Hali ya mazingira ya uuzaji wa chakula katika maeneo mengi ya Stendi ni hatarishi kwa afya

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Salaam Wakuu,

Katika maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii kama vile stendi na hospitali ni kawaida mazingira hayo kuzungukwa na biashara mbalimbali za vyakula.

Maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam hasa msimu huu wa mvua kumekuwa na uchafu uliokithiri maeneo ya vituo vya daladala.

Hali hii ya uchafu imeharibu mazingira mengi ya vituo vya barabara na kusababisha muonekano wa wafanyabiashara wa chakula kutia kinyaa na kuhatarisha afya za walaji wa vyakula hivi.

Hivyo, nalitumia jukwaa hili kuomba mamlaka na wahusika wakiwamo Mabwana na Bibi Afya kupita na kusimamia usafi katika maeneo yote ya uuzaji wa chakula nchi ili kulinda afya za Watanzania kwa kuepusha magonjwa ya kipindupindu na homa za matumbo.

Pia nawashauri wanunuaji wa chakula kutumia nafasi zao kusisitiza usafi wa mazingira katika maeneo wanayonunulia vyakula.

1683785213127.png

1683784936557.png

Picha: Sehemu ya chakula Mwenge Stendi

1683785025903.png

Picha: Sehemu ya chakula Kawe Stendi

Picha hizo juu nimezipiga leo Asubuhi (11/05/2023) maeneo ya Mwenge na Kawe.

Nawasilisha.
 
View attachment 2617461

View attachment 2617457
Picha: Sehemu ya chakula Mwenge Stendi

View attachment 2617459
Picha: Sehemu ya chakula Kawe Stendi

Picha hizo juu nimezipiga leo Asubuhi (11/05/2023) maeneo ya Mwenge na Kawe.

Nawasilisha.
Wahusika na walione
 
Back
Top Bottom