Hali ya utoaji huduma za afya nchi unatisha

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari ya wakati huu mabibi na mabwana

Kwanza niwape pole na moja kwa moja niende kwenye mada husika.

Leo nimeamka siko sawa ikabidi niende kituo cha afya ili nipate hudumu kidogo. Nikaenda kituo cha afya cha kwanza binafsi nikauliza getini nikaambiwa nichukue namba 159 nikaona uongo nitachelewa.

Nikaenda kituo cha afya cha pili nikapata namba 43 halafu muhudumu anaita namba 27 nikaona hapo sawa. Nikafika mapokezi naambiwa umeme hamna so ni ngumu kutumia NHIF ikabidi niongee na mtu wa mapokezi akakubali kutumia simu yake akajaza taarifa ujumbe ukaja nikasaini nikamaliza.

Kwenda kwa daktari nimekuta wagonjwa 30 huku mm ni wa 43 halafu madaktari wapo 2 yaani kituo cha afya madaktari ni 2.

Nimekaa hadi saa 7 kamili kuanzia saa 3 nikaona bora nikale natoka nje kama mita 300 nakutana ajali ya pikipiki. Nimeenda kula narudi nakuta majeruhi bado hajaanza kupewa huduma vifaa hamna hadi kununua. Vifaa kuletwa dokta mmoja kaenda kuhudumia majeruhi kabaki mmoja.

Hadi mda huu ambao hatujakusanya madaftari tupo 28 na wanazidi kuja. Wengine wamemuona daktari ila dawa hukuna wameondoka. Waliotoka maabara wamerudisha majibu wapo kama 14 na daktari ni mmoja. Hadi mda huu mimi niliyefika saa 3 bado na wa saa 2 bado.

Wagonjwa wanagombana kisa foleni mwenye mgonjwa aliyezidiwa hajapishwa na mgonjwa mwenye unafuu.

Nahili mkalitazame.

MREJESHO
Nimeshindwa kupata rufaa ya kwenda hospitali ya mkoa leo sababu ya kukatika kwa umeme wameshindwa kuverify NHIF card yangu.

Hali ni mbaya
 
Huduma za bima huwa zipo hivyo miaka nenda rudi na ajira wamebana,wataalm wapo tu mitaani hawana ajira
 
Ungetaja basi na hiko kituo
Vipo vituo havina foleni kabisa
 
Back
Top Bottom