenye mzunguko hakuna hela," amesema.

Hata hivyo, Mdee amesema katika bajeti ya mwaka 2017/18, Serikali inatarajia kukopa Sh7 trilioni, mkopo wa ndani ukiwa ni Sh6 trilioni na mkopo wa nje Sh1 trilioni.
"Serikali hii ambayo haizisaidii benki zake zichanue, ndiyo hiyo hiyo inategemea kukopa Sh6 trilioni kwenye benki hizo hizo," amesema Mdee.
Source: Mwananchi
 
Nimekuelewa ufafanuzi wako Waziri Kivuli wa Fedha Mh. Halima Mdee (Mbunge CHADEMA), maana yale maelezo ya Msemaji Mkuu wa Serikali kwa wahariri wa vyombo vya habari yalikuwa ya jumla jumla sana na wala manufaa yake hayaonekani ktk mifuko ya wananchi mtaani na vijijini.

Pia pongezi kwa vyombo vya habari kujitokeza kumsikiliza waziri kivuli maana naona ''mic '' zimejazana mithili ya press conference ya kimataifa.
 
Kwa wenzetu topiki za aina hii hujadiliwa kwenye vyombo vya habari na wasemaji kutoka vyama vyote na hata wasio na vyama.

Kumuachia msemaji wa chama kimoja aseme halafu anataka msemaji wa serikali ajibu ndio mwanzo wa vurugu. Yaani hapo nimebaki hoi. Mtu kajiita waziri kivuli. Anawashukuru vyombo vya habari kumfikishia ujumbe. Sasa hiki ni kikao cha bunge, ni kampeni ya uchaguzi au ni kitimutimu cha upinzani na serikali?

CNN, MSNBC, FOX, na wengineo hawaishiwi habari kwa sababu topiki za namna hii wanazirusha na wanapata maoni ya wasemaji bila ya vurugu za kitaifa.

Mambo mengine ya Tanzania ni ya Tanzania. Sijawahi kusikia popote duniani waziri kivuli akihutubia taifa.



Tatizo lako liko wapi haswa mkuu? Ungekuwa unafahamu maana ya multiparty democracy isingekupa shida kuelewa kwanini waziri wa fedha kivuli anaweza kuhutubia taifa. Kwa taarifa yako, ni Afrika yetu hii ambako watu walioko upinzani wanaonekana hawana mchango, lakini kwa nchi za wenzetu ungekuta timu ya wachumi wa serikali wamejaa hapo kuchukua hoja ili kuandaa taarifa ya kujibu hizo hoja.

Njoo sikiliza majibu yatakayotolewa hapo, hayatawiana na hoja alizotoa Halima. Hii yote inatokana na kutokuelewa. Ndo maana watu wako busy kupambana na kina Maalim na siyo kutengeneza hoja zenye kujenga. Nimefurahia strategy ya upinzani sasa hivi, kupiga pale pale mpaka majibu yatoke. Majibu yanayoakisi hali halisi.
 
Hamna lolote...
Magufuli wanamsakama tu kwa kuwa ameua mtandao wa kifisadi...

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchumi ni sayansi, huwezi kuficha ukweli, msishangilie wakati mtumbwi mliopanda unaanza kuzama, mimi binafsi nakiri mkuu ana nia njema, lakini njia anayopitia inaweza isitufikishe katika malengo yetu kama taifa, umefika wakati Wachumi watoe ushauri naye aukubali ili historia imkumbuke

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zen2017
Unaishi dunia gani ndugu yangu?
Manake naona unachanganya mambo tu

Yeye ameita Press kutoa kile alichosema ili kifikishwe alikokusudia.
Hilo unalolisema ni kitu kingine ambacho kinaweza kuitwa mdahalo/malumbano ya hoja n.k na vipindi kama hivyo viko vingi ktk televisio na radio...mada imeandaliwa wahusika wa pande zote wanaitwa kwa kadri itakavuowapendeza waandaaji na kulingana na maudhui waliyokusudia kuyafikisha kwa jamii waliyoikusudia.

Na hivyo vipindi vipo vingi.. Mfano mmoja wapo ni "This week in perspective cha TBC one.
Midahalo ingine kama hiyo inaandaliwa na taasisi mbalimbali kama UDASA n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mdee bana apeleke bangi zake huko,kama anataka majibu yatakayompendeza yeye amenoa,majibu yameshatolewa aache kihere here
 
Lini mlimsikia Hillary Clinton akiita press conference nje ya kampeni za uchaguzi kutoa maoni yake dhidi ya kinachofanywa na serikali?

Muelewe Mdee hata atoe pointi kali vipi CCM watamuona mzushi tu. Na hata aongee pumba vipi CHADEMA watamshangilia.

Ndio maana kwa wenzetu Mdee anaweza kukaa behind the scene akangurumisha topic za upinzani kwenye vyombo vya habari kila siku zikajadiliwa na wananchi wakaelimika bila ya yeye kuonekana mchochezi.

Na hiyo pia hiyo itamuondolea msemaji lawama ya kulaumiwa ikiwa atasema kitu kimakosa.
 
Kama wewe ni upande wa upinzani, ukijua rais atashtakiwa, nchi itapata njaa December au kubana kwake pesa kutauwa biashara, hizo ndio sera zake. Muacheni atekeleze sera zake. Akiharibu si ndio vizuri kwenu. 2020 bado miaka mitatu tu.

Awamu iliyopita pesa nje nje iliitwa ya mafisadi, sasa huyu kabadili staili mwacheni tuone matokeo.

Kama anafanyia pesa ubahili ndio sera zake hizo. Kila rais na sera zake.
Ninachojua mimi hakuna bahili aliyewahi kufa njaa.
 
Na pia msichukulie vitu for granted. Serikali hailazimiki kujibu hii hotuba, especially kama inapojibu inaambiwa majibu hayajaridhisha. Serikali haiwajibiki kwa chama cha upinzani hasa inapokuwa vyama vyenyewe vya upinzani ni vingi.
 
Back
Top Bottom