Mdau
JF-Expert Member
- Mar 29, 2008
- 1,789
- 470
Wadau, hali ya kiuchumi ni tete kwa sasa, na inavyoonekana, baada ya uchaguzi hali itakua mbaya zaidi..hii inatokana na pesa nyingi kuhamishiwa kwenye shughuli za uchaguzi na matumizi mengine yasiyo ya lazima lakini yanayoendana na uchaguzi...kwa mfano;
1. Baadhi ya wafanyakazi wa serikali (hasa walimu) wamekatwa pesa katika mishahara ya ya mwezi Septemba, walipolalamika, wameambiwa ni (makosa?) ya mfumo wa kibenki, watarekebeshiwa mwezi Oktoba..
2. Wanafunzi wapya na wa zamani watakaojiunga vyuo vya elimu ya juu mwezi November hawana uhakika wa kupata mkopo katika semesta ya kwanza ya masomo yao, hili nimedhibitishiwa na baadhi ya wahusika Bodi ya mkopo...
3. Mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula hauonyeshi kupungua makali katika kipindi cha miezi 6 iliyopita...
4. Fedha ambazo wizara na taasisi mbalimbali hupewa kwa matumizi zimepunguzwa/kukatwa katika rate ambayo haijapata kutokea...
5. Taasisi mbalimbali zimeamriwa kupeleka pesa zilikuwa zimepangwa kwa matumizi yao hazina ili ziingizwe katika kampeni...
Dalili hizi si njema kabisa, jitihada za makusudi zinatakiwa kufanywa, ama sivyo nchi yaweza tumbukia ktk matatizo makubwa zaidi...
/