Hali ya mtu kuongea peke yake inasababishwa na nini?

Elon J

JF-Expert Member
Sep 30, 2022
630
1,847
Kuna jamaa yangu age yake ni kati ya miaka 29-30, huyu jamaa shida yake muda wote kuongea peke yake tena, muda mwingine Kwa vitendo kabisa.

Yaani huyu jamaa anaweza kuanza kuelezea mipango yake labda anayoenda au anayotaka kuifanya badae kiasi kwamba ukajua kila kitu. Au mnaweza mkawa mmepiga story fulani ukiondoka bado anaendelea kuiongea wakati we ushaondoka🤣

Na jamaa kiakili yuko poa kabisa. Hana tatizo lolote la akili. Sasa wataalamu hii hali Inatokana na nini hasa?
 
Anaongea na majini
 
Na jamaa kiakili yuko poa kabisa. Hana tatizo lolote la akili.
Umenichekesha sana mkuu. Eti hana tatizo lo lote la akili wakati anajiongelesha peke yake tena wakati mwingine kwa vitendo kabisa...😁😁😁

Shida yetu huwa tunadhani kuwa mtu kuwa na tatizo la akili ni mpaka atembee uchi, aokote makopo au aokoteze chakula kwenye majalala. Kwenye ishu ya mental health yaani bado tuko nyuma mno...mpaka pale mtu akifanya mambo ya ajabu ndo utasikia "mbona jamaa alikuwa poa tu" ....

Akienda hospital naamini tatizo lake litagundulika na anaweza kusaidiwa maana huko anakoelekea sidhani kama ni kwema.

Screenshot_20230625_144300_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom